Dr. SLAA sasa atoa facts suala la CCM & silaha, amvaa Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. SLAA sasa atoa facts suala la CCM & silaha, amvaa Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Aug 22, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Wakuu

  Jana Jumanne, timu kadhaa zinazounda timu moja ya Operesheni Sangara-M4C ilikuwa inamalizia kiporo cha Mvomero, ambako kabla ya mapumziko ya siku mbili kwa ajili ya Siku Kuu ya Eid-El-Fitr, kata kadhaa zilibaki katika mashambulizi makali ya Jumamosi. Mashambuzi hayo yamemng'oa Amos Makalla kutoka huko Dar es Salaam kuja jimboni kusalimia wananchi! Anakumbuka shuka kumekucha...

  Katika mikutano aliyofanya jana na timu yake, Dkt. Slaa alitoa more facts juu ya zile tuhuma nzito alizotoa juzi kwenye press conference kuwa CCM wamekuwa wakiingiza nchini silaha bila vibali wala kulipia leseni, kisha wanawapatia vijana wao wanaowekwa kwenye makambi mbalimbali (kama ile ya Ulemo, Iramba, Singida, wakati wa uchaguzi mdogo Igunga) ambayo hutumika kuandaa na kufundisha vijana kwa ajili ya kufanya utekaji, utesaji na hata kuua...

  Katika hatua ya mbele zaidi, amesisitiza kuwa kama ambavyo hawajawahi kuchomoka katika mtego mwingine wowote ule hasa katika masuala ya ufisadi na kuhujumu maendeleo ya watu wa nchi hii, katika hili la kuingiza silaha nchini kwa nia ya kudhibiti CHADEMA na kudhuru viongozi wake (wapinzani wao wa kisiasa) "CCM hawatachomoka pia".

  "Kwa hili pia CCM hawachomoki, wamo kwenye mtego wetu tena kwa mara nyingine, leo naanza kwa kutoa kidogo tu, wakiendelea kuja na maneno matupu nitatoa facts na nyaraka zingine zaidi, na sasa katika hatua hii suala hili linamhusu Kikwete akiwa kama Mwenyekiti wa CCM na Amiri Jeshi Mkuu, ndiye anayehusika na masuala haya, afanyie kazi suala hili ili Watanzania wapate majibu ya kina na ukweli.

  "Wakati wa uchaguzi mdogo Igunga waliweka vijana kwenye makambi kama pale Ulemo, Iramba mkoani Singida, wakifundishwa mbinu za kuteka, kutesa na kuua, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya CCM kudhibiti wapinzani wao kisiasa, wakilenga CHADEMA na hasa kudhuru viongozi wake. Waliwapatia bunduki, mojawapo ni silaha iliyotengenezwa China, yenye uwezo wa kubeba risasi 8 kwenye magazine yenye namba J137, walikuwa nayo vijana hao kambini.

  "Tunamtaka Kikwete, kama Amiri Jeshi Mkuu na pia akiwa Mwenyekiti wa CCM atuambie, silaha hii iliingiaje nchini na kwa nini ilikuwa mikononi mwa CCM, tutashusha nondo zaidi, kuendelea kuivua nguo CCM na mikakati ya kumaliza wananchi wa nchi hii wasiokuwa na hatia," alisema Dkt. Slaa katika vijiji mbalimbali vya Kata za Langali na Mlali, Mvomero, Morogoro.
   
 2. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  longa mkuu longa, tumsubiri Nape na majibu yake hovyo
   
 3. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Inakuwa vigumu kuamini hizo tuuma ama ni propaganda.
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na Dr Slaa kwa 100%. CCM wamekuwa AL QAEDA mno !
   
 5. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na bado mengi yatafichuliwa ifikapo 2015 . Halita salia jiwe juu ya jiwe.
   
 6. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Labda hao ndio baadhi ya wahuni walioshiriki kumteka Dr. Ulimboka. Aibu kubwa kwa CCM kuanzisha kundi la kigaidi chini ya ulezi wa Mwigulu.
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Akimaliza muhula wake tumpeleke Kikwete moja kwa moja The Hague.
   
 8. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani kama ni kweli hiyo ni kashfa nzito sana kwa taifa letu, lakini kama siyo ni hatari pia! Ni muhimu vyombo vya usalama vikachunguza!
   
 9. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Nape anachezea moto natamani aendelee kuchemka wanaume wamshukie boss wake mazima. Nape jana kabeep leo Dr kapiga simu.

  Nape atuamnbie je hiyo bunduki waliitoa wapi na nani aliisajili kwa nini ilikwenda kwenye makambi yao. Nape akumbuke alikubali kuwa huwa CCM wana makambi ya kufundisha vijana wao vita na kuteka sasa aseme bunduki za nini wakati kuna polisi, mgambo, nk na kama wanahitaji bunduki kwanini wasisajili wakati ni ruksa mtu kumiliki silaha???

  Nape akumbuke CCM wameteka, wameua na wanatoa kauli chafu na za dharau kama zile za Igunga sasa wanalia.
  Mahakama zikifanya kazi vizuri Tanzania tutaheshimiana na wehu watapungua.
   
 10. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Bunduki za nini?
  Mbona yeye alikamatwa na mbili mfukoni kule Arusha?
  Hivi ile kesi iliishia wapi?
   
 11. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Endelea kuwa Tomaso lkn umeshatajiwa na namba ya silaha husika J137, na Kikwete ndio mdau mkuu namba1.
   
 12. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawatachunguza kwa7bu watajiumbua wao wenyewe.
   
 13. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  CCM au Chama Cha Mafioso wamekuwa wakifanya vitu bila kujali kuwa kuna kubadilika kwa wakati. Ule mfumo uliowazaa na kuwapa kiburi wa chama kimoja ulishakufa ingawa wao wanadhani bado uko hai. Heri wangekuwa na akili wakatumia japo moja ya common sense wangejifunza kilichojiri Kenya mwaka 2002 KANU ilipodondoshwa na kufurushwa madarakani. Kwa vile CCM ni Chama Cha Mafedhuli hawana uwezo wa kujifunza hadi yawakute.
   
 14. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mbona hapa kuna upuuzi mtupu.
  Andiko lote haluna fact hata moja kusubstantiate hizi serious allegations.

  Ndo matatizo ya monologue, wanakijiji watshangilia tu Dr Slaa.
  Leo akija mtu akasema CDM wameficha mabomu sehemu fulani kwa kujiandaa na uchaguzi , bila vielelezo si mtaamini ? Au siyo
   
 15. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alikutwa bastola halali anayoimiliki kisheria, kila kitu kipo wazi. Wekeni wazi na nyie hiyo silaha namba J137 yenye risasi 8.
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Album mpya ya chadema ni "bubu". Tutasema, tutataja.

  Na kuna misukule inashangilia, wanafanywa kama kama watoto wa kuku, "mtanyonya kesho".
   
 17. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wewe usiwe mtumwa wa mawazo namba ya siraha (bunduki) iko hapo waitolee ufafanuzu wala sio siasa
   
 18. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ni zake na anazimiliki kihalali na sheria inamruhusu,Una swali jingine?
   
 19. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hili zito na kubwa!
   
 20. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Ni mtu mjinga mjinga tu anaweza kuamini hii trend of thoughts, kuwa silaha moja ndo ina wawinda viongozi wa CDM wakati mwenyewe DrSlaa alikutwa ana mbili!

  Wakuu April Fools day ilishapita!
   
Loading...