Dr. Slaa: Natishwa

Dr. Slaa: Natishwa

Dk amesema anatishwa yeye na familia yake. Akielezea amezidi kusema kama ni mapenzi ya mungu yatimizwe mimi sitang"ang'ania.

Chanzo: Rfa magazeti/RAIA TANZANIA.

Hata mimi na familia yangu tunatishwa na gazeti la Raia Tanzania.
 
Huyu dr slaa kuna jambo,kwanin hajtokezi,ama na yeye anataka umaarufu,lakini chadema bwan kwisha matusi yote yale kw lowassa kwa sasa amekuwa lulu nimewadharau,mna tamaa hamuwezi kulinda laslimali za nchi nyie chadema na ukawa yenu,hamna maana kwetu watanzania wa kawaida

Ccm na mamlaka ya juu ndio wanao linda rasilimali za nchi !!!???.subiri tunakuletea kipaumbile cha kwanza elimu .cha pili elimu na cha tatu elimu .utaelewe tuuu
 
Bahati mbaya au nzuri MKUBWA huyo (ETI) nasikia aliwahi kuwachunga kondoo wa BWANA, kama nilikweli chonde chonde zingatia maneno ya bwana wako.....ASIYE NA DHAMBI AWE WA KWANZA KUMTUPIA JIWE....mwisho wa kunukuu!
 
Anatishwa Na Simba Kwenye Ndoto Au Ni Majini Yanamwijia Ndotoni? Hebu Tononeka Vizuri Nasisi Tujue Anatishwa Na Nini Mkuu?
 
Kova kova kova, usipuuze taarifa hizi, haiwezekani kwa wiki sasa slaa hajaonekana hadharani.
 
Raia Tanzania ni kijalida cha ccm! Ingawa mmiliki ni jenerali Ulimwengu lkn nashangaa saaanaa

Ha ha magwanda bwana mnachekesha sana,jenerali akiandika habari za kyichamva ccm mnamuona anafaa,akiandika habari za kweli kuhusu chandimu mnaanza oooh huyu anatumiwa,hivi kwa akili yenu mlidhani slaa atamkubali lowassa?
 
Ha ha magwanda bwana mnachekesha sana,jeneral8 akiandika habari za kyichamva ccm mnamuona anafaa,akiandika habari za kweli k7husu chandimu mnaanza oooh huyu anatumiwa,hivi kwa akul8 mlidhani slaa atamkubali lowassa?

Tulia dawa imeaza kudanya kazi
 
Mhuu kweli huyu lowasa katikisa nchi media zote ziko na lowasa na slaa tu sasa ccm cjui itakuaje?
 
DSC09963.jpg
 
tusijipe moyo mazee docta anazingua, anaturudisha nyuma.

.....hali sio shwari, hata kama atajitokeza ila kuna shida kwani hata Mabere Marandu amesema ni kujidanganya kama watasema kila kitu ni sawa wakati katibu mkuu watu hawamwoni na wenzake.
 
.....hali sio shwari, hata kama atajitokeza ila kuna shida kwani hata Mabere Marandu amesema ni kujidanganya kama watasema kila kitu ni sawa wakati katibu mkuu watu hawamwoni na wenzake.

Nafurahishwa na jinsi Dr Slaa alivyogeuka ghafla Kuwa kipenzi cha ccm na wana ccm,najiuliza ikitokea chadema wakampitisha kugombea urais mnapenz haya yataendelea ?au kwa uroho wa madaraka mliona atarudi Kuwa adui

...mkuu kabla magamba hawajakujibu wewe wajibu kwanza kuwa EL asingekatwa mngesema ni msafi. Mihemko ya kisiasa isiwafanye mkawa vipofu, nyani haoni ku***le.
 
Chadema hatumtegemei dr slaa asepe fasta,,hana jipya msaliti makamanda tusonge mbele...
 
