Dr Slaa kutikisa Dar leo

Dr Slaa kutikisa Dar leo

Status
Not open for further replies.

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa leo Jumamosi anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara Dar es Salaam katika uwanja maarufu wa Kampala ulioko Gongolamboto.

Katibu wa Jimbo la Ukonga Juma Mwaipopo akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari amesema Dr Slaa ataunguruma katika viwanja hivyo ikiwa ni maalum kwa ajili ya kukusanya maoni ya Katiba mpya.

Dr Slaa anatarajiwa kuambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu Mabere Marando,Wabunge John Mnyika na Halima Mdee,Mkurugenzi wa sera na utafiti Mwita Waitara pamoja na viongozi mbalimbali walioko makao makuu.

Kwa siku za karibuni Chadema imekuwa ikipata ufuasi mkubwa jimboni Ukonga na hii ni kutokana na jimbo hilo kuwa kama vile halina mbunge kutokana na matatizo makubwa yaliyopo jimboni humo.

Kumekuwa na ubovu mkubwa wa miundombinu jimboni Ukonga hasa kipindi cha mvua ambapo nauli ya daladala imekuwa ikifika hadi shilingi 1000/-

Tayari kuna shamrashamra nyingi kusubiri ujio huo wa Dr Slaa ambaye ana mvuto wa kipekee nchini.
 
Mbona sehemu zingine hawaji,waje hata biafra jamani kila siku pande hizo tu,wengine hamtutendei haki kabisa,njooni na kinondoni basi.
 
Tumesha sema huju JF na kwengineko kuwa, CHADEMA Dar hamna lenu.

Ni vyema nguvu kubwa muielekeze vijijini, kwani Dar tayari wameshaikataa CHADEMA siku nyingi ingawa makao makuu ya chama yapo hapa hapa Dar.
 
Endelea kujipa moyo, wananchi wa Dar wana hasira sana na nyie maccm
 
Tangu lini Dar ikatikiswa na slaa? Kweli mmekuwa watu voroja siku hizi!
 
Tumesha sema huju JF na kwengineko kuwa, CHADEMA Dar hamna lenu.

Ni vyema nguvu kubwa muielekeze vijijini, kwani Dar tayari wameshaikataa CHADEMA siku nyingi ingawa makao makuu ya chama yapo hapa hapa Dar.

Mkuu HAMY-D
Labda kama unaongelea vijiji vya KENYA hivi vya Tanzania sidhani kama wana muda wa kupoteza kumsikiliza mtu laghai na mpotovu wa maadili kama slaa
 
Last edited by a moderator:
Tumesha sema huju JF na kwengineko kuwa, CHADEMA Dar hamna lenu.

Ni vyema nguvu kubwa muielekeze vijijini, kwani Dar tayari wameshaikataa CHADEMA siku nyingi ingawa makao makuu ya chama yapo hapa hapa Dar.
  • :frog:" Ndo maana hawana wabunge kabisa DSM":wave:
 
Chama na HAMY-B
Yani wana akili kama kuku wa kizungu kutaga kila mara....

CCM dar inakubalika wapi? dar ina majimbo 8, ni lipi sisiemu walishinda kihalali.

Karibu Dr.Slaa watu watakuja kwa mapenzi yao na nauli zao bila kushombwa na malori.
 
Mbona sehemu zingine hawaji,waje hata biafra jamani kila siku pande hizo tu,wengine hamtutendei haki kabisa,njooni na kinondoni basi.

Mkuu kajembe usijali majimbo yote yatatembelewa
 
Last edited by a moderator:
Tumesha sema huju JF na kwengineko kuwa, CHADEMA Dar hamna lenu.

Ni vyema nguvu kubwa muielekeze vijijini, kwani Dar tayari wameshaikataa CHADEMA siku nyingi ingawa makao makuu ya chama yapo hapa hapa Dar.

You never deserve my comment!
 
tunawakaribisha xanaaaa....marando jembe nakuaminia.
 
Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa kesho Jumamosi anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara Dar es Salaam katika uwanja maarufu wa Kampala ulioko Gongolamboto.

Katibu wa Jimbo la Ukonga Juma Mwaipopo akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari amesema Dr Slaa ataunguruma katika viwanja hivyo ikiwa ni maalum kwa ajili ya kukusanya maoni ya Katiba mpya.

Dr Slaa anatarajiwa kuambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu Mabere Marando,Wabunge John Mnyika na Halima Mdee,Mkurugenzi wa sera na utafiti Mwita Waitara pamoja na viongozi mbalimbali walioko makao makuu.

Kwa siku za karibuni Chadema imekuwa ikipata ufuasi mkubwa jimboni Ukonga na hii ni kutokana na jimbo hilo kuwa kama vile halina mbunge kutokana na matatizo makubwa yaliyopo jimboni humo.

Kumekuwa na ubovu mkubwa wa miundombinu jimboni Ukonga hasa kipindi cha mvua ambapo nauli ya daladala imekuwa ikifika hadi shilingi 1000/-

Tayari kuna shamrashamra nyingi kusubiri ujio huo wa Dr Slaa ambaye ana mvuto wa kipekee nchini.

Hapo penye red, hivi huo ni mkutano wa kampeni au kukusanya maoni juu ya rasimu ya katiba?
 
Tumesha sema huju JF na kwengineko kuwa, CHADEMA Dar hamna lenu.

Ni vyema nguvu kubwa muielekeze vijijini, kwani Dar tayari wameshaikataa CHADEMA siku nyingi ingawa makao makuu ya chama yapo hapa hapa Dar.

Mkuu, wameona waende gongolamboto pengine huko watawapata wafuasi wao wa kisarawe, chanika na maeneo ya pembezoni. hapa Mjini kati wamechemsha sana. hata huko gongolamboto wataaibika sana
 
Chama na HAMY-B
Yani wana akili kama kuku wa kizungu kutaga kila mara....

CCM dar inakubalika wapi? dar ina majimbo 8, ni lipi sisiemu walishinda kihalali.

Karibu Dr.Slaa watu watakuja kwa mapenzi yao na nauli zao bila kushombwa na malori.

acha kuweweseka wewe. ni hivi majuzi tu CHADEMA imegaragazwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. au umesahau?
 
Kweli hawa watu wa chukua chako mapema wana beba watu toka vijijini ila kwa chadema watu ni nauli zao sio kubebwa
 
Mmeambiwa dk slaa atakua gongo la mboto sasa mbona mnatoka mapovu sn nyie magamba, subirini kwinini ingie
 
kweli hawa watu wa chukua chako mapema wana beba watu toka vijijini ila kwa chadema watu ni nauli zao sio kubebwa

ni kwa utaratibu huo ndo maana mnawakamua mpaka nauli zao. Hamna huruma nyie!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom