CCM,kwa hiari yake,iliamua kukabidhi kwa serikali ,Chuo cha Kivukoni kilichokuwa na dhima ya kufundisha makada wake nadharia za siasa na uongozi.Tunasimuliwa ,kuwa,wakati huo vijana na makada wake walikuwa ni mahiri katika fani za ujenzi wa hoja za kimantiki tena zilizojengwa katika nadharia na itikadi za Karl Max.
Sasa Kivukoni imekabidhiwa serikalini na wakuu wa chama hawakuona umuhimu wa kuanzisha chuo mbadala kwa makada wake...
Chuo hicho kilikuwa na maana sana wakati wa mageuzi kuliko ilivyokuwa wakati wa ''chama kushika hatamu''.
Matokeo yake watetezi wa CCM,wakiwemo hapa jamvini, wanaanika udumavu wa fikra kwa upotoshaji usiomithilika
Kwa kweli mimi ningeshangaa sana kama wangekuwa wanajenga hoja kisayansi!Sasa ajitokeze mtu anieleze hawa jamaa wanajifunza wapi?Nani anieleze kama chama hicho bado kinao uwezo wa kuwavutia wajenzi mahiri wa hoja kujiunga nacho!Kweli hawa ni kina Pangloss aliowachambua Jenerali Ulimwengu!