Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,367
- 100,408
wewe Kimbunga nilikuwa nakuona mchangiaji wa maana hapa JF kumbe ni walewale tu yaani unaenda kuokoteza habari za vijiwe vya kahawa uswahilini unaleta JF? shame on you! jipange au na wewe gamba??
ukiondoa kufukuzwa na chama mi nadhani hata kuhamia chama kingine kunakufanya kuwa si manachama mwaminifu wa ccm,labda kama kuna katiba mpya ya ccm inayotambua hata watu waliohama chama kuwa wanachama waokweli shule na vyuo vyetu vina kazi sana kama ndio watu wanafikiri hivi. Kama hajarudisha manake kuwa anayo? Yaani hakuna uwezekano mwingine wowote ule? Mimi pia niliwahi kuwa na kadi ya CCM na hadi leo sijairudisha na sina mpango wa kuirudisha....
CLUE: Uanachama wa CCM unakomaje?
kweli shule na vyuo vyetu vina kazi sana kama ndio watu wanafikiri hivi. Kama hajarudisha manake kuwa anayo? Yaani hakuna uwezekano mwingine wowote ule? Mimi pia niliwahi kuwa na kadi ya CCM na hadi leo sijairudisha na sina mpango wa kuirudisha....
CLUE: Uanachama wa CCM unakomaje?
Hivi hata usiporudisha kadi Katiba ya CCM inasema hivi kuhusu uanachama:
7. (1) Mtu akikubali kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo:-(a) Atatoa kiingilio cha Uanachama(2) Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.
(b) Atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda anaweza kulipa ada ya mwaka mzima mara moja.
(c) Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa
(3) Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:-(a)Kufariki.(4) Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.
(b)Kujiuzulu mwenyewe.
(c)Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d)Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e)Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f)Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.
Nape, Katibu Mwenezi wa Chama anapaswa ajue haya.
My take:
Uongo na kuchafuana bado vinatumika kama mtaji wa kisiasa. Watu wameshaamka, tutumie mambo yenye maslahi ya nchi kufanya siasa.
Kama hajarudisha kadi, Nape anataka kuwaambia wana CCM kuwa Slaa bado mwana CCM?
Nnauye Jr, mtu akishaacha kulipa ada, au kujiunga rasmi na chama kingine si lazima arudishe kadi. Anakuwa si mwanachama kwa mujibu wa katiba ya CCM.
Mkuu OSOKONI vijiweni ndiko kuna wapiga kura. Hapa JF kuna wachambuzi. Usipuuze habari za vijiweni. Nakushauri uwe unajichanganya vijiweni ili uweze kupata habari nyingi ambazo huwa hazipatikani hapa JF.
Hii post ni ya siku nyingi kabla Nnape hajasema kuwa dr. ana kadi ya CCM!
Well said!Kinachonikera ni siasa zinazojengwa katika upotoshaji, uongo, vijimaneno n.k. badala ya mambo yenye maslahi kwa maendeleo ya nchi yetu!
Siasa hizi bado zinategemea upumbavu wa wananchi kuendelea kukubalika. Ndio mtaji ambao Nape anatumia.
Chama tawala kilipaswa kuonesha mfano katika hili jambo. Na wananchi wanazidi kuamka kwa kuona uongo na upotoshaji wa wazi kama huu.
Arudishe asirudishe mamoja!Hivi, Mchezaji wa Simba akihamia Yanga jezi zote za simba atazirudisha?
Wengi hamjamuelewa Nape anamaanisha nini? ni kwamba ukienda kinyume na CCM basi urudishe ile kadi yao, ila kama haujarudisha wewe bado ni CCM. na wana CCM ni pamoja na hawa;Katibu Mwenezi wa CCM hajui uanachama wa CCM unaishaje!