Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 524
Wikiendi iliyopita nilitembea Hifadhi za Ngorongoro na Lake Manyara ambapo nililala Karatu Jimboni kwa Mhe. Slaa kwa siku mbili. Wakati narudi nilipitia Lodges kadhaa na nilivutiwa sana na jitihada za wenyeji wa Karatu kuitumia sekata ya Utalii ili kujinufaisha kiuchumi.
Wakati narudi nilipita Lodge na Campsite moja ya mwenyeji wa pale ambaye amebadilisha nyumba yake na kuifanya ya kupokea wageni (watalii) na amefunga mahema kwa wanaohitaji kulala pale waendapo Lake Manyara au Ngorongoro Crater. Nilimuuliza Mjasiria mali yule juu ya changamoto wanazopata kwa ujasiriamali huo.Jambo mojawapo lililonihuzunisha na ambalo pia linamkera Mzawa yule ni juu ya Wakenya kuvamia eneo la KAratu na kununua ardhi kutoka kwa wenyeji na viongozi wa vijiji-mfano uongozi wa Kijiji cha Lotya ambao wameuza mlima mzima kwa Mkenya mmoja na sehemu nnyingine ya ardhi imeuzwa kwa Mwarabu.
Wenyeji wa KAratu wamepapatikia sana kuuza ardhi zao kwa wageni ambao wanatoa pesa nyingi kununua ardhi ili kukinga utajiri utokanao na Sekta ya Utalii. Nijuavyo mimi sheria ya nchi inakataza Wageni kumiliki ardhi na wWageni hawa toka Kenya wanaonunua ardhi ni watu binafsi ambao hawajulikani hata na Kituo cha Uwekezaji (TIC). Hili jambo limeniuma sana maana naona kuwa wageni hao watkuja kutufanya watumwa wao muda si mrefu.
Natoa changamoto kwako Mh. Slaa ufuatilie hili, maana wewe ni mwana JF na kwangu hii ndo njia rahisi ya kukufikishia ujumbe huu. Walinde wapiga kura wako.