Elections 2010 Dr. Slaa Jangwani katika Picha

Duh! Hii imekaje? hebu fafanua zaidi.

Kubalini tu yaishe, hapa mmekamatika, hasa pale mnapokutana na mkombozi wa watanzania! Mungu wetu hajalala usingizi.. kaona mafisadi wanakotupeleka watatumaliza, katuletea mkombozi wa Slaaa

Go, go Slaa.. magogoni is wating for you!

Bythe way, mmeona kadi za chama cha mafisadi zinavyo chanwa chanwa huko MUSOMA town? na bado ndo kwanza ngoma imeanza!
 
Key words to NOTE from Dr. W. Slaa

........Watanzania mkinipa ridhaa ya kuongoza.............Jambo la kwanza ninawaomba Mtuombee Duwa ili atupe hekima ya KUONGOZA NA SI KUTAWALA kama walivyofanya wenzetu...................
 
Key words to NOTE from Dr. W. Slaa

........Watanzania mkinipa ridhaa ya kuongoza.............Jambo la kwanza ninawaomba Mtuombee Duwa ili atupe hekima ya KUONGOZA NA SI KUTAWALA kama walivyofanya wenzetu...................
Hakika yalikuwa maneno mazito yalijaa hekima, busara na moyo wa kumcha Mungu. Kabisa! Hata mimi yalinigusa sana.
 
Mwaka huu JK ataupata Urais kwa jasho, hatapewa kwenye sahani bila kuutolea jasho. Hakuna cha ushindi wa tsunami wala nini.

Nani kakwambia ataupata, labda useme ataikwiba kama alivyofanya Kibaki.
 
b9awcl.jpg


Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Dkt.Wilbrod Slaa, akizungumza na wakazi wa Dar es Salaam waliofika katika viwanja vya Jangwani kumsikiliza.

Hizi picha za leo kweli?
 
Unabii!! Chadema kitakuja kuunda serikali. Muda wa Chama Cha Mafisadi (CCM) kufa ni sasa!!
 
Duh! I don't know of what happended right now! But I gave all the weaknesses of slaa, Mod have have removed them!. strange as it is! I previoulsy have an idea that JF is a platform where we dare talk openly. I never knew that it is a platfom where Chadema dare talk openly! And for the same reasons, I will never be back on this platform. However, at this juncture, I have no means to convince you that Slaa he is unfit for anything except for MP position. The mass of Tanzania know it all, and we know it all. Keep on dreaming and goodluck

Wana JF wenzangu maana ya Kanyafu Nkanwa ni katamu mdomoni. Huyu mbumbumbu ni moja kati ya watu wanaoiba na kula keki ya Taifa. Hakuna haja ya kubishana naye, ametumwa kutetea ushenzi na uchafu unaofanywa na CHAMA CHA MAFISADI kwa faida ya tumbo lake. Tarehe 31 October 2010 Keko, Ukonga, Kingoruwila na magereza mengine yote yaliyopo nchini hayatatosha maana tutawaweka ndani mafisadi papa wote na vibaraka vyao ikiwa ni pamoja na zezeta hili linalojiita Kanyafu Nkanwa. Huyu jamaa ni nkonyofu fijo kangi alinikigune kya nyoko. ( Ni mpumbavu sana na pia ana laana ya Mama yake)
 
It all depends BAK. Wakipangwa wababaishaji mia, mmoja atakuwa kiongozi wao. Slaa anaweza kuwa kwa hii stage

Na wakipangwa vipofu 10 lazima kutakuwa na kiongozi wao.Unfortunately,vipofu tunaowazungumzia hapa ni wale wenye macho mazima kabisa lakini hawaoni.MENTAL BLINDNESS,huh!
 
Siamini kabisa kama kuna watu wanaota eti siku moja Slaa atakuja kuwa Rais wa Tanzania!!! Bwahaha hahah...Keep on dreaming...
 
Duh! I don't know of what happended right now! But I gave all the weaknesses of slaa, Mod have have removed them!. strange as it is! I previoulsy have an idea that JF is a platform where we dare talk openly. I never knew that it is a platfom where Chadema dare talk openly! And for the same reasons, I will never be back on this platform. However, at this juncture, I have no means to convince you that Slaa he is unfit for anything except for MP position. The mass of Tanzania know it all, and we know it all. Keep on dreaming and goodluck
Go join Michuzi's blog where you can talk nonsense and be cheered just as you cheer when Kikwete talks nonsense.
 
Duh! Hii imekaje? hebu fafanua zaidi.
Aha Kibunango Upo ? ama kweli Mmungu kadiri ,wengi wetu wahaka ulitungia na kujiuliza yuwapi huyu kiumbe wake ?kampeni ndio zimeanza hizo ,hebu tupe kidogo mtazamo wako jungu kuu halikosi ukoko.
 
Miezi hii tutasoma mengi toka kwa hawa watu kuja and then baada ya Dr Slaa kuingia Ikulu watakaa kimya hutaona hata mmoja hapa.
 
