Sasa naamini Wtz wengi tumekuwa ma-mbumbumbu au Mazezeta, hivi tunashindwa kujadili majanga makubwa yaliyopo nchini kwa sasa, tunajadili na kulumbana juu ya imani za dini? ndiyo maana tunaendelea kutawaliwa ki-imla kwani tunawalaumu hao viongozi wakati na sisi tunaonesha matatizo ndiyo yaleyale, hapa tatizo ni Sisi wananchi kuacha ushabiki ili itakapofika fulsa nyingine ya kuwapata viongozi wapya wenye muonekano wa kutujali basi tuwachague. Na swala hapa sio usomi bali Busara, Hekima na kuwajali watu unaowaongoza. Mungu wabariki watanzania wote na uwaondolee roho za chuki uwape amani. Amina