Dr Slaa hajui kutofautisha mvao wa kichama na wa shughuli za kitaifa?

Pole saana, labda haufahamu Dr. Slaa ni nani? Yeye ni Katibu Mkuu Wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Kwa hiyo anapoalikwa mahali popote anakwenda kama katibu wa CHADEMA, na si vinginevyo, kwa hiyo muda wote yupo kazini anatuwakilisaha watanzania tulio wengi kwa sababu kimsingi yeye ndo chaguo la wengi japokuwa hakuwa chaguo la tume ya uchaguzi
 
Hana nyingine
hiyo ndo sare
ya kazi manake
kwa raha gani haswa
wananji walionayo
mpaka ahangaike
kununua suti
by the way hajapata wa kunuhonga kama
nanihii!hata yeye
kama si kuuza mali zetu
angevaa zile za rangi ya kifisad
i!!!!!!!

Hebu fafanua kidooogo tu kwenye red hapo, kwamba.........asingeuza....????/
 
Kwani vazi la khaki, Slaa, na CHADEMA kipi kilitangulia. Mavazi ya Rangi hiyo yapo tangu zamani, sasa wewe (Candid Scope) values na psychological set up zake unazoziattach kwenye vazi hilo ndo linakupa tabu. Assume kwamba rangi ilikuwepo tangu zamani kisha potezea. Unahitaji kumuona Psychiatric Doctor akunomalize.
 
Yaani wewe ukiona rangi ya kaki tu unamaanisha ni sare za CDM? Haya mawazo uharo!!
 
Candid Scope, hoja yako ni dhaifu sana mkuu wangu, ingawa kuna baadhi ya wabishi na kwa makusudi wanatak ku prlong hii thread wanakuunga mkono kwa hoja dhaifu kama uliyoitoa hapo.

Nina swali nataka nikuulize:

Hivi kanzu ni vazi la kidini?
mbona enzi za Ali Hassan mwinyi alikua akilivaa sana katika shughuli za kitaifa na hakuna aliyejali? bado tunaona wabunge kama Adam Malima anatinga Kanzu mpaka mjengo na hakuna anayeongea ( Bungeni vazi rasimu inajulikana ni suti) kule Zanzibar wawakilishi ni kama sale ya kuingilia barazani hakuna anayeuliza..

Wakuu wa mikoa na Wilaya wanavaa sare za Chama katika shughuli za kitaifa mbona hujaji?

Na hiyo Picha uliyoweka hapa unajua ilipigwa katika Mazingira gani? ( labda Dr Slaa alikuwa katika shughuli za kiofsi akaletewa ujumbe ndio akafika pale, au ulikuwa unategemea angeenda mpaka kwake akavae Suti?

Thread yako ni Trash kabisa mkuu, na unavyoendelea kuitetea Reputation yako inashuka humu ndani, kubali umeteleza tusonge mbele au kama nyamaza kimya..

Mwisho: au unataka lianzishwe jukwaa la Mavazi na Mitindo humu JF?? ongea na Invisible anaweza kukufikiria
 
Matatizo ya Slaa na washamba wenzake yapo wazi sana. Haya ni matokeo ya kuzaliwa vijijini na kuja mjini ukubwani. Mtu kama Halima Mdee hawezi kufanya ushamba kama huo hata siku moja.

pole hivi na wewe ni wa mjini.
 
Mbona mnakwepa hoja zangu na kujenga tu utetezi wa kumlinda Slaa na hoja ya mvao huo? Makinda pale angevaa ya CCM hapa ninyi wenyewe mnaopinga hapa mngemsema mama huyu hadi kufikia kutapika matusi ya nguoni.

Mara nyingi hapa kumetokea malalamiko kwamba viongozi wa CCM na wa serikali wamekuwa wakivaa sare za chama wakati wanafanya shughuli za umma au taifa. Hakuna hata mmoja kati ya ninyi mnaopinga kujibu swali la malalamiko ya muda mrefu ambayo yamekuwepo hapa Jamii Forums kuhusu nafasi ya mavazi ya chama katika shughuli za chama na shughuli za umma au kitaifa kuwatetea ila kutukana tu. Mara nyingi tu tumekuwa tukijadili viongozi waonyeshe tofauti ya shughuli za kichama na shughuli za umma au kitaifa.

Leo kwa kuwa jambo hilo linamhusu Dr. Slaa basi ukweli umechepushwa na kujenga hoja ya kutetea na kuwa ni haki kufanya hivyo, ila kwa CCM si haki. Kutolipa posho mishahara ya viongozi wa Chadema hapa Jamii Forums hawakuona kama kosa, lakini ingejulikana wazi kama viongozi wa CCM wanafanya hivyo kungekuwa na malalamiko mengi tu hapa JF.

Ninyi ndio mna utetezi dhaifu kabisa kwani mnachokifanya ni kushabikia mtu na chama bila kufuata misingi ya haki za msingi kwa mtazamo wa wananchi wote. Lakini hamtumii busara kuona kwamba kuruhusu jambo hilo liendelee litafanya mambo mengine pia yafunikwe funikwe kama CCM ifanyavyo kwa kile moyo ukipenda bila bila uchambuzi wa kiakili tutaendelea na dhima ya kulindana tu bila kukosoana, hii ni kasoro kubwa na tatizo kwa sisi waafrika.

Wengi hapa hawapendi kabisa kuona viongozi wa serikali wakivaa mavazi ya chama, au matukio ya umma baadhi ya viongozi wa serikali kuvaa mavazi ya chama. Kwa maana hiyo hawa viongozi wa Chadema kujenga mazoea ya kuvaa sare zilizozoeleka kama za chama chao hata katika nafasi ambazo si za matukio ya kichama bali ni matukio ya umma yanayojumuisha watu mbalimbali wa makundo yote bila kujali itikadi za kichama ni udhaifu wa mtazamo wa jumla katika mambo ya umma au kitaifa, hii ni kasoro kubwa inayohitaji kukosolewa na kusahihiswa.

Mvao una maana yake, na dio maana kiitikadi na kichama kunakuwa mvao au rangi fulani inayoonyesha utambulisho wao. Hilo linaeleweka, na pia mazingira ni jambo la msingi kusoma wapi unaenda na kwa shughuli gani unaenda kufanya, na hivyo uwe na mvuto kwa utakaokutana nao kwani katika umma utakutana na watu wa makundi yote iwe wa vyama vya siasa, wasio wanasiasa, viongozi wa dini, watu wa kimataifa nk. Kama utavaa vazi la CCM hata kwenye arusi au kanisani na msikitini au sherehe za uhuru wa Tanganyika tutakuona una upungufu fulani kwani jambo hilo si la kiitikadi za CCM bali umma wote wa watanzania wenye itikadi tofauti. Vinginevyo kuendekeza jambo hilo ipo siku ukivaa vazi kama hilo utajisikia uko peke yako na kichokoo kwa vile si mahali pake. Juzi hapa wengi wametoa malalamiko kwamba sherehe za Uhuru zimegubikwa na UCCM badala ya utaifa. Hapa naona kabisa kasoro kubwa ya wengi wetu kupinga tu bila kuangalia upande wa pili wa sarafu.

Mbunge Zitto kabwe ni mfano mzuri wa mmoja wa viongozi wa Chadema ambaye anakuwa makini wapi anatakiwa kutinga na magwanda na wapi si pa kutinga na magwanda.

Juu ya mvao wa kiarabu (kiislamu) ni jambo linaloeleweka ambalo si vema kulijadili hapa kutokana na unyeti wake ambao kila mmoja wetu anajua kama ukipinga lisivaliwe nini kitatokea tunajua, jambo hilo tunaliita ni common sense. Ni jambo la kiimani na si kiitikadi. Ni dhahiri Kardinali Pengo ukimwalika hatavaa UCCM, Uchadema, UCUF nk, bali ni kiongozi wa kiroho tofauti na kiongozi wa kisiasa na hakuna anayeshangaa hilo. Hakuna atayashangaa, lakini wengi watashtuka kumwona Kikwete ametinga jukwaani kwenye sherehe za kitaifa amevalia kanzu ya barakashia. Kwani yeye kiogozi wa kitaifa bila kuja itikazi za kichama au dini. Hivyo anatakiwa avae mvao usioleta hisia mbaya kwa baadhi ya wananchi wake.