Kwanini utushawishi kwamba Dr. Slaa hafai kuwa rais ila anafaa kuwa Mbunge? Inakuwaje mtu afae kuwa Mbunge lakini asifae kuwa Rais? Sifa za wagombea wa nafasi hiyo ni zile zile, kasoro umri tu. After all, wewe ni nani mpaka utuambie kwamba hafai? Hoja zako za kum-disqualify Dr. Slaa hazina mashiko hata kidogo, sana sana naona ni uzushi.

Mwisho kabisa, naona Dr. Slaa ni tishio kwa Kikwete na ndio maana umekazana kwamba anafaa akagombee Ubunge ili Kikwete apate mteremko. Mwaka huu JK ataupata Urais kwa jasho, hatapewa kwenye sahani bila kuutolea jasho. Hakuna cha ushindi wa tsunami wala nini.

Na wewe nani amekuambia kuwa Dr. Slaa anafaa? Tarehe 31 October mwananchi ndio atakayeamua ni nani anafaa. Tunaongea hapa kama vile Wanajamii forums ndio watu pekee watakaopiga kura. Jamani jaribuni kuwa objective. Acheni utopia. Upinzani bongo bado kabisa. Watanzania bado waoga sana. Hata Mr Mbowe kasema hili leo. Ni vigumu kuondoa woga wa Watanzania ndani miezi miwili.

Jaribuni hata kufanya utafiti nchi nyingine za Afrika muone jinsi wapinzani walivyofight kuchukua madaraka. Sio rahisi kama mnavyofikiri. Ningependa sana kuona Tanzania inaongozwa na chama kingine, lakini sidhani kama vyama vya upinzani ni strong enough kuwa-convince wananchi.

I am sorry and feel bad to say to say this but bado hatujawa na strong opposition in Tanzania. And this is not good.
 
Jambo moja hamna mtu anaweza kubisha. DR SLAA ameleta challenge kubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Kama CHADEMA wataendelea na kasi hiyo hata baada ya kuisha uchaguzi mkuu, uchaguzi mkuu wa 2015 patakuwa hapatoshi. Ila kwa sasa CHEDEMA na DR SLAA kwa uono wangu hawana nafasi yoyote ya kuweza kwenda Ikulu. Nitatoa sababu tatu kwa leo.

Sababu ya kwanza CHEDEMA bado hakijaenea vizuri katika nchi kiasi cha kupata sura ya kitaifa. Ushahidi wa ili ni mwingi. Mosi, katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni walipata wenyeviti wa serikali za mitaa chini ya asilimia 2. Hiyo ina athari kubwa mno katika uchaguzi kwa mtu anayetafakari. Tuzingatie kwamba katika kipindi kifupi cha kampeni cha miezi miwili si rahisi kuweza kuzifikia sehemu zote za nchi. Mosi, Chedema imeweka wagombea wa ubunge na udiwani chini ya asilimia 40. Hiyo inawafanya waweke uzito zaidi katika majimbo ambako wameweka wabunge na kuwaacha CCM watambe katika majimbo ambayo Chadema hawana mgombea. Tatu, katika sehemu nyingi za mikoani na hasa vijijini CHADEMA hawana hata ofisi. Ofisi zao zinaishia katika magari ya kampeni za uchaguzi.

Sababu ya pili, tofauti na CCM na hata CUF kidogo, kampeni zote za CHADEMA zimebebwa na DR SLAA. hiyo inaweza kuthibitishwa hata na namna vyombo vya habari vinavyo ripoti. Kwa upande wa CCM utasikia kampeni za mgombea uraisi, kampeni za mgombea mweza, kampeni za wabunge mbalimbali na zote zikiwanadi wagombea wa CCM katika maeneo mengi ya nchi. Kwa mtaji huo, CCM wana nafasi kubwa kuuza sera zao katika sehemu kubwa ya nchi kwa kutumia wagombea wao mbali mabli tofauti na CHADEMA inayomtumia sana DR SLAA. DR Slaa peke yake hawezi kumaliza hata robo ya Tanzania.

Uwezo na maandalizi ya wagombea wengi wa Chadema katika ngazi ya ubunge na udiwani ni mdogo ukilinganisha na wa CCM. Matokeo yake wanangoja hadi DR SLAA aje ndio waweze kufanya kampeni zao.

Kwa sababu nilizotaja hapo juu pamoja na zingine nyingi ambazo nitazibaini kadili tunavyoendelea kujadili CHADEMA bado mapema kuweza kuchukua uraisi. Nguvu za ziada na za kuendelea zinahitajika ili kupata uwezo wa kwenda Ikulu. Ushauri wangu ni kwamba baada ya uchaguzi mkuu, Chadema waweke msisitizo sana katika kukisambaza chama. Kwa kuanzia, wahakikishe kila kata wana ofisi na kila wilaya na mkoa ofisi ya kueleweka. Ofisi ya makao makuu pia inatakiwa iboreshwe ifanane fanane na chama chenye kiu ya kwenda Ikulu. Pia wajitahidi kufanya uwiano katika viongozi wake na wabunge wa viti maalumu. Kigezo cha elimu peke yake, kwa maoni yangu hakifai. Chama kiangalie pia uwakilishi wa kimikoa na makundi mengine ya kijamii yenye nguvu.

Natanguliza shukulani yangu ya kupata majibu ya kistaarabu yenye kujibu hoja sio kuataki mtu.
 
Back
Top Bottom