Baada ya kamanda Makongoro Wasira kujiunga na M4C siku chache zilizopita, leo tena watoto wengine wa Wasira wamejiunga na M4C na kukitupia virago Chama cha Baba yao CCM. Waliojiunga leo katika Makao makuu ya Chadema na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa ni kamanda Ester Wasira na Lilian Wasira.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa kadi walikuwa na haya ya kusema:Ester wasira: (Ni mwanasheria, graduate wa UDSM)
(i) Chadema ni Chama cha kizalendo na mkombozi wa dhati wa Mtanzania.
(ii) Chadema kinaleta matumaini mapya kwa Watanzania hasa vijana wasio na kazi na matumaini, Watanzania wenye maisha magumu hata kushindwa kumudu milo miwili kwa siku, akina mama wanaohangaika vijijini bila matibabu ya uhakika, maji, umeme, nyumba bora nk
(iii) CCM imedumaza nchi, nchi imekuwa kama mtu aliyedumaa kwa kukosa protein, haikui tena, Chadema ni damu mpya yenye kuweza kuingiza protein kwenye mishipa ya nchi iweze kufufuka na kukua tena.
(iv) Chadema kina viongozi imara na kwa maneno na matendo yake wanawadhihirishia watanzania kuwa ni waadilifu na wana nia njema ya kuipeleka Tanzania mbele. Alimalizia kwa kuwaasa vijana, akina mama na wazee wajiunge na M4C ili kuijenga Tanzania mpya. Alimalizia kwa kusema, Kwa msaada wa Mungu, Tanzania Mpya inakuja.
Lilian Wasira (Mwanasheria, graduate wa TUDARCO):
(i) Alielezea furaha yake kwa kujiunga na Chama makini na chenye kuleta matumaini mapya kwa mtanzania
(ii) Aliwaasa vijana, akina mama na wazee wajiandikishe kwa wingi nafasi itakapotokea na 2015 wakamalizie kazi ya ukombozi kwa kuipigia Chadema kura
(iii) Amewaasa Watanzania kuacha kulalamikia maovu ya CCM na kuchukua hatua ya kuiweka CCM pembeni na kuleta Chadema kama chama mbadala. Alisema hakuna sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama watanzania hawathubutu kuchagua chama mbadala na badala yake kuendelea kuichagua CCM na kulalamika kila siku kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi
(iv) Kwamba CCM imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 hivyo ni wakati sasa wa kuiweka pembeni na kuingiza chama kipya, mawazo mapya na kujenga mfumo mpya wa uongozi. Hakuna kitu CCM imeshindwa kufanya kwa miaka 50 inaweza kufanya kwa miaka 5 au 10 ijayo.
(v) Anasema ana imani na sera za chadema kuwa ndizo zitatukomboa. Amewapa moyo viongozi wa Chadema wasitishwe na vitisho na mauaji yanayofanywa na dola na kusema yupo tayari kwa M4C na yupo tayari kulipuliwa kama walivyolipuliwa wanachadema wengine na kuuawa kama itambidi afanye hivyo.
(vi) Kwamba Chadema ni Chama kinachosubiri kuingia Ikulu isipokuwa tu watu wajiandikishe, wapige kura na walinde kura.
(vii) Nae alimalizia kwa kusema Kwa msaada wa Mungu Tanzania mpya inakuja.Dr Slaa alitiwa moyo sana na ujasiri ulioonyeshwa na vijana hawa pamoja na maneno ya kizalendo waliyoongea na akawakarisha kwenye uwanja wa mapambano ya M4C.
Peopleeeeeeeeeeeeees poweeeeeeeeeeeeeeer
Mzee Wasira upo? narejea maneno yako pale jangwani 10.06.2012 kwamba 'Mbowe ATAPATA LAANA YA WAZEE' kwa kuwa hatambui kazi nzuri iliyofanywa na Mzee Aikael Mbowe pamoja na Nyerere (akimaanisha kwa nini Mbowe yuko CDM) Je Wasira utawalaani na hawa watoto kwa kuwa hawaitambui kazi yako na ccm?
anayeichimbia CDM kaburi atatumbukia mwenyewe.....
Habari njema sana . Ndio ccmweli wajue sasa nguvu ya cdm!
*******************
Cdm haitafikisha mwaka-wassira
Hawa mabinti ni watoto wa KAKA YAKE Steven Wassira (Mzee wa Gombe), Baba yao anaitwa George Wassira, kwa hiyo ni familia ya Wassira na kusema 'Watoto wa Wassira" ni sahihi na wala sio upotoshaji kama magamba wanavyojaribu kupotosha. Nakumbuka wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru suala la Vicent Nyerere lilivyowatoa jasho magamba lakini bado wakaangukia puaTunakaribia kupata ukombozi sasa.Ninachojua ni kwamba hao si watoto wa Wasira maana hawafanani naye hata kidogo. Hao watoto wa baba mwingine kabisa kwa hiyo wasira hatasema kitu zaidi ya kukubaliana na mawazo yao maana ni watu wazima.
Kama ni watoto wake, basi walichukizwa na kitendo cha baba yao (WASIRA) kusinzia sinzia kila wakati kama ana sleeping sickness (UGONJWA WA KUSINZIA SINZIA KILA MARA).
Mh wanafanana na mama yao,japo sijamuona .
Ha ha ha ha ha ha ha.. Mkuu umenichekesha mno yaani.. Kweli JF ni zaidi tiba..
Unamaana hawafanani na babayao? Hapa sijaelewa vizuri.
Ni kweli Bushloiyaiz. Si watoto wa Steven Wassira. Hebu na wataje majina matatu. Inaonekana ( it appears) ni watoto wa ndugu yake tyson na inaonekana ( it seems) familia hizo mbili hawaelewaniSio watoto hasa wa tyson,kama sikosei wanamwita tyson baba mkubwa or something.
Nani amekuambia familia hazielewani? Labda kama hawaelewani kwa kutofautiana kimtazamo kuhusu ni chama kipi chaweza kujengaTanzania tunayoitaka. Usibuni tu mambo kwa kusema vitu ambavyo havipoNi kweli Bushloiyaiz. Si watoto wa Steven Wassira. Hebu na wataje majina matatu. Inaonekana ( it appears) ni watoto wa ndugu yake tyson na inaonekana ( it seems) familia hizo mbili hawaelewani
Ni kweli Bushloiyaiz. Si watoto wa Steven Wassira. Hebu na wataje majina matatu. Inaonekana ( it appears) ni watoto wa ndugu yake tyson na inaonekana ( it seems) familia hizo mbili hawaelewani
ni wa George Wasira! Baba yao anaishi kibaha,na aliwatelekeza toka wakiwa wadogo akaoa mke mwngne! So wao hawaelewan na ding yao! Wanaishi ukonga.