Dr. Slaa kuzungumza na Vyombo vya Habari, Serena Hotel - Septemba 1, 2015

Status
Not open for further replies.
Kamanda kwani wewe ulikuwa unampenda Lowassa, Tabwe Hiza, Sumaye?
ila nilikuwa siwachukii kwa dini zao.
A%20S%20shade.gif
 
Tatizo ni yule mdada mwenzenu alishafanya mazoezi ya ufirst lady kabisa.

Wacha tuweke akiba ya maneno lakini Dr Slaa ameboa, option iliyopo mwaka huu ni kuing'oa ccm kwa gharama yoyote tuifumuwe nchi tupange mifumo upya na katiba mpya ili sasa wajr aina ya viongozi tuwatakao awamu ijayo.
Currently mtu mwenye ushawishi mkubwa ni Lowasa tu, Dr Slaa angegalagazwa na magufuri mapema asubuhi aanze kutudanganya kuna kontena la kura.
Kama Dr alidhani yeye ni bora ni kwamba ajuwe kuanzia leo watu tunataka mabadiriko na hatuna mpango na vyama vyao.

Kwahiyo kama Dr.slaa angegaragazwa na magufuri ina maana endapo lowassa angegombea urais kupitia ccm chadema/ukawa wasingesimamisha mgombea urais?
 
Mnataka tu ku-preempt pigo litakalowapata maana mnajua Dr Slaa anajua madhambi yenu yote.
Kama mnajiamini kwa nini mnaanza kwa kumchafua eti kahongwa.
Unafikirk sote hatuna upeo wa kudadavua mambo?
Ni wazi sasa hivi kuna Chadema asilia na Chadema maslahi. Na mgombea wenu feki Lowassa hana upeo wa kumfikia hata 10% Dr Slaa.
Wananchi nao wameanza kuzinduka na Dr Slaa atakapomaliza kesho mtakuwa mmebaki uchi!
Na muache kutumia excuse ya mabadiliko kutaka kutuingizia Fisadi papa kwa mlango wa nyuma! Mwacheni Dr Slaa aongee na muache spinning!

Mabadiliko kumuweka fisadi?mabadiliko gani hayo?
 
Inasikitisha kuona CHADEMA asili nao wamepewa limbwata na kina LAKI si pesa, nao eti 'wanamtukana' Dr. Slaa, kweli?????

Dah nahic mbowe hajui aya handle vp haya mafuriko ya kimaslahi kutoka ccm, mpaka sasa kuna chadema maslahi na chadema asilia, wengi miongoni mwa chadema asilia ni kama wamesusa hivi na wanahisi kupuuzwa, chadema maslahi now ndo kila kitu, walipo hawajui hata katiba ya cdm inaseaje but ndo wanajifanya wao ndo chadema sanaaaaa! Kuna mpasuko mkubwa sana unakuja, u will tell me,

na unaambiwa lowassa anahudumia timu alokuja nayo toka ccm tu, hawa wa chadema watajijua wenyewe, akina makene ni kama wamesusa hivi, hata kutoa update kutoka kwenye mikutano hawataki
TEAM LOWASSA WANAJIONA WAO NDO CHADEMA SANA KULIKO CHADEMA ASILIA, WAKATI AKINA DR SLAA WANAHENYA KUKIJENGA CHAMA WAO WALIKUWA CCM WANAKULA BATA
 
Hatimaye katibu mkuu wa Cham cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Wilbrod Slaa ameamua rasmi kuachana na siasa baada ya tafakari ya muda mrefu.

Kesho Slaa anatarajiwa kutangaza uamuzi wake huo ndani ya 'Dar es Salaam Serena hotel' ambao utakuwa ni pigo kubwa kwa vyama vinavyounda UKAWA.

Katika hatua nyingine mwanachama wa CHADEMA anayeamini katika siasa za Dr. Slaa, G Sam ameamua kumuunga mkono kutokana na mizengwe ya uteuzi wa mgombea urais ndani ya chama hicho.

"Nitapiga kura kwa Halima Mdee na mgombea udiwani wa Chadema ila siyo kwa Edward Lowassa" anasema G Sam.

G Sam anamuonea Edward Lowassa kama mgombea dhaifu sana asiyeweza kwenda sambamba na kasi ya chama hicho. Aidha G Sam anakiri kuwa hana tatizo na Edward Lowassa kuhusu mambo ya ufisadi bali ni kutokana na udhaifu unaoonekana waziwazi juu ya mgombea huyo.

One of the worst posts I have ever seen.
 
Huu uchaguzi mpaka unaisha kuna watu watakuwa matajiri wa kutupwa,,, pia athari za huu uchaguzi ni baadhi ya kwenda jela hapo 2016,, raia wanaweza kupata uahueni wa maisha..
 
Safi sana ngoja tuangalie mawasiliani yakoje, hawa wezi koko wanafikiri Tanzania ni ya kwao peke yao au ni mali yao. EL amekuwa mwizi tangu miaka ya 1970 hadi leo bado ana kiu ya pesa za walipa kodi. It will never happen whatever the case.

Uwaziri mkuu aliteuliwa lini? so JK aliteua mwizi sugu? usalama wa taifa walikuwa wapi? ndio maana tunadai mabadiliko na tuna amini kuyafikia kwa kumtumia yeye huyo mwizi tangu 1970. Watanzania wanataka mabadiliko......CCM imeshindwa kuwaletea mabadiliko hayo
 
Naona umeona sheria imenza so unaamua kutuprovoke

Kwani hujui?angalia wagombea urais wa vyama vyote alafu linganisha majina yao na List of Shame; utakayemuona kwenye list ile ndio mgombea fisadi na chama chake ndio ficho la mafisadi.
 
CHADEMA ASILI STAND UP, inakuaje leo mpo kimya Dr. anapondwa na 'wanachama' wasio na hata mwezi ndani ya chama na nyie mmekaa kimya na wengine pia kuthubutu kumponda?? HII HAIKUBALIKI.. Leo kina Ocampo four, laki si pesa ndo wanaoojua Chadema na misingi yake???
 
Kwahiyo kama Dr.slaa angegaragazwa na magufuri ina maana endapo lowassa angegombea urais kupitia ccm chadema/ukawa wasingesimamisha mgombea urais?

Wewe ikifaa uwe mganga wa kienyeji kupiga dogori tu.
Lowasa alikuwa anaogopwa tangu akiwa ccm ni superpower.

Huu uchaguzi Lowasa anashinda tena kwa mbali mno kilichopo sasa hivi ni kuweka mikakati ya kuzilinda kura tu.

Magufuri hakujiandaa kwa dhati kugombea Urais ni Lowasa na kundi lake ndio wamelazimisha mgombea wa ccm awe Magufuri baada ya kumkata Lowasa, sasa wamekigeukia kinyago walichokichonga wenyewe.
 
Kwahiyo kama Dr.slaa angegaragazwa na magufuri ina maana endapo lowassa angegombea urais kupitia ccm chadema/ukawa wasingesimamisha mgombea urais?
Hujatendea haki jina lako.... hapa sio suala la cross multiplication rather the best ndo anae pewa nafasi na kwa sasa EL ni zaidi ya Dr. Slaa...
 
Dr Slaa staafu tu baba! Umejenga chadema kwa ukimya wa Lowassa! Leo Lowassa ameongea ukweli kuhusu ufisadi anaolazimishwa nao! Ukweli huo umemweka huru na kuaminiwa na vyama vyote vya siasa kupeperusha bendera yao ya urais 2015!

Sio Ikulu sio Kikwete aliyewahi kukana ukweli aliobainisha Lowassa kuhusu richmond. Hii maana yake ni kwamba Lowassa kaongea ukweli mtupu!

Sasa wewe unasusa nini? Unataka Lowassa asiseme ukweli?

Mwombe radhi Lowassa kwa kumbebesha mzigo mkubwa wa ufisadi aliotakiwa kubebwa na Bosi wake! Ukimya wa Lowassa ni hekima toka kwa Mungu! Mungu ni mkimya! Kwa kumuomba radhi maana yake Mungu naye atakusamehe. Japo ni siasa lakini Mungu bado ana nafasi kuu. Usibeze maana kila mtu hulipwa sawasawa na maneno na matendo yako!

Kikwete ndio fisadi sio Lowassa!
Sijawahi kuona mtu ambaye amewahi kuwa padre akawa na uchu wa madaraka! hii ndio naanza kuiona sasa hivi! kama walimuita ili ajieleze na akajieleza na wakamuelewa sasa Dr alitaka nini? eti aruhusiwe ila asipewe kugombea nyadhifa kubwa nyooo!! Wewe Dr wewe ona aibu! yaani lowassa awe pembeni kuwa mwanachama wa kawaida wewe ndio upeperushe bendera ya UKAWA? Duu haya yangekuwa maajabu ya dunia kabisa! Tunahitaji mtu mwenye uwezo, mbinu, akili, mikakati na mipango ya kutupeleka tunakotaka na kati ya Dr na lowassa, lowassa alimzidi Dr! Wewe ita press fanya lolote ongea lolote ila haturudi nyuma! tukirudi nyuma tutageuka kuwa jiwe. Kamwe wanaharakati hawana tabia ya kuangalia nyuma.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom