Emma.
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 19,932
- 5,566
Lowassa amesitisha zoezi la kupokea wageniSio bure umerogwa
Lowassa amesitisha zoezi la kupokea wageniSio bure umerogwa
Imenichukua miezi 36, kujifunza ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo( chadema), nimejifunza mengi.
Tangu kuondoka kwa ward Kabour aliyekuwa katibu Mkuu kutokea kigoma na nafasi yake kushikwa na mtaalamu wa sheria,na falsafa ya theolojia,Dr wilbroad Slaa,nimeona hakika kiongozi huyu ni wa kutukuka.
Kuonesha kuwa amefanya kazi kubwa pale alipofanya yafuatayo:
KUIMARISHA TAASISI ZA CHAMA
Alianza na kuwajengea uwezo watumishi wa makao makuu katika nyanja ya kitaalamu na kitaaluma,akawapa nafasi kwenda nje kusoma,akaanzisha kurugenzi ya sheria,kurugenzi ya habari,kurugenzi ya ulinzi na usalama,kurugenzi ya fedha,na kurugenzi nyingine nyingi ambazo zimeiweka chadema kuwa taasisi.
Usishangae unapoona timu ya Tundu Lissu,Tumaine Makene, Mohamed Mtoi,Lwakatare,na John Mrema ( kutaja wachache), ccm imepata kazi kweli kiasi cha kuishi wasiyoyatengeneza.kwa mujibu wa katiba ya chama aliitekeleza
KUUNDA TAASISI
Baada ya kazi hiyo,alianza kujenga taasisi za Bawacha,Bavicha,Chaso na Baraza la wazee..
Hii ilikuwa kazi yake aliyopewa na wanachama wa chadema.amefanya kazi kubwa sana.
Bawacha ambaye ilikuwa na wanachama laki tano 2000,imepelekea kuwa na wanachama milioni tatu nchi nzima.2015
Baraza la vijana,Bavicha kutoka wanachama laki mbili,2000, kwa sasa wanachama wamefikia milioni moja. Na si kuongezeka kwa idadi tu,bali pia mabaraza haya yapo ngazi za chini kabisa ya tawi nchi nzima,huwezi kwenda Itungu,Ikungi,mahaha,longido,kyaka,matemanga,nyamagoto, Misenyi,Madabank usikute ofisi za bawacha na bavicha.
Haikutosha akishirikiana na Mh.Mbowe,na timu yake,waliona chama bila wasomi, akaunda chaso ambaye kusema kweli limekuwa zao la vijana wabunge akina Kafulila,Zitto kabwe, Halima Mdee,Mnyika na wengineo wengi wanaotarajiwa kuwatumikia watanzania kupitia Udiwani na Ubunge Mwaka huu 2015.
Baraza la wazee amelifanikisha kuliimarisha likikishauri chama kwa kiasi kikubwa.
Dr.Slaa akiamini nidhamu,uvumilivu,utu,kiasi na umoja ndio njia ya kujenga Taifa lenye Usawa,na uchapakazi alishauri chama kuwa mwaka 2013 kisingefanya uchaguzi bali kiende ngazi ya kata,tawi na kisha msingi.Uchaguzi wa serikali za mitaa umeonesha matunda ya ushauri wake.kwani chadema imeshinda kwa kishindo kuliko wanavyojinasibu ccm kuwa ushindi mdigo,maana yapo maeneo ambapo tangu uhuru 1961 ccm imekuwa ukitawala vijiji,vitongoji na mitaa,lakini safari hii maeneo hayo yameenda na chadema yote.
Watu makini,kwa kazi makini,hakika Dr.Slaa ni mtu makini asiyeyumba kwenye kusimamia kanuni,katiba sheria na taratibu. Kiongozi ambaye ni very strategic katika mipango yake.
Inaonesha,katika mahojiiano binafsi niliyofanya na watumishi wa serikali ya Tanzania,wanamuona kama kiongozi wa kupigiwa mfano ameijenga chadema viliyo kutoka falsafa ya mtu,kwenda falsafa ya kitaasisi.
Si ajabu unapoongea na watu kupitia mitandao ya kijamii nje na ndani ya nchi, kwenye twitter,facebook,jamiiforum na sciber utakuta wanasema" Dr Slaa ni hazina ya watanzania,
Na hata angepewa nchi hatawaangusha watanzania"
Chadema Kwanza
Mmesikia kwa Musa imenenwa kuwa "USIZINI" lakini Mimi nawaambia mtu atakaemwangalia mwanamke kwa jicho la kumtamani,amekwisha kuzini nae moyoni. Dr.Slaa yeye ndiye kajisogezea kabisa pasina hata ndoa.
