Tatizo ninaloliona katika mada hii wengi wetu ni mashabiki badala ya kujadili maudhui ya mada iliyoletwa. Inaonekana wengi wetu hawafahamu au kupambanua mahali na nafasi ya shughuli za umma na shughuli za kichama.
Chama ni jumuia au kikundi cha watu chenye kufuata itikadi na malengo waliyojiwekea ili kujenga umoja wa kufanikisha azima yao. Iwe katika siasa, social, kazi, nk. Kwa hoja hiyo itashtua na kushangaza watu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni kutoka chama cha CCM akijaa ikulu na sare za chama chake, au akiwa katika majukumu yake kama rais awe katika sare za chama chake.
Kwa vyo vyote inavyoonjeka kwa upande wa viongozi wa serikali kutoonyesha uchama katika shughuli za kiserikali na kitaifa, vivyo hivyo hata vyama vya upinzania ambavyo havijashika dola bado viongozi wake wawapo katika majukumu au matukio ya shughuli za kitaifa ambazo zinajumuisha watu wote bila kujali itikadi za kichama wanatakiwa kuweka kando mvao unaotambuliwa na chama chao na badala yake wavae mavazi ya kawaida.
Mkuki kwa nguruwe okay, lakini kwa binadamu ni machungu. Ushabiki wa aina hiyo siko tayari kuuruhusu katika dhamiri yangu safi kwa nchi yangu. Kesho hawa hawa Chadema wataweza fanya mambo ambayo hayakubaliki kama wafanyavyo CCM maana yake tutaendelea kushabikia tu kama watu tusio na akili timamu? Huu ni utoto maana yake hakuna ukomavu wa kifikra na kiupembuzi. Hata mpinge kwa nguvu zote jambo hilo halikubaliki, na kwa imani yangu Dr. Slaa kama amesoma mada hii amenielewa.
Hata hivyo naheshimu mawazo na mchango wa kila mmoja maana akili ni nywele na kila mmoja ana zake, hivyo pamoja na kutoa mada hii sikuwa na maana kwamba wote watakubaliana, kwani wengine wanahitaji muda kuelewa, na ipo siku wataelewa niongeleayo.