Dr Slaa kufikishwa Mahakamani!

Dr Slaa kufikishwa Mahakamani!

Tangulieni mahakamni mtaaibika sana,
JK mwenyewe anashangaa nani kampa Dr. Slaa hizo habari, Naomba Mungu Mtangulie kabla ya wiki ijayo kwisha kwani mtaumbuka sana,
 
Ni vizuri sana akifunguliwa mashtaka ila hao watakaofungua mashtaka wahakikishe wamefanya mawasiliano ya kutosha kuhakikisha kuwa mkuu wa nchi atatoa ushahidi kwa kuwa mnasema wenyewe kuwa tuhuma hizo zinamhusu mkuu wa nchi. Kama katiba inampa kiongozi huyo kinga ya kupelekwa mahakamani basi mfahamu kuwa hapo ni shidaaaaa.
 
Huyu jamaa na Dr. Slaa,,halali kila muda anamuwaza Slaa.
 
Chezea mimi namaliza wewe
images (3).jpg
 
Anzeni na ile list of shame aliyoitaja Mwembeyanga, then mje na EPA kwani mliodai ni vijikatasi tu vya mtandani then mje na RADA pia mtuambie ile chenji yetu mmeipeleka wapi?
 
WanaJF,

Kufuatia tuhuma mbalimbali ambazo Dr Slaa amezielekeza kwa mkuu wa nchi, rais wa JMT, Dr Kikwete, wadau mbalimbali wamejipanga kuhakikisha Dr Slaa anapelekwa mahakamani kwa lengo moja tu, nalo ni kuthibitisha tuhuma zake dhidi ya mkuu wa nchi.

Dr Slaa ambae ni katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) ameelekeza tuhuma nzito kwa rais Kikwete bila kutoa ushahidi wowote wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari siku ya alhamisi ya tarehe 16/10/2014.

Wadau hao wamesema kwa kipindi kirefu tu wamekuwa wakimpuuza Dr Slaa kutokana na tuhuma zake hewa dhidi ya CCM na viongozi wa serikali, lakini wadau hao wameongeza kwamba, kwa hatua ambayo Dr Slaa ameifikia sio tena ya kupuuzwa, bali anapaswa kuwajibishwa.

Aidha, itakumbukwa kuwa ni desturi ya Dr Slaa kuongea maneno ya hovyo kutokana na tabia yake ya kuokoteza habari za vijiweni ambazo kimsingi hazina tija yoyote kwa Watanzania. Hivyo wadau hao wameazimia kumuadabisha kutokana na tabia yake.

Porojo tu
 
Back
Top Bottom