Nimegundua chadema wanaweweseka sana, kama Dr. Slaaa haonekani na mmepata mtambo wa kweli kifedha ss Dr. Slaa wa nn? make kaonekana hafai mawazo yake yamepuuzwa na kaamua kukaa penbeni, shida iko wapi? Dr. Slaa anajitambua vema na ndo mpinzani wa kweli, yani awekwe mtu ambaye hafai alafu yy ashabikie, hayo yanafanywa na watu ambao wakati mwingine si makini. Na je kama ni muhimu sana, mbona kawekewa mtambo Lowasa? Lakini nina imani tutafika kwa siasa za bongo.
 
CHADEMA WASIPOCHUKUA HATUA DHIDI YA GAZETI HILI NITAWASHANGAA SANA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, ambaye tayari amekwishakujivua uanachama wa chama hicho, amesema maisha yake binafsi pamoja na ya familia yake sasa yapo hatarini.


Hatua hiyo ya Dk. Slaa kufichua hatari hiyo inayomkabili dhidi ya maisha yake aliiweka bayana mwishoni mwa wiki katika mawasiliano yake na chumba cha habari cha Kampuni ya Raia Mwema Ltd, inayochapisha gazeti la kila wiki la Raia Mwema na gazeti hili la Raia Tanzania, linalochapishwa kila siku.

Slaa alilieleza Raia Tanzania kwamba kuna juhudi kubwa zinazofanywa na watu ambao hakuwa tayari kuwataja, akisema juhudi hizo zinalenga kutengeneza mizengwe ya kila aina na kisha kumdhuru, lakini hata hivyo, akisema haogopi chochote na kama ni "Mapenzi ya Mungu yatimizwe."
"Ni dhahiri ninatengenezewa mizengwe ya kila aina. Inaonekana maisha yangu na ya familia yangu sasa yako hatarini. Nimekuambia (mwandishi wa gazeti hili) ili ikitokea chochote ujue siyo bahati mbaya. Sijawahi kuogopa na wala sitaogopa. Mtetezi wangu ni Mungu aliyehai na nina hakika atanilinda kama yanayopangwa siyo mapenzi yake. Kama ni mapenzi yake yatimie na isiwe kama ninavyotaka mimi," alisema Dk. Slaa.

Ilivyokuwa kujivua uanachama
Maisha ya Dk. Slaa yapo hatarini ikiwa ni takriban wiki moja tangu ajiuzulu wadhifa wake wa Katibu Mkuu Chadema na kisha kujivua uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Katika uamuzi wake wa kujiuzulu na kisha kujivua uanachama, Dk. Slaa pia aliweka bayana kwamba anastaafu shughuli za kisiasa, akifanya hivyo kutokana na uongozi wa juu wa Chadema kumkaribisha "kwa mizengwe" ndani ya chama hicho aliyekuwa kada wa CCM, Edward Lowassa, ambaye sasa ndiye mgombea wao pekee wa urais.

Dk. Slaa hakubaliani na namna Lowassa alivyokaribishwa Chadema bila kufuata utaratibu waliokubaliana ndani ya vikao vya chama hicho.

Taarifa ambazo gazeti hili lilizipata wiki iliyopita zinasema, miongoni mwa mali za Chadema ambazo Dk. Slaa alizirejesha baada ya uamuzi wake wa kujiuzulu na kujivua uanachama, ni pamoja na gari alilokuwa akitumia kwa nafasi yake ya Katibu Mkuu. Mbali na gari hilo, alirejesha pia nyaraka nyingine za chama hicho.

Raia Tanzania lilipata taarifa za kurejeshwa kwa mali hizo za Chadema na kupiga kambi Ijumaa iliyopita, maeneo ya Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam hadi liliposhuhudia tukio hilo la kihistoria.

Majira ya saa 3.15 hivi, gari aina ya Noah lenye namba za usajili T 217 BUZ liliingia katika Ofisi za Chadema likiwa na watu wawili na gazeti hili liliwashuhudia wakiteremka na mkoba mwekundu na kisha kuingia ofisini.

