Kwa akili ndogo tu tena ya kawaida, CCM huwa wanapongeza kitu kinachofanywa na mpinzani, pale wanapoona kwamba kinawasaidia. ndio maana na wewe umeleta haya malalamiko ya Dr. Slaa - huo unaoitwa "ushauri". impact unayoiuliza mojawapo ni hiyo jitihada kubwa sana ya ninyi wapiga filimbi, kupigia kelele sana kwamba wanachofanya UKAWA hakina maana na haikifai. kingekuwa kweli hakifai, wala msingepiga kelele hivyo!
Jiulize, huyo Naibu Spika kukailia kiti kile mfululizo, kuna impact gani? maana kwa kawaida kuna Spika, Naibu Spika, wenyeviti, na wote huwa wanafanya kazi pamoja. sasa Spika hayupo - anatibiwa India, Wenyeviti wamepigwa ban, sasa hizo shughuli zingine ambazo anatakiwa kuzifanya Naibu spika kwa niaba ya Spika, na kwa niaba yake mwenyewe, ambazo sasa hivi hazifanyiki ili kupambana na UKAWA. Jiulize impact kwa afya yake, kufanya kazi hiyo mfululizo, na kuacha zingine zote. Jiulize psychological impact kwa kila siku unasusiwa, unaingia watu wanaondoka, hata kama amekula jiwe usoni, kuna vitu vinaungua ndani yake.
Taasisi nzima ya Bunge sasa inayumba, kutokana na jitihada kubwa za kudeal na UKAWA. na kama panic tactics, imekuja ban ya kuwazuia kuongea na wananchi waliowachagua, ambayo ni kinyume na katiba na sheria ya vyama vya siasa. kwa hiyo kuvunja huko sheria kwa serikali, ni mojawapo ya impact ya action ya UKAWA. na kwa kuwa serikali inavunja katiba na sheria halali, hiyo inaweka rekodi mbaya na kuiweka serikali katika wakati mgumu, na hii itajitokeza baadaye. kwa hiyo hizo kelele zenu ni dalili tosha kabisa kwamba mmekalia moto, matako hayatulii. toka lini mkawa na uchungu na mafanikio ya UKAWA???