Mkulima mimi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2009
- 233
- 32
- Thread starter
-
- #21
Hiyo nyekundu ni ungo mkubwa. Dr. Slaa hiyo sheria kaisomea wapi au sheria ya kanisa ndio inamfanya kubobea kitaaluma katika sheria?
Nawasiwasi kama Dr. Slaa hana washauri wa kweli. kwani habari ya mshahara kuongezeka sio ya leo na wala hajaanza baada ya kampeni. watu wamesha kula mishahara miwili mpya na kampeni hazina hata wiki sasa hapo si ukilaza jamani. Hao FOS au FOD wanamshauri nini kama ndio anatuletea hizi pumba hata kabla hajaanza kampeni.
Hili la mishahara Dr Slaa angeliliacha kwa sasa. Hali ya WAFANYAKAZI wa Nchi ni mbaya. Kupinga nyongeza yoyote kwao hata kama sheria, taratibu na kanuni hazikufuatwa itamweka pabaya Dr Slaa. CCM wanajua sana kupindisha na kutoa tafsiri mbovu kwa kauli za wapinzani wao. Yeye Dr Slaa aseme atawafanyia nini Wafanyakazi wa nchi hii atakapokabidhiwa dola.
Hiyo nyekundu ni ungo mkubwa. Dr. Slaa hiyo sheria kaisomea wapi au sheria ya kanisa ndio inamfanya kubobea kitaaluma katika sheria?
Nawasiwasi kama Dr. Slaa hana washauri wa kweli. kwani habari ya mshahara kuongezeka sio ya leo na wala hajaanza baada ya kampeni. watu wamesha kula mishahara miwili mpya na kampeni hazina hata wiki sasa hapo si ukilaza jamani. Hao FOS au FOD wanamshauri nini kama ndio anatuletea hizi pumba hata kabla hajaanza kampeni.
No Dr hajapinga ongezeko la mishahara na hata wafanyakazi wanalifahamu hilo na kila siku anazungumzia tofauti ya kipato kati ya juu na chini. Anachosema ni kuwa kwa nini uwaambie huna fedha za kuwapa nyongeza hata kama kura hawatakupa halafu ukiona wamechukizwa na jambo hilo wakati wa kampeni unaongeza nje ya utaratibu wa matumizi ya fedha za umma?Hili la mishahara Dr Slaa angeliliacha kwa sasa. Hali ya WAFANYAKAZI wa Nchi ni mbaya. Kupinga nyongeza yoyote kwao hata kama sheria, taratibu na kanuni hazikufuatwa itamweka pabaya Dr Slaa. CCM wanajua sana kupindisha na kutoa tafsiri mbovu kwa kauli za wapinzani wao. Yeye Dr Slaa aseme atawafanyia nini Wafanyakazi wa nchi hii atakapokabidhiwa dola.
Padre alitumia suala la TUCTA na wafanyakazi kuwa ni chambo ya kujinasia kura. lakini hakujua kuwa JK ana utaratibu wa kuongeza mishahara kwa watumishi kwa utaratibu maalum.Sasa sijui atatoka vipi?
No Dr hajapinga ongezeko la mishahara na hata wafanyakazi wanalifahamu hilo na kila siku anazungumzia tofauti ya kipato kati ya juu na chini. Anachosema ni kuwa kwa nini uwaambie huna fedha za kuwapa nyongeza hata kama kura hawatakupa halafu ukiona wamechukizwa na jambo hilo wakati wa kampeni unaongeza nje ya utaratibu wa matumizi ya fedha za umma?
Acha awe wazi,wafanyakazi wa sasa sio Mabwege tena watamwelewa Dr. Slaa na kufahamu kuwa nyongeza hiyo ni kebehi kwao na wameuza utu wao uliodhalilishwa pale Diamond. Sheria ifuate mkondo wake pingamizi lisonge mbele.
Hivi wanao mpinga slaa ni wasaliti? Mbona wanaonekana kama watu wa ajabu...! Kulikoni hakuna uhuru wala demokrasia!?
