Dr. Slaa, Mbowe waweka historia Kilombero!

Sasa wewe huoni CCM inaboresha sera ya uwekezaji kwa wafanyibiashara wadogo kama jamaa yako? Nipe muda nafuturu

Chama
Gongo la mboto DSM
Unakula daku na sio unafuturu wenzako wakina ritz hawaji humu jamvini kipindi hichi cha mwezi wa toba kwa kujua watasema uongo lakini wewe unaganda humu Huku ukisema uongo uliopitiliza heri usingefunga
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amefufua upya sakata la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, akitaka serikali ithibitishe hadharani mtu anayetajwa kuhusika na tukio hilo.

Akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Ifakara, Morogoro jana, ikiwa ni sehemu ya Operesheni Sangara awamu ya pili, Dk. Slaa aliyeambatana na viongozi wakuu wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, alisema kuwa Serikali ya CCM imekuwa na kiburi cha kuwatisha wanaotaka kutetea maslahi ya wananchi.

Alisema kuwa imefikia hata hatua ya wengine kutishiwa vifo, huku akitolea mfano wa kutekwa, kupigwa na kisha kuumizwa Dk.Ulimboka, aliyetendewa unyama huo usiku wa kuamkia Juni 26 katika msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

“Serikali ina nguvu ya kuvifungia vyombo vya habari kwa sheria dhalimu ya magazeti ya mwaka 1977, lakini haitaweza kuzuia midomo ya watu kujadili suala zima la kutekwa huko kwa Dk. Ulimboka,” alisema.
Dk. Slaa ambaye alikuwa akishangiliwa kwa nguvu, aliongeza kuwa, kuanzia sasa CHADEMA itaanzisha mapambano kwa ajili ya kutaka kupata ukweli juu ya aliyemteka Dk. Ulimboka.

Alisema kuwa miongoni mwa simu zilizowasiliana na Dk. Ulimboka ni Ramadhan Ingondhur, aliyetajwa kama mtu wa mwisho kabla ya kutekwa pamoja na namba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Mabwepande, aliyemtaja kwa jina la Abdallah Punja.

“Serikali na Usalama wa Taifa wanapaswa kusimama hadharani na kuuambia umma Ramadhan ni nani na kwanini anahusika na Idara ya Usalama wa Taifa.

“Mimi ni muumini wa Usalama wa Taifa na wala siwaondolei hadhi, lakini kwa mwendo huu ni wao wenyewe ndio wanajiondolea hadhi yao, na sasa wamekaa kufuatilia mikutano ya vyama vya siasa, hususan CHADEMA,” alisema Dk Slaa.

Akizungumza katika mkutano huo, Mbowe alisema umati uliokusanyika unaonesha namna wakazi wa Kilombero walivyomthamini aliyekuwa mbunge wa viti maalumu, marehemu Regia Mtema.
Mbowe aliomba jina la uwanja wa Ifakara libadilishwe na kuitwa Uwanja wa Ukombozi, na kwamba hali hiyo iwe chimbuko la ukombozi kwa Mkoa wa Morogoro.

Aliwataka wakazi wa Kilombero kuacha kulalamika na badala yake wachukue hatua kwa kuachana na CCM na kujinga na CHADEMA.

“Ndugu zangu kila mmoja ana wajibu wa kujiuliza kafanya nini kwa ajili ya nchi yake, watoto wake na anawaandalia nini siku zijazo. Tambueni tupo katika utwala usiowajali na hili jukumu lenu ninyi wananchi kujiondoa katika hali hii na si kazi ya Dk Slaa, Mbowe au Lissu,” alisema.
Mbali na Dk. Slaa na Mbowe, viongozi wengine waliokuwa katika msafara huo ni Joshua Nassar (Arumeru Mashariki), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Hamad Yusuph (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar), Suzan Kiwanga (Viti Maalumu), Joyce Mukya (Viti Maalumu) na wengine wa makao makuu.
Naye Lissu, alisema baada ya kupita kuanzia Mikumi hadi Ifakara, hajui ni kwanini bado wakazi wa wilaya hiyo wanaendelea kuikumbatia CCM huku akishangazwa na kitendo cha wananchi hao kuendelea kutozwa ushuru wa mazao ambao serikali ilikwishaupiga marufuku.

Alisema ufike wakati wananchi wawakatae viongozi wasiochaguliwa kuwa wawakilishi wao kwani wanasimamia masilahi ya waliowateua kama inavyotokea sasa katika maeneo mbalimbali.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Mbilinyi alijibu kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa wapinzani wanapinga maendeleo, akisema kwamba si kweli, kwani wao wanapingana na mipango inayowapa fursa mafisadi kujineemesha, huku wananchi wakiendelea kuogelea katika umasikini.
 
Duh, huyu mzee kumbe bado yupo kwenye ulingo wa siasa? Awaachie tu vijana.

BTW hatuna haja ya kumjadili tena huyu mzee cuz hana jipya tena. Kila siku anakuja na mambo yaliyopita!
 
Unakula daku na sio unafuturu wenzako wakina ritz hawaji humu jamvini kipindi hichi cha mwezi wa toba kwa kujua watasema uongo lakini wewe unaganda humu Huku ukisema uongo uliopitiliza heri usingefunga

Uongo ni pale unaposema kitu ambacho ndani nafsi unajua ukweli unadanganya kama vile Dr. Slaa alipokuwa akimtaja Josephine mke wakati akijua fika ni kimada, mimi natetea ninachoamini ni ukweli mpaka hapo utakonithibitishia vinginevyo na mimi nikubaliane na wewe kwamba huo ni ukweli na baadaye niongee kinyume na ukweli nilioukubali hapo ndio nitakuwa nasema uongo, lingine usiwe na wasiwasi na funga naamini ni swafi na hakuna binadamu yeyote atakae ipima.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Duh, huyu mzee kumbe bado yupo kwenye ulingo wa siasa? Awaachie tu vijana.

BTW hatuna haja ya kumjadili tena huyu mzee cuz hana jipya tena. Kila siku anakuja na mambo yaliyopita!

kama wewe ukiachiwa vipi utamudu kwa hizi pumba zako unazopost kila siku kweli??
 
Rejao nilikuwa nakupa 'respect'
ila kwa hili hapana umeniuzi.

Duh, huyu mzee kumbe bado yupo kwenye ulingo wa siasa? Awaachie tu vijana.

BTW hatuna haja ya kumjadili tena huyu mzee cuz hana jipya tena. Kila siku anakuja na mambo yaliyopita!
 
Duh, huyu mzee kumbe bado yupo kwenye ulingo wa siasa? Awaachie tu vijana.

BTW hatuna haja ya kumjadili tena huyu mzee cuz hana jipya tena. Kila siku anakuja na mambo yaliyopita!

Mke wa Fisadi wewe !
 
Ni Udini wa Ikulu au Serikali nzima ya CCM. Haiingii akilini Mtekwaji ni Dr STEVEN, Watekaji ni AHMED, RAMADHAN na ABEID. Mpelelezi mkuu SULEIMAN KOVA na amri ilitoka kwa Alhaji J.MRISHO.... Nani anabisha kuwa Udini Ulipewa kipaumbele na serikali ya ccm ktk Utekwaji wa Dr STEVEN ULIMBOKA?. Ni nani na kwa ushahidi upi ataweza kuisafisha ccm na kashifa hii ya Udini kwa Dr Steven huku makanisa zaidi ya 26 yamekwisha kuchomwa Znz?.
 
Duh, huyu mzee kumbe bado yupo kwenye ulingo wa siasa? Awaachie tu vijana.

BTW hatuna haja ya kumjadili tena huyu mzee cuz hana jipya tena. Kila siku anakuja na mambo yaliyopita!

Umekunjwa mabakuli mangapi ya uji?
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amefufua upya sakata la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, akitaka serikali ithibitishe hadharani mtu anayetajwa kuhusika na tukio hilo.

Akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Ifakara, Morogoro jana, ikiwa ni sehemu ya Operesheni Sangara awamu ya pili, Dk. Slaa aliyeambatana na viongozi wakuu wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, alisema kuwa Serikali ya CCM imekuwa na kiburi cha kuwatisha wanaotaka kutetea maslahi ya wananchi.

