Dr Slaa kuzindua miradi ya maji Kyela

Dr Slaa kuzindua miradi ya maji Kyela

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa anatarajiwa kuzindua visima sita vya maji katika jimbo la Kyela.

Akizungumza na wanahabari kiongozi wa Chadema Kyela na Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa Abraham Mwamanyaki amesema visima hivyo vimefufuliwa na Chadema mara tu baada ya kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa Vijiji na kufanikiwa kuongoza halmashauri ya mji wa Kyela.

Mbunge wa Kyela Harrison Mwakyembe na CCM yenye madiwani wengi walishindwa kufufua visima hivyo kwa madai hamna hela kutokana na ufisadi mkubwa uliopo ndani ya Halmashauri hiyo.

Dr Slaa amealikwa kuzindua visima hivyo kutokana na maombi ya wananchi wa Kyela ambao wana imani kubwa Dr Slaa ndiye atakayekuwa Rais wa awamu ya tano.

Mm ni mmoja kati ya familia nyingi zilizo kuwa zimeathirika kwa kukosa maji hapa Kyela Mbugani nyumbani kwangu!Tulikuwa tunaamka saa 8 usiku kwenda kutafuta maji!

CHADEMA ndani ya week maji kila sehemu yapo,naamka saa 1 asubuhi maji yapo na hakuna tena kuamka usiku na giza totoro

Kwa hili walilofanya CHADEMA ndani ya week wanastahili mno pongezi maana CCM liliwashinda kwa miaka

At least sasa tunafaidi ndoa zetu maana "Mama" hatuamki tena usiku wa mnene kutafuta maji tukiwaacha wake zetu vitandani
 
Taratibu wananchi wataanza kupata maendeleo kupitia serikali za CDM!
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa anatarajiwa kuzindua visima sita vya maji katika jimbo la Kyela.

Akizungumza na wanahabari kiongozi wa Chadema Kyela na Mjumbecwa mkutano mkuu amesema visima hivyo vimefufuliwa na Chadema mara tu baada ya kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa Vijiji na kufanikiwa kuongoza halmashauri ya mji wa Kyela.

Mbunge wa Kyela Harrison Mwakyembe na CCM yenye madiwani wengi walishindwa kufufua visima hivyo kwa madai hamna hela kutokana na ufisadi mkubwa uliopo ndani ya Halmashauri hiyo.

Dr Slaa amealikwa kuzindua visima hivyo kutokana na maombi ya wananchi wa Kyela ambao wana imani kubwa Dr Slaa ndiye atakayekuwa Rais wa awamu ya tano.
Nna hakika serikali itazuia hilo lisifanyike, ni fedheha kwao. Mtakuja kuniambia hapa.
 
Big up CHADEMA,Dr. W.P.Slaa ndio rais wangu wa awamu ya tano. No one like him!
 
Atakuwa anatafuta mke mwingine wa mtu kazi yake kuvizia wake za watu.
 
Nna hakika serikali itazuia hilo lisifanyike, ni fedheha kwao. Mtakuja kuniambia hapa.

Ni vizuri umetambua kuwa ni kinyume cha sheria anayezindua miradi yote iliyotokana na serikali ni mwakilishi wa serikali.
 
Ila apo kyela swala la maji safi halihitaji visimA kwa sana ila inahitajika ule mladi Wa maji ya bomba ufufuliwe ccm wameshauua
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa anatarajiwa kuzindua visima sita vya maji katika jimbo la Kyela.

Akizungumza na wanahabari kiongozi wa Chadema Kyela na Mjumbecwa mkutano mkuu amesema visima hivyo vimefufuliwa na Chadema mara tu baada ya kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa Vijiji na kufanikiwa kuongoza halmashauri ya mji wa Kyela.

Mbunge wa Kyela Harrison Mwakyembe na CCM yenye madiwani wengi walishindwa kufufua visima hivyo kwa madai hamna hela kutokana na ufisadi mkubwa uliopo ndani ya Halmashauri hiyo.

Dr Slaa amealikwa kuzindua visima hivyo kutokana na maombi ya wananchi wa Kyela ambao wana imani kubwa Dr Slaa ndiye atakayekuwa Rais wa awamu ya tano.
Asante Kamanda Molemo kwa Tarifa nzuri sana hizi, Mungu aendele kumpa nguvu Mzee wetu
 
Uzi umeingiliwa na wezi wa Tegeta Escrow,waliobeba pesa ktk benki ya Stanbic kwa lumbesa.
Cc: chooni= msalani
 
Hebu tuwekane sawa. Hivi halmashauri inaongozwa na wenyeviti wa mitaa? Wapi nafasi ya madiwani?
 
Hvi Kyela nako kuna shida ya maji? Iweje chadema hiyo hiyo chini ya kamanda Mnyika inashindwa kuleta maji ubungo?
 
Back
Top Bottom