Dr Slaa hajui kutofautisha mvao wa kichama na wa shughuli za kitaifa?

Kwani kumkomboa mwananchi kuna mapumziko?
Mapambano ya kuung'oa udhalimu yatakoma pale tu Chama Twawala kitakapoondolewa madarakani,
Ndipo gwanda zitakapowekwa pembeni kisha tuanze kugonga vyuti
 
Dr. Slaa anatakiwa kutofautisha akiwa katika harakati za kichama na shughuli za umma. Si kila anakokwenda ni magwanda tu, siku akiingia ikulu itakuwa ni ikulu nzima full sare za magwanda. Kwa vyo vyote viongozi wetu watofautishe nafasi za kuvaa sare za chama na nafasi ambazo za umoja wa kitaifa ambapo nguo za kwaida zinavaliwa ili mwingine asisikie vibaya kuchangamana kwa kufikiria kiitikadi.

Candid Scope,
Nilidhani hii ilikuwa nafasi nzuri kuwaelimisha watz wenzetu aina ya huduma zinazotolewa na Hospitali ya CCBRT, mathalan VVF, matatizo ya mdomo wa sungura, mtoto wa jicho huduma ambazo ni hospitali chache chache nchini zinatoa kwa kiwango cha juu cha utaalamu,kuzungumzia mafanikio na changamoto zilizoko. Mmmh! tunaishia kuzungumzia mavazi! Taifa liko kweli njia panda kama wa aina hii ndio Great Thinkers.
 
Slaa ana suti moja tu ya rangi ya jani la mgomba. Kila siku alikuwa anapiga hiyohiyo wakati akiiingia bungeni. Alivyotangaza kugombea ubunge ndiyo akapewa hivyo vijipea viwili vya magwanda ili awe anabadili na kale kasuti kake.

Hali ya kifedha ya Slaa kwa sasa si nzuri kuweza kununua suti.
Hii imetokana na kubanwa na TRA kurejesha pesa ya kodi aliyokuwa akikwepa kulipa kwenye posho zake.
Kwa sasa posho inakatwa kodi, familia imeongezeka, hivyo haitatosha kununua suti.
Magwanda ndo kimbilio ili kumlinda katika uvaaji.
 
Slaa ana suti moja tu ya rangi ya jani la mgomba. Kila siku alikuwa anapiga hiyohiyo wakati akiiingia bungeni. Alivyotangaza kugombea ubunge ndiyo akapewa hivyo vijipea viwili vya magwanda ili awe anabadili na kale kasuti kake.

kwa hiyo?
 
Matatizo ya Slaa na washamba wenzake yapo wazi sana. Haya ni matokeo ya kuzaliwa vijijini na kuja mjini ukubwani. Mtu kama Halima Mdee hawezi kufanya ushamba kama huo hata siku moja.

Dodoma kuna joto sana.
Ndo umeona humu kuna unafuu?
 
Rangi za CDM ni blue bahari, nyekundu na nyeusi ( ka nitakuwa sijakosea) Kwa hiyo magwanda si sare rasmi za CDM ...Nadhani itakuwa la maana tukiita vazi rasmi la taifa
 
Mwita 25 nae ameanza utumbo wake sasa wewe uliezaliwa mjini halafu ndo nini sasa!hilo vazi mngelifanyia kwanza ufuatiliaji mjue likoje duniani na pia kwa hapa futilieni kama ni la chama,maana mjengoni huingii na vazi la chama hata kitambaa hairuhusiwi,kumbukeni ya Mwigulu alipofaninishwa kabeba kitambaa cha CCM ilikuwa je?sio una kuja na thread ya vazi ambalo haulijui,hata mtaani kuna watu wanavaa lakini si wana CDM.
 
Huyo ndio mwanaume! Mwanaume wa ukweli hawezi kuhongwa suti na mwanaume mwenzie....!
 
Kuendelea kuchangia upuuzi mi siwezi natoka,maana naona watu wanaanza kuleta jokes au ujinga wa magamba au sijui ni kitu gani,sidhani kama huu ndio u-great thinker.
 
Back
Top Bottom