Wakati huo nje ya ofisi, kulikuwapo pikipiki moja iliyokuwa ikizunguka Mtaa wa Ufipa kana kwamba inafanya doria.
Baada ya muda mfupi, saa 3:20 hivi, watu hao walitoka nje ya Ofisi ya Chadema wakiwa mikono mitupu, wakaingia kwenye gari lao na kuondoka eneo la Ufipa. Raia Tanzania lilishuhudia pikipiki hiyo iliyokuwa ikifanya doria ikiingizwa ofisini humo muda mfupi baadaye.

Kuhusu kurudisha kadi yake ya uanachama wa Chadema Ijumaa usiku, Dk. Slaa aliliambia Raia Tanzania akisema: "Sikuwahi kurudisha kadi ya CCM, kwa nini nirudishe kadi ya Chadema? Kadi ni mali yangu na hili nimekuwa nikilieleza mara kwa mara."
Mbali na kauli hiyo ya Slaa, moja ya vyanzo vyetu vya habari kutoka Makao Makuu Chadema kilieleza; "Hilo sasa ni suala ambalo confirmed (ni rasmi). Dk. Slaa amejivua nafasi yake ya Ukatibu Mkuu na kujivua pia uanachama wa Chadema. Amekerwa na namna mambo yalivyofanyika hovyo, bila kujali misingi ya utawala na maadili katika chama."
Dk. Slaa aliacha uanachama wa CCM na kuingia Chadema mwaka 1995 baada ya kutoridhishwa na mchakato wa kusaka wabunge ndani ya chama hicho.

Mwaka huo 1995 alishinda ubunge kupitia Chadema na kudumu bungeni hadi mwaka 2010 alipogombea urais na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Jakaya Kikwete, huku matokeo ya kura za urais yakigubikwa na tuhuma za uchakachuaji.

Tangu gazeti hili lilipoweka hadharani wiki iliyopita ukweli kwamba mwanasiasa huyo anayekubalika zaidi nchini ameacha nafasi ya Katibu Mkuu wa Chadema, kumekuwa na uzushi mwingi katika mitandao ya kijamii nchini.

Uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wake Chadema kwa kutoridhishwa na kupokewa kwa Lowassa kwenye chama hicho bila masharti, umefuatiwa na juhudi kubwa kutoka kwa watu mbalimbali kukanusha taarifa hizo kwa malengo ambayo hayajaeleweka wazi, lakini Ijumaa Dk. Slaa aliliambia Raia Tanzania kwamba ameamua kukaa kimya na kutojibizana na watu hao, asije akawa kama wao.

"Nimezoea kusimamia maadili ninayoyaamini. Nimeheshimu na kutii dhamira yangu daima kwa kuwa naamini Mungu huzungumza nasi kupitia dhamira zetu ndiyo maana binadamu tuko tofauti na viumbe wengine. Watasema mengi, propaganda daima hazijengi," alisema Dk. Slaa na kuongeza:

"Wanaotumia propaganda kuhalalisha uamuzi mbovu, hawajui madhara wanayoyasababisha.

"Nitakuwa sina tofauti na wao nikipoteza muda kujibu kila kinachoandikwa kwenye mitandao. Nakuhakikishia sitakwenda chama kingine, bali nimestaafu siasa ili nitumikie taifa langu kwa njia nyingine," alimwambia mwandishi wetu.

Akizungumzia taarifa zilizozagaa kwamba angezungumza na waandishi wa habari, Dk. Slaa aliliambia Raia Tanzania kwa kifupi: "Sina mpango huo, sina papara, najua kuna mengi yatasemwa. Wakati ukifika nitayazungumzia."

Kutokana na uamuzi huo wa Dk. Slaa ni dhahiri sasa Chadema kinakabiliwa na wakati mgumu wa kusaka mrithi wa Katibu Mkuu huyo wa zamani aliyekuwa amekifikisha chama hicho katika kilele cha siasa Tanzania, na tayari watu wa karibu na Lowassa wameanza kujipanga kwa ajili ya kuinasa nafasi hiyo ya Katibu Mkuu.


 
Back
Top Bottom