Ni Mungu gani huyo anae shabikia uzinzi? Neema ya Mungu haiwezi kushuka sehemu yenye uchafu kama huo.
Hivi Mzee Slaa anaweza kukemea zinaa kama kweli yeye ni neema iliyotoka kwa Mungu?
fist lady wa babu atakua nan
Acha kufuru.Padri mzinzi mpora wake za watu!!!! Una mwita hazina wakati analiza watu alipora wake zao? Na analiza mke aliyemtelekeza?
Kamanda hivi UKAWA wasipomchagua Dr.Slaa mtavunja huo umoja wenu wa maghumashi?
Mkuu hivi tangu uchaguzi Mkuu mpaka sasa ni miaka mingapi imepita?je katika miaka hiyo chadema haiwezi kupata wana chama hao million 4?je chadema wakati wa uchaguzi Mkuu uliopita ilikuwa na wenyevit wa serikali za Mitaa wangapi?je Leo ina wangapi na kwa nini hilo huulizi?Uzuri wa Pro-Chadema mwenzao yeyote akija na pumba kama zinawafurahisha uwa hawezi kuhoji zaidi ya kishangilia tu bila kutimia akili zao.
Huyu mleta mada anawadanganya wenzake kuwa Bavicha na Bawacha wana wanachama milioni 4.
Ukiangalia uchaguzi mkuu ulioshapita Dr.Slaa alipata kura milioni 2 tu Tanzania.
mkuu kama Mungu angeonesha hadharani uchaguzi unaofanywa hadharani na viongozi wako wa ccm juu ya wake za watu na dada zake naamini ungeomba Ardhi ipasuke uingieMmesikia kwa Musa imenenwa kuwa "USIZINI" lakini Mimi nawaambia mtu atakaemwangalia mwanamke kwa jicho la kumtamani,amekwisha kuzini nae moyoni. Dr.Slaa yeye ndiye kajisogezea kabisa pasina hata ndoa.
Ni Mungu gani huyo anae shabikia uzinzi? Neema ya Mungu haiwezi kushuka sehemu yenye uchafu kama huo.
Hivi Mzee Slaa anaweza kukemea zinaa kama kweli yeye ni neema iliyotoka kwa Mungu?
Atakuwa mama yako anza kuwa na furaha ya kuingia magogoni kwa kuwa first lady atakuwa bimkubwa wako.
Kamwe nchi hii haiwez kutawaliwa na viongoz wa dini,padre au shekh wabaki kuwa tumikia waumin wao tu,ktk maisha yangu cjawahi kuckia Rais wa nchi yyte eti alikua Padre hyo haipo huyo nikiongoz ambae aptia viapo vingi na vizito mno vya dini yake vp cc wa dini nyingne c atatufanya kama mlinz wake Kagenzi alivo mfanya hatupo tyr kwa hayo cc watz
Watanzania wengi wanaimani na Dr. SlaaTumpeni Dr. Slaa walau tuone km kuna mabadiliko ktk uongozi make vyama vinaanzishwa havipewi fursa ya kuongoza !! Ina maana gani basi? Tukibahatika kuondoa ufisadi tutakuwa tumefanya mapinduzi ya kweli#! Hakika hatutalalamika juu ya matumizi mabaya ya resources.
Watanzania wengi wanaimani na Dr. Slaa
Kamwe nchi hii haiwez kutawaliwa na viongoz wa dini,padre au shekh wabaki kuwa tumikia waumin wao tu,ktk maisha yangu cjawahi kuckia Rais wa nchi yyte eti alikua Padre hyo haipo huyo nikiongoz ambae aptia viapo vingi na vizito mno vya dini yake vp cc wa dini nyingne c atatufanya kama mlinz wake Kagenzi alivo mfanya hatupo tyr kwa hayo cc watz
Amepata mkuu Mimi na familia yangu kura zote ndio kwa Slaa
Hata familia wanamtaka Dr. SlaaMkuu ni aibu katika karne hii wewe kuwaamulia familia yako au subordinates wako nani wampigie kura, ruhusu mawazo huru kuanzia kwenye familia yako hadi kazini kwako. Ni haki ya kikatiba mtu kuchagua kiongozi yeyote kadiri ya utashi wake.