Picha iliyopigwa hapa ilikuwa katika mazingira yaliyokuwa na ratiba maalumu kwa muda mrefu na yeye Slaa akiwa kama mwenyeji wa kumpokea Makinda pale. Nadhani hilo nimekujibu pia.

Tujitahidi kujadili na kupima mambo kwa akili na isiwe kwa mtindo ambao nimeona ni wa kishabiki au kile moyo ukipenda tutarudi kule kule kwa yanayojilia kwenye CCM hadi chombo kinaenda mrama bado wako ngangari kutetea na kulindana uozo unazidi kusambaa na kuhalalishwa hakuna cha kuvuana magamba tena. Lazima kujenga na kuruhusu hali ya kukosoana, kusahihishana na kuangalia mambo katika manufaa ya umma wote na wawapo katika shughuli za kichama iwe kwa utaratibu wa chama.
 
Dodoma nipo kikazi tu lakini uliza historia yangu uambiwe.

historia yako itabaki kuwa yako tu haina nafasi na wala umuhimu wowote kwa mtu kuijua, toa mawazo yenye maana kulingana na hali halisi: kwaheri.
 
Eti na wewe umefikiria? Utumwa mbaya. Halafu chadema hawana sare rasmi. Hizo combat unazoziona mitaani sio vazi rasmi la chama. Umewezaje kulogin? Mbona unaonyesha kama hujui lolote?

Watanzania wenzangu tukue pamoja na taifa, tufikiri kama watu ambao tuna umri wa miaka 50 tunayosherehekea, vinginevyo tunaendelea mtindo wa KiCCM.

Tunatakiwa kujenga na kuimarisha dhana ya kukosoana, kusahihishana na kuwa na hulka ya kushauriana pale tunapoona mkondo wa kujengeka matabaka unajitokeza, huo ndio mwono mpana na wenye manufaa na maslahi kwa kudumisha mshikamano na amani kwa taifa letu.

Kushabikia kila kitu tu kiwe kibaya au kizuri anachofanya kiongozi tunayempenda kinaweza kumharibu hata akafanya mambo mengine kwa kuwapendeza wananchi bila kuangalia athari zake kwa jamii mbalimbali zinazounda taifa zima. Hivyo wengi wetu tunahitaji kujenga na kuulinda mtazamo wa kitaifa zaidi na mambo ya kichama yawe na dhamira nzuri ya kujenga utaifa badala ya kitabaka.

Hii dhana ya kuwalinda viongozi kwa nguvu zote hata pale wanapoteleza kidogo au pale wanapotakiwa kutumia tu busara ya kawaida kupima mazingira na shughuli wanayokwenda kufanya ndio kujengeka kwa tabia mbaya ambayo imekiharibu chama cha CCM kujenga mfumo wa kulindana iwe ndani ya chama au serikalini, matokeo yake sasa yako hadharani.

Ushabiki wa kiitikadi ni hatari sana maana unaharibu viongozi na kuwaona miungu na wao kujisikia kama wanastahili hivyo. Naweza kufananisha ushabiki huu na dereva anayeendesha gari la abiria. Dereva anaendesha gari kwa kasi, na abiria wanafurahia huku wakimhamasisha kwa ule wimbo mzuri usemao
"dereva chechema chechema na gari X2, tupate kuona ufundi wa gari X2. Kitakachotokea baada ya dereva kuvimbishwa kichwa ni kuhamasika kuongeza speed, na matokeo yake watakaonusurika watajutia wakati wako chumba cha dharura hospitalini, kwa vile hawakuangalia athari zinazoweza tokea kwa kumhamasisha dereva kuendesha gari kupitiliza speed limit.