Leta source vinginevyo hatutaki majungu humu
Amekurupuka huyo na washauri wake wako kisiasa zaidi badala ya kutafuta ukweli.kura hazitafutwi hivyo .Hiyo nyekundu ni ungo mkubwa. Dr. Slaa hiyo sheria kaisomea wapi au sheria ya kanisa ndio inamfanya kubobea kitaaluma katika sheria?
Nawasiwasi kama Dr. Slaa hana washauri wa kweli. kwani habari ya mshahara kuongezeka sio ya leo na wala hajaanza baada ya kampeni. watu wamesha kula mishahara miwili mpya na kampeni hazina hata wiki sasa hapo si ukilaza jamani. Hao FOS au FOD wanamshauri nini kama ndio anatuletea hizi pumba hata kabla hajaanza kampeni.
Mkuu hilo (red) ni kweli, hawajui kugoma na ni watiifu sana. Ila sasa hivi wamekeisha elewa kuwa kile chumba cha kupigia kura uyafanyayo mule ni siri yako. Na wao wana siri yao moyoni. Wamechoka,wamefedheheshwa na kupuuzwa sana na utawala uliopita na sasa ndio wakati wao wa kutumia silaha waliyo nayo, KURA. Kama huliamini hilo mkuu ni bahati mbaya. Hakuna watumishi walikuwa wagumu kuelewa kuwa wanatumiwa kama walimu,lakini hebu fanya utafiti kidogo uone misimamo ya walimu sasa hivi utaona mabadiliko ambayo hata CCM wenyewe wameshashtukia.Wafanyakazi wa Tanzania hawako hivyo unavyowafikiria. Hawajui kugoma. Ni watiifu sana. Wengi wao wanaridhika sana anapopewa nafasi inayomwezesha kufanya ubadhirifu. Hawatamwelewa Dr Slaa hasa katika kipindi hiki ambacho CCM inaweza kucheza rafu yoyote ile ikiwemo hiyo nyongeza kinyemela ya mishahara. CCM wanajua marefa wote ni wao. NEC, RPP na vyombo vya DOLA.
Luiza naona una michango 11 tu uliochangia kwa mwezi huu wa nane hapa JF na kama michango 10 iliyopita inafanana na hivi utakimbia hapa JF muda si mrefu maana hapa ni pa watu vichwa tu. Huwa hoja baki ukisoma hoja za wenzio.Amekurupuka huyo na washauri wake wako kisiasa zaidi badala ya kutafuta ukweli.kura hazitafutwi hivyo .
Pingamizi ni la kitoto hilo. halijaenda shule.limekurupukaJK ni sawa na the late ODUAR wa Nigeria, hakuna muda R.I.P.Dr kaona wafanyakazi wameongezwa mishahara siku chache kabla ya kampeni ndio maana anataka kumuwekea pingamizi JK pia namuongezea amuwekee pingamizi ili kulinda afya yake asije akatutia hasara ya kuendesha uchaguzi mdogo hapo baadae.
Hoja ikiwepo manake husomwa na kuchangiwa kulingana na maono ya mchangiaji. Usiogope tuko pamoja. si lazima tukubaliane katika unayoyawaza wewe.JF inakutana na vichwa mbalimbali.ni kwa hoja tu si kukimbizana.hasira ya nini?Luiza naona una michango 11 tu uliochangia kwa mwezi huu wa nane hapa JF na kama michango 10 iliyopita inafanana na hivi utakimbia hapa JF muda si mrefu maana hapa ni pa watu vichwa tu. Huwa hoja baki ukisoma hoja za wenzio.
CV ya Dr Slaa
EDUCATION
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993-1993
TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985-1985
St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980-1981
St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977-1981 [Doctor of Canon Law (Latin: Juris Canonici Doctor or JCD)]
Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974-1977
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972-1973
Itaga Seminary School A-Level Education 1970-1971
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966-1969
Karatu Primary School Primary Education 1962-1965
Daudi Primary School Primary Education 1961-1961
Kwermusl Primary School (Mbulu) Primary Education 1958-1960
Nikiangalia hapo sioni sehemu inapoonesha kasomea sheria zetu nje ya sheria ya kanisa (Canon Law)