Sijui nimjibu Dr. Slaa?
Mwaka 2011 nikiwa mwanafunzi wa kidato cha sita huko Ihungo boy's high school nikichukua masomo ya HGE niliwahi kuwa kiongozi wa ngazi ya jimbo wa umoja wa wanafunzi wakatoliki yani ( Tanzania Young Catholic Students TYCS)
Nafasi yangu hii ilinifanya niwe karibu na baba padri mmoja ambaya alinipenda nami nilimpenda na ninampenda sana. Alitamani sana niwe kasisi yani Padri nimtumikie Mungu nilitumikie na kanisa pia.
Basi mara zote nilipokuwa nikikutana na baba padri alikuwa akiniuliza juu ya maamuzi yangu ya kwenda seminary baada ya masomo ya high school.
Daima nilimwambia baba padri, baba mimi ninaona sina wito wa kuwa padri ila ninawito wa kumtumikia Mungu na nchi yangu katika siasa. Nikamwambia ninamaono ya kuwa kiongozi katika taifa langu nishirikiane na viongozi wenzangu wa upinzani tuiondoe CCM tulete mabadiliko nchini.
Baba akaniuliza viongozi wapi wa upinzanzi utakaoshirikiana nao kuleta mabadiliko nchini. Jina la kwanza kulitaja lilikuwa la Dr Slaa. Nilijua ili nimshawishi huyu padri basi nianzie jina la mtu ambaye aliwahi kuwa padri kama yeye.
Yule padri aliniambia Dr. Slaa hawezi kuendelea kuwa upinzani mpaka mtakapokuja kuingia ikulu. Nilishtuka sana sana akaniuliza mbona unastuka nikamwambia haiwezekani, akaniambia utayakumbuka maneno yangu.
Nikamuuliza kwa nini, akanijibu akasema mtu akishindwa kutunza maagano ya daima aliyokubaliana na Mungu hawezi kuheshimu maagano aliyowekeana na wanadamu wenzake.
Akaniambia kama hiyo haitoshi mtu aliyefundisha uaminifu mbele ya madhabahu halafu hata baada ya kutoka utawani akaoa mke mmoja akamuacha halafu akachukua mwingine akawa anasema ni mchumba wake wanalala kitanda kimoja na mchumba wake mtu huyu hawezi kuwa mwaminifu kwa chochote.
Kisha akaniambia kabla Mungu hajakuchukua utashuhudia maajabu ya huyo mzee wako hutoamini. Nami nakuombea uzima Mungu akupe maisha uone rangi mbili za mzee wako.
Nayashuhudia mambo niliyoambiwa na baba yangu wa kiroho ningali bado kijana.
So matamshi yake ya hivi karibuni yanayopingana na uharisia wa mambo jinsi ulivyo nchini havitutishi maana sasa tabia yake ya asili inafunuliwa bayana
Wasalaam nyote!