Alisema kuwa imefikia hata hatua ya wengine kutishiwa vifo, huku akitolea mfano wa kutekwa, kupigwa na kisha kuumizwa Dk.Ulimboka, aliyetendewa unyama huo usiku wa kuamkia Juni 26 katika msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

"Serikali ina nguvu ya kuvifungia vyombo vya habari kwa sheria dhalimu ya magazeti ya mwaka 1977, lakini haitaweza kuzuia midomo ya watu kujadili suala zima la kutekwa huko kwa Dk. Ulimboka," alisema.
Dk. Slaa ambaye alikuwa akishangiliwa kwa nguvu, aliongeza kuwa, kuanzia sasa CHADEMA itaanzisha mapambano kwa ajili ya kutaka kupata ukweli juu ya aliyemteka Dk. Ulimboka.

Alisema kuwa miongoni mwa simu zilizowasiliana na Dk. Ulimboka ni Ramadhan Ingondhur, aliyetajwa kama mtu wa mwisho kabla ya kutekwa pamoja na namba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Mabwepande, aliyemtaja kwa jina la Abdallah Punja.

"Serikali na Usalama wa Taifa wanapaswa kusimama hadharani na kuuambia umma Ramadhan ni nani na kwanini anahusika na Idara ya Usalama wa Taifa.

"Mimi ni muumini wa Usalama wa Taifa na wala siwaondolei hadhi, lakini kwa mwendo huu ni wao wenyewe ndio wanajiondolea hadhi yao, na sasa wamekaa kufuatilia mikutano ya vyama vya siasa, hususan CHADEMA," alisema Dk Slaa.

Akizungumza katika mkutano huo, Mbowe alisema umati uliokusanyika unaonesha namna wakazi wa Kilombero walivyomthamini aliyekuwa mbunge wa viti maalumu, marehemu Regia Mtema.
Mbowe aliomba jina la uwanja wa Ifakara libadilishwe na kuitwa Uwanja wa Ukombozi, na kwamba hali hiyo iwe chimbuko la ukombozi kwa Mkoa wa Morogoro.

Aliwataka wakazi wa Kilombero kuacha kulalamika na badala yake wachukue hatua kwa kuachana na CCM na kujinga na CHADEMA.

"Ndugu zangu kila mmoja ana wajibu wa kujiuliza kafanya nini kwa ajili ya nchi yake, watoto wake na anawaandalia nini siku zijazo. Tambueni tupo katika utwala usiowajali na hili jukumu lenu ninyi wananchi kujiondoa katika hali hii na si kazi ya Dk Slaa, Mbowe au Lissu," alisema.
Mbali na Dk. Slaa na Mbowe, viongozi wengine waliokuwa katika msafara huo ni Joshua Nassar (Arumeru Mashariki), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Hamad Yusuph (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar), Suzan Kiwanga (Viti Maalumu), Joyce Mukya (Viti Maalumu) na wengine wa makao makuu.
Naye Lissu, alisema baada ya kupita kuanzia Mikumi hadi Ifakara, hajui ni kwanini bado wakazi wa wilaya hiyo wanaendelea kuikumbatia CCM huku akishangazwa na kitendo cha wananchi hao kuendelea kutozwa ushuru wa mazao ambao serikali ilikwishaupiga marufuku.

Alisema ufike wakati wananchi wawakatae viongozi wasiochaguliwa kuwa wawakilishi wao kwani wanasimamia masilahi ya waliowateua kama inavyotokea sasa katika maeneo mbalimbali.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Mbilinyi alijibu kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa wapinzani wanapinga maendeleo, akisema kwamba si kweli, kwani wao wanapingana na mipango inayowapa fursa mafisadi kujineemesha, huku wananchi wakiendelea kuogelea katika umasikini.

Mbona ni kama Dr. SLAA alikuwa anawaomba msamaha wananchi hao wa Ifakara kwa kutokana na kifo cha Regia Mtema? CDM nayo inatakiwa kuwaeleza watanzania na hasa wale wa Morogoro na Tarime utata wa vifo vya Rejia Mtema na Chacha Wangwe na aache kujificha kwenye kichaka cha Ulimboka ambaye kutekwa kwake kulitokanana na ubedhuli wake wa kusababisha vifo vya wagonjwa ambao wangeweza kupona endapo wangepata Matibabu. Akawaulize wafiwa wanatamwambia aliyemteka Ulimboka.
 
Ni Udini wa Ikulu au Serikali nzima ya CCM. Haiingii akilini Mtekwaji ni Dr STEVEN, Watekaji ni AHMED, RAMADHAN na ABEID. Mpelelezi mkuu SULEIMAN KOVA na amri ilitoka kwa Alhaji J.MRISHO.... Nani anabisha kuwa Udini Ulipewa kipaumbele na serikali ya ccm ktk Utekwaji wa Dr STEVEN ULIMBOKA?. Ni nani na kwa ushahidi upi ataweza kuisafisha ccm na kashifa hii ya Udini kwa Dr Steven huku makanisa zaidi ya 26 yamekwisha kuchomwa Znz?.
Mbona sakata la zima kuituhumu Serikali linawekwa mbele na Wakristu na hasa wale wa kutoka kaskazini, hapa tuseme ni udini na Ukabila? HELLEN KIJO BISMBA, ANANILEA NKYA, JOHN MNYIKA, SLAA, REGINALD MENGI n.k. Mkuu hapo hujasema lolote bora ungekuja na hoja nyingine. Hii ndiyo sababu itakayofanya Watanzania wengi tuamini kuwa Serikali na vyombo vyake inasingiziwa kwa kutengeneza mazingira ya udini kumbe wahusika ni wale wenye sera za udini, ukabila na umajimbo (sera za CONSERVATIVE kule uingereza, mshirika mkubwa wa CDM). Jana kuna mtu alirusha Thread humu anashauri Ulimboka akirejea ajiandae kugombea 2015 kwa tiketi ya CDM), kwa kauli hiyo bado watanzania tusiamini kwamba mkasa wa Ulimboka ulitengenezwa na CDM kwa kushirikiana wachaga (ANANILEA NKYA, BISIMBA na MENGI) kwa kivuli cha wanaharakati?
 
Mbona ni kama Dr. SLAA alikuwa anawaomba msamaha wananchi hao wa Ifakara kwa kutokana na kifo cha Regia Mtema? CDM nayo inatakiwa kuwaeleza watanzania na hasa wale wa Morogoro na Tarime utata wa vifo vya Rejia Mtema na Chacha Wangwe na aache kujificha kwenye kichaka cha Ulimboka ambaye kutekwa kwake kulitokanana na ubedhuli wake wa kusababisha vifo vya wagonjwa ambao wangeweza kupona endapo wangepata Matibabu. Akawaulize wafiwa wanatamwambia aliyemteka Ulimboka.
Inaelekea ndio umeamka halafu una hang over bado hujui unachoandika pata supu ya makongoro na limao uzimue halafu urudi upya uangalie ulichoandika nafikiri uta edit au kuondoa kabisa
 
Ndiyo majibu yenu, hamna sera tena. Nchi haItatawalika kwa majungu, fitina na uzushi kweli? Subiri ZITTO achukue nchi 2015 kama u-chagga utakuwemo tena ndani ya CDM na majungu yenu hayo.
 
Mbona sakata la zima kuituhumu Serikali linawekwa mbele na Wakristu na hasa wale wa kutoka kaskazini, hapa tuseme ni udini na Ukabila? HELLEN KIJO BISMBA, ANANILEA NKYA, JOHN MNYIKA, SLAA, REGINALD MENGI n.k. Mkuu hapo hujasema lolote bora ungekuja na hoja nyingine. Hii ndiyo sababu itakayofanya Watanzania wengi tuamini kuwa Serikali na vyombo vyake inasingiziwa kwa kutengeneza mazingira ya udini kumbe wahusika ni wale wenye sera za udini, ukabila na umajimbo (sera za CONSERVATIVE kule uingereza, mshirika mkubwa wa CDM). Jana kuna mtu alirusha Thread humu anashauri Ulimboka akirejea ajiandae kugombea 2015 kwa tiketi ya CDM), kwa kauli hiyo bado watanzania tusiamini kwamba mkasa wa Ulimboka ulitengenezwa na CDM kwa kushirikiana wachaga (ANANILEA NKYA, BISIMBA na MENGI) kwa kivuli cha wanaharakati?

Kwa taarifa yako "UNENE NALI NSUGUMA O SHINYANGA-Kishapu. NATABHAMANILE NA BHACHAGA BHAKO".. Tafuta mkalimani akutafsirie wewe kilaza.
 
Wewe si umeolewa huko Kaskazini, sina haja ya kujua ulichokiandika.
 
Back
Top Bottom