Dr. Slaa, hili linawezekana Jimboni mwako?

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Wikiendi iliyopita nilitembea Hifadhi za Ngorongoro na Lake Manyara ambapo nililala Karatu Jimboni kwa Mhe. Slaa kwa siku mbili. Wakati narudi nilipitia Lodges kadhaa na nilivutiwa sana na jitihada za wenyeji wa Karatu kuitumia sekata ya Utalii ili kujinufaisha kiuchumi.

Wakati narudi nilipita Lodge na Campsite moja ya mwenyeji wa pale ambaye amebadilisha nyumba yake na kuifanya ya kupokea wageni (watalii) na amefunga mahema kwa wanaohitaji kulala pale waendapo Lake Manyara au Ngorongoro Crater. Nilimuuliza Mjasiria mali yule juu ya changamoto wanazopata kwa ujasiriamali huo.Jambo mojawapo lililonihuzunisha na ambalo pia linamkera Mzawa yule ni juu ya Wakenya kuvamia eneo la KAratu na kununua ardhi kutoka kwa wenyeji na viongozi wa vijiji-mfano uongozi wa Kijiji cha Lotya ambao wameuza mlima mzima kwa Mkenya mmoja na sehemu nnyingine ya ardhi imeuzwa kwa Mwarabu.

Wenyeji wa KAratu wamepapatikia sana kuuza ardhi zao kwa wageni ambao wanatoa pesa nyingi kununua ardhi ili kukinga utajiri utokanao na Sekta ya Utalii. Nijuavyo mimi sheria ya nchi inakataza Wageni kumiliki ardhi na wWageni hawa toka Kenya wanaonunua ardhi ni watu binafsi ambao hawajulikani hata na Kituo cha Uwekezaji (TIC). Hili jambo limeniuma sana maana naona kuwa wageni hao watkuja kutufanya watumwa wao muda si mrefu.

Natoa changamoto kwako Mh. Slaa ufuatilie hili, maana wewe ni mwana JF na kwangu hii ndo njia rahisi ya kukufikishia ujumbe huu. Walinde wapiga kura wako.
 
Vipi mlio hudhuria mahakamani huko Karatu...!!
....Alisema upande wao umekamilisha maandalizi ya ushahidi na kumtaja shahidi wa kwanza, anayetarajiwa kupanda kizimbani leo kuwa ni Joseph Haimu.

Vielelezo vyote vilivyowasilishwa mahakamani hapo na wakili Mwaluko na mwenzake Mpaya Kamara, vilikubaliwa na kupokewa na mahakama.

Upande wa utetezi katika kesi hiyo unaongozwa na Tundu Lissu, anayemtetea Dk. Willbrod Slaa na wakili wa serikali aliyetambulika kwa jina moja la Mgiwa, ambaye anamtetea mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa....?
 
Wikiendi iliyopita nilitembea Hifadhi za Ngorongoro na Lake Manyara ambapo nililala Karatu Jimboni kwa Mhe. Slaa kwa siku mbili. Wakati narudi nilipitia Lodges kadhaa na nilivutiwa sana na jitihada za wenyeji wa Karatu kuitumia sekata ya Utalii ili kujinufaisha kiuchumi.

Wakati narudi nilipita Lodge na Campsite moja ya mwenyeji wa pale ambaye amebadilisha nyumba yake na kuifanya ya kupokea wageni (watalii) na amefunga mahema kwa wanaohitaji kulala pale waendapo Lake Manyara au Ngorongoro Crater. Nilimuuliza Mjasiria mali yule juu ya changamoto wanazopata kwa ujasiriamali huo.Jambo mojawapo lililonihuzunisha na ambalo pia linamkera Mzawa yule ni juu ya Wakenya kuvamia eneo la KAratu na kununua ardhi kutoka kwa wenyeji na viongozi wa vijiji-mfano uongozi wa Kijiji cha Lotya ambao wameuza mlima mzima kwa Mkenya mmoja na sehemu nnyingine ya ardhi imeuzwa kwa Mwarabu.

Wenyeji wa KAratu wamepapatikia sana kuuza ardhi zao kwa wageni ambao wanatoa pesa nyingi kununua ardhi ili kukinga utajiri utokanao na Sekta ya Utalii. Nijuavyo mimi sheria ya nchi inakataza Wageni kumiliki ardhi na wWageni hawa toka Kenya wanaonunua ardhi ni watu binafsi ambao hawajulikani hata na Kituo cha Uwekezaji (TIC). Hili jambo limeniuma sana maana naona kuwa wageni hao watkuja kutufanya watumwa wao muda si mrefu.

Natoa changamoto kwako Mh. Slaa ufuatilie hili, maana wewe ni mwana JF na kwangu hii ndo njia rahisi ya kukufikishia ujumbe huu. Walinde wapiga kura wako.

Ibrah hiyo tayari imeonyesha kwamba wananchi tumekuwa mbumbu wa sheria, hawajui kule Musoma kuna upungufu wa ardhi hadi kupelekea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, hilo nafuu zaidi ni pale tutakapo kuwa na mapigano na Wakenya.
Bila shaka Zitto ni mwana JF tafadhali wanaojua PM yake wampelekee taarifa hii kama hajaiona maana yawezekana yuko busy na kamati ya madini. Lazima waondoke
 
Back
Top Bottom