Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,190
- 128,243
eti wadau
Hivi chenge ameshafungwa kwa lile kosa la ufisadi?
Mnajaribu kujikakamua!
Habari hii haikuwa na maana yoyote kuletwa hapa. wanaoenda mahakamani la msingi ni kuenda huko siyo kututangazia hapa.
eti wadau
Waliufyata alipotajwa kwenye list of shame itakuwa hili? Hao ni wajinga wachache wanaoishi kwa kujikomba. Wanataka kusema wao wanauchungu kuliko mkewe au wanae. Hawana akili
WanaJF,
Kufuatia tuhuma mbalimbali ambazo Dr Slaa amezielekeza kwa mkuu wa nchi, rais wa JMT, Dr Kikwete, wadau mbalimbali wamejipanga kuhakikisha Dr Slaa anapelekwa mahakamani kwa lengo moja tu, nalo ni kuthibitisha tuhuma zake dhidi ya mkuu wa nchi.
Dr Slaa ambae ni katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) ameelekeza tuhuma nzito kwa rais Kikwete bila kutoa ushahidi wowote wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari siku ya alhamisi ya tarehe 16/10/2014.
Wadau hao wamesema kwa kipindi kirefu tu wamekuwa wakimpuuza Dr Slaa kutokana na tuhuma zake hewa dhidi ya CCM na viongozi wa serikali, lakini wadau hao wameongeza kwamba, kwa hatua ambayo Dr Slaa ameifikia sio tena ya kupuuzwa, bali anapaswa kuwajibishwa.
Aidha, itakumbukwa kuwa ni desturi ya Dr Slaa kuongea maneno ya hovyo kutokana na tabia yake ya kuokoteza habari za vijiweni ambazo kimsingi hazina tija yoyote kwa Watanzania. Hivyo wadau hao wameazimia kumuadabisha kutokana na tabia yake.
kumbe bado unaexist? Mzima lakini? Manake wewe umekuwa kazi yako ni moja tu kuapmbana na dr slaa. Ila kwa muda haukuwepo hewani au ulikuwa unakuja kwa id tofauti. Au wewe ni nape?
WanaJF,
Kufuatia tuhuma mbalimbali ambazo Dr Slaa amezielekeza kwa mkuu wa nchi, rais wa JMT, Dr Kikwete, wadau mbalimbali wamejipanga kuhakikisha Dr Slaa anapelekwa mahakamani kwa lengo moja tu, nalo ni kuthibitisha tuhuma zake dhidi ya mkuu wa nchi.
Dr Slaa ambae ni katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) ameelekeza tuhuma nzito kwa rais Kikwete bila kutoa ushahidi wowote wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari siku ya alhamisi ya tarehe 16/10/2014.
Wadau hao wamesema kwa kipindi kirefu tu wamekuwa wakimpuuza Dr Slaa kutokana na tuhuma zake hewa dhidi ya CCM na viongozi wa serikali, lakini wadau hao wameongeza kwamba, kwa hatua ambayo Dr Slaa ameifikia sio tena ya kupuuzwa, bali anapaswa kuwajibishwa.
Aidha, itakumbukwa kuwa ni desturi ya Dr Slaa kuongea maneno ya hovyo kutokana na tabia yake ya kuokoteza habari za vijiweni ambazo kimsingi hazina tija yoyote kwa Watanzania. Hivyo wadau hao wameazimia kumuadabisha kutokana na tabia yake.
Nani mwenye watoto wasiojua mama zao?1.Nani kapora mke mtu?.
2.Nani kashindwa upadri?
3.Nani kavunjwa mkono na demu wake?
Na mengineyo