MUSSA ALLAN
JF-Expert Member
- Oct 13, 2013
- 18,925
- 13,263
Wana Jamvi, Amani Iwe nanyi!
Kama mtakumbuka mwaka 2012 baada ya Mwandishi wa habari aliyekuwa anaripotia CHANNEL TEN ndugu Daudi Mwangosi kuuawa kwa kupigwa Bomu na Polisi huko Iringa.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Ndugu W. Slaa, aliitembelea familia ya marehemu na kuahidi kuitunza, pamoja na kuwasomesha watoto walioachwa na marehemu mpaka kidato cha nne.
Sasa imepita miaka minne lakini hakuna kilichofanyika!Watoto wa Marehemu bado wanakabiliana na changamoto kali za kukosa mahitaji muhimu kama ada za shule na mengineyo.
Mjane wa Mwangosi bado anapambana na maisha magumu haswa baada ya kuachwa na Mumewe!
Wakazi wengi wa Iringa na Tanzania kwa ujumla wanajiuliza, wako wapi wafadhili waliojitapa enzi zile kuwa watasimama kidete kuhakikisha kuwa Familia ya Mwangosi haitaabiki?
Wako wapi wanasiasa uchwara mithili ya Mzee Slaa ambao walisema kuwa watatumia mpaka senti yao ya mwisho kuhakikisha kuwa familia hii haitawahi kutaabika kwa namna yoyote ile?
Je,Zile zilikuwa porojo tu za kisiasa?
Imekuwaje leo Mzee Slaa umekimbilia Canada na kuiacha Familia hii ikipata shida?
Au maneno uliyomwambia mjane siku ile yalikuwa ni porojo tu za kisiasa?
Mungu atusamehe!
Dr.W.Slaa