Ni kawaida yangu kuipinduapindua sarafu pande zote, kwani kuona upande mmoja nitakuwa nimekosa details ambazo ziko upande mwingine, kwani kuifahamu vizuri sarafu unatakiwa uone pande zote, ndipo unapoweza kuitofautisha na sarafu nyingine.

Unataka uwe mshauri wake wa mavazi!

Au kwa vile kombati ni ngumu kama jinsi utatuambia ni uhuni.
 
Unataka uwe mshauri wake wa mavazi!

Au kwa vile kombati ni ngumu kama jinsi utatuambia ni uhuni.

Na ndivo utakavyotuambia we unafikiri utasema ni?

Kombati ni ngumu kama jinsi kwaiyo dr muhuni,au mnasemaje jamani?

Tatizo lenu hamtaki kukosolewa.

Hahaha huyu mtoa mada sijui aliwaza nini hahaha
 
Mleta mada unaweza kuniambia mavazi ya shughuli za kitaifa ni yapi hayo na ni kwa mujibu wa nani?
 
Huyo ndio mwanaume! Mwanaume wa ukweli hawezi kuhongwa suti na mwanaume mwenzie....!

lakini wakati huo huo kuna chama kinapata 40% ya pesa ya kuendeshea chama kutoka kwa mr Davy cameroon.ha ha haa!it means all fellowers wa .....
 
Matatizo ya Slaa na washamba wenzake yapo wazi sana. Haya ni matokeo ya kuzaliwa vijijini na kuja mjini ukubwani. Mtu kama Halima Mdee hawezi kufanya ushamba kama huo hata siku moja.

Mwita,yani kitendo cha wewe kuijua dar au kuzaliwa Dar unajihisi eti unaijua miji kuliko Dr na akina sisi?ama kweli usimuulize kipofu ukubwa wa sikio la tembo.Siku ukiijua miji utajiona mjinga kwa kudhani alozaliwa Dar ndo wa mujini.
 
Katika medani ya kisiasa mtu anapokuwa maarufu anahitaji kuwa na strategist ambaye atamfunda katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kuongea, watu atakaokutana nao na nini mood inayofaa kwa aina, rika na mtazamo wa watu atakaoongea nao.

Kuna kuwa na mbunifu wa kumwandaa namna bora ya kuonekana atokeapo kwenye hadhara, maana mwonekano wa nje nao ni sehemu ya mvuto kwa jamii, namna gani ya kutengeneza nywele zake ili kumpendezesha, kwa mfano seneta Kerry alipokuwa anagombea urais wa Marekani akiwa mpinzaniwa Bush, nywele zake zilikuwa kubwa mno, akashauriwa azipunguze ili kuonekana mzuri zaidi kuliko nywele zake zilivyokuwa zinatia uvivu kuziangalia.

First lady mtazamiwa kwa wenzetu walio na upeo na uzoefu ni mtu muhimu katika kumwandaa rais kwa vile yuko muda mwingi naye na ni mtoaji wa ushauri wa kwanza wawapo peke yao huwa wana nafasi ya kujadili majukumu ya rais. Ndio maana first lady naye huwa katika midahalo ya kampeni na anaulizwa na kupimwa uwezo wake katika masuala ya jamii.

Kwa vyo vyote ulimwengu wa leo tofauti na kizazi kilichopita, na tuongeleayo hapa ni mambo mazuri na muhimu kwa viongozi watazamiwa kujifunza na kuyatendea kazi.

Tuhataka Kamanda Mbowe na Dr. Slaa wakati mwingine watokee na mvao wa kawaida, wa kichama na ule wa kimataifa ili tujue watakapotuwakilisha kimataifa wataonekanaje. Wasije ingia United Nation na magwanda wakaonekana kichokoo. Kuwa rais si kutembelea vijiji tu, kuna mambo chungu nzima, na sasa wana nafasi ya kujifunza namna ya kufanya watakaposhika dola. Tusione haya kuwakosoa na wawe radhi kukosolewa ili wajifunze, maana elimu haina mwisho hadi tutakapozawadiwa sanda.
 
Back
Top Bottom