Dr Slaa na Zanzibar

Kwailo hata mimi naona chadema wanatakiwa wakazebuti upande wa zanzibar ambao bado hawaja julikana sana
 
Kwa mkakati uliopo ni kwamba cdm watakuja zanzibar baada ya kumaliza operation sangara katika kanda tano za huku bara na kazi itakuja kufanyika kwa wiki mbili mfululizo huko pemba na unguja kwa maana kazi aliyopewa maalimu seif sasa imezorota kidogo baada ya uchakachuaji wa cuf kuwa ccm b.

Go cdm go, hakuna dini wala kabila kwenye swala la maendeleo hivyo wazanzibari msihofu chadema hiyoooooo inakuja na mtaipenda tu.

Hakuna kulala mpaka kieleweke!!!!!!!!!!!!!!.
 

Inakuwaje nchi mbili zinaungana halafu moja inakufa moja inabaki. Ndio maana hata vyama vilivyopo havina mtazamo mzuri kuhusu Tanganyika na Zanzibar. Mfano; Tanganyika hakuna muafaka. Mombo hovyo tu, hapa suala ni katiba.:wink2:
 
Wako katika mchakato wa kupata vibali vya kwenda huko. Mpaka jana jioni walikuwa wanazungushwa na watu wa uhamiaji. Zanzibar ni nchi nyingine ati.
 
Naona hapana haja ya kumlaumu Dr Slaa kwa hili kwani tunajaribu kudanganyana kujidai kuwa Zanzibar ni sehemu ya Muungano wa Tanzania. Tunasema hivyo kwa lengo moja tu nalo ni kuizuia Zanzibar kujiendeleza kivyake.
Si Dr Slaa tu bali hata Rais wa unaoitwa Muunganmo wa Tanzania haonyeshi kuwa anajali mambo ya Zanzibar. Hotuba zake zote kwa kawaida ni masuala ya Tanganyika. Bunge vile vile mambo yake ni ya Tanganyika na ukweli ni kuwa huu Muungano ni kiini macho tu kwani Tanzania ni Tanganyika na unaposikia jambo linalohusu Zanzibar linazungumzwa basi ni kiini macho. Hata hili la vyama vya siasa ni kiini macho na ndio maana CHADEMA ni chama cha Bara tu.
 


CCm ndo wamejaa udini wa vibarakashekhe + CUF wanatamani iwe nchi ya wavaa misuri.
Hilo swala la udini limeletwa na huyo M-dowans wenu akidhani ataungwa mkono yeye na CDM ichukiwe kumbe sivyo.
 
CCm ndo wamejaa udini wa vibarakashekhe + CUF wanatamani iwe nchi ya wavaa misuri.
Hilo swala la udini limeletwa na huyo M-dowans wenu akidhani ataungwa mkono yeye na CDM ichukiwe kumbe sivyo.

Kwanza tunaita misuli na sio misuri na la pili kwa taarifa yako hilo unalolidai si kero kwa Wazanzibari wenye asilimia 99 waumini wa hiyo dini unayoikejeli.
 
Zanzibar hamna kitu kwani wazanzibari wanajua Karume na Seif walikubaliana nini?
 
Zanziba kwa mujibu wa katiba yao ni nchi kamili sasa na sisi watanganyika tunahitaji Tanganyika yetu na ndio Serikali tatu,Kamuulize na JK ni shughuli gani anazofanya Zanzibar au ccm ya zanzibar unazani ndio ccm ya bara,au cuf ya zanzibar ni sawa na cuf ya bara?hapo kuna tatizo tena kubwa.........Tuacheni na chadema yetu tuacheni na shujaa wetu dr slaa katika ulombozi wa Tanzania kwani hadi hao wazenji fleva watanufaika kwakuwa sie hatuna hiyana kama wao....
 
Wakuu sorry nime lazimika kufuta post ya Jesuit pamoja na zote zilizo mquote. Hii ina tokana na ukweli kwamba Jesuit ana leta uchonganishi. Kwa post zake zilizo pita inaonyesha kabisa ana jichanganya. Kuna post ajidai ni Mkristo na zingine ajidai ni Muislamu ili mradi basi tu kuchonganisha. Endeleeni na mada wakuu.
 

Mkuu pengine Jesuit ni halfcast wa hizo dini mbili..................:wink2:
 
 
Kwa kuwa wazanzibar ni waelewa basi Chadema hakihitaji kuja kutangaza sera huko kwani zimeshaeleweka na kama wameelewa halafu bado hawasikii nakuwa na mashaka na huo uelewa wao,

lakini pia zanzibar ni kama Temeke kwa ukubwa, sioni hata maana ya kuwatembelea maana kila mtaa kuna mbunge na mwakilishi, na hata CUF sioni kwanini hata kilikuwa ni chama kikuu cha upinzani kwa kuwa na viti vingi vya Pemba sehemu amabyo ni ndogo kuliko hata kigamboni!! yaani tulitakiwa tuvipime vyama kwa kuangalia wamepata wabunge toka wapi, huwezi ukawa na wabunge 20 toka Pemba ukamsinda wenye wabunge wanne tuka sehemu nyingine kama kigoma,mwanza, arusha, moshi, na ukitaka kujua kama hiki chama kina udini au ukabila pima kwa kuangalia hata wabunge wake wametoka wapi na je ni wadini mchanagnyiko?

so kwa mtazamo wangu tunapoongelea maswala ya nchi yetu Tanganyika ndio kiini maana hakuna Tanzania kama huna Tanganyika na Zanzibar.
 
Wazanzibari ndio waelewa zaidi? Waelewa wa nini? Kuolewa na CCM ndio uelewa? Laiti mngejua mlivyousaliti upinzani usileta porojo zako hapa.
Dudusssss!!!
 
Wazanzibari ndio waelewa zaidi? Waelewa wa nini? Kuolewa na CCM ndio uelewa? Laiti mngejua mlivyousaliti upinzani usileta porojo zako hapa.

Pole mkuu.
Unajua kuolewa kwa CUF zanzibar ndio imeamsha nchi nzima ? Unajua suala la kuleta mjadala wa katiba na kupata nguvu ni kuowana kwa CUF na CCM Hapa Zanzibar ? sasa jee huoni kuwa huo ni uwelewa mkubwa ? Kwa sababu faida ya matunda ya zanzibar ndio sasa ndio itawafaidisha na tanganyika ?

Hebu pima kwanza kabla hujaongea.
 
Chadema bado ni chama kichanga, hakijajipanga sawa sawa kitaifa, tunawakaribisha Zanzibar
 

Muandishi umeona hapo red ? Mi naweza kusema zanzbar ni part ya jamuhuri ya muungano lakini sio wa tanzania,kwa sababu muungano wa nchi mbili ni ulikuwa unaitwa hivi jamuhuri wa muungano wa tanganyika na zanzibar.

Sasa kilichofanyika ni kwamba tanganyika imeitwa tanzania sawa na kuita zaire CONGO,so unaponiambia ni part ya jamuhuri ya tanzania inamaaa tumo ndani ya tanaganyika.

Ndio maana tumekibadilisha kile kipengele cha katiba kuwa zanzibar n nchi ina mipaka yake ,wengi ya watanganyia wakifahamu na part ya jamuhuri ya tanzania lakini so hivyooo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…