Dr Slaa awakabidhi Kadi Makamanda Ester Wassira na Lilian Wassira

Baba yao je hakuwahi kuhama kama nakumbuka vizuri?aligombea hata ubunge.mtoto wa nyoka hatabadilika kuwa wa mnyoo ataendelea kuwa na sumu ya njoka
 
Baada ya kamanda Makongoro Wasira kujiunga na M4C siku chache zilizopita, leo tena watoto wengine wa Wasira wamejiunga na M4C na kukitupia virago Chama cha Baba yao CCM. Waliojiunga leo katika Makao makuu ya Chadema na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa ni kamanda Ester Wasira na Lilian Wasira.

Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa kadi walikuwa na haya ya kusema:
Ester wasira: (Ni mwanasheria, graduate wa UDSM)

(i) Chadema ni Chama cha kizalendo na mkombozi wa dhati wa Mtanzania.
(ii)
Chadema kinaleta matumaini mapya kwa Watanzania hasa vijana wasio na kazi na matumaini, Watanzania wenye maisha magumu hata kushindwa kumudu milo miwili kwa siku, akina mama wanaohangaika vijijini bila matibabu ya uhakika, maji, umeme, nyumba bora nk

(iii)
CCM imedumaza nchi, nchi imekuwa kama mtu aliyedumaa kwa kukosa protein, haikui tena, Chadema ni damu mpya yenye kuweza kuingiza protein kwenye mishipa ya nchi iweze kufufuka na kukua tena.

(iv)
Chadema kina viongozi imara na kwa maneno na matendo yake wanawadhihirishia watanzania kuwa ni waadilifu na wana nia njema ya kuipeleka Tanzania mbele. Alimalizia kwa kuwaasa vijana, akina mama na wazee wajiunge na M4C ili kuijenga Tanzania mpya. Alimalizia kwa kusema, “Kwa msaada wa Mungu, Tanzania Mpya inakuja.


Lilian Wasira (Mwanasheria, graduate wa TUDARCO)
:
(i)
Alielezea furaha yake kwa kujiunga na Chama makini na chenye kuleta matumaini mapya kwa mtanzania

(ii)
Aliwaasa vijana, akina mama na wazee wajiandikishe kwa wingi nafasi itakapotokea na 2015 wakamalizie kazi ya ukombozi kwa kuipigia Chadema kura

(iii)
Amewaasa Watanzania kuacha kulalamikia maovu ya CCM na kuchukua hatua ya kuiweka CCM pembeni na kuleta Chadema kama chama mbadala. Alisema hakuna sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama watanzania hawathubutu kuchagua chama mbadala na badala yake kuendelea kuichagua CCM na kulalamika kila siku kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi
(iv) Kwamba CCM imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 hivyo ni wakati sasa wa kuiweka pembeni na kuingiza chama kipya, mawazo mapya na kujenga mfumo mpya wa uongozi. Hakuna kitu CCM imeshindwa kufanya kwa miaka 50 inaweza kufanya kwa miaka 5 au 10 ijayo.
(v)
Anasema ana imani na sera za chadema kuwa ndizo zitatukomboa. Amewapa moyo viongozi wa Chadema wasitishwe na vitisho na mauaji yanayofanywa na dola na kusema yupo tayari kwa M4C na yupo tayari kulipuliwa kama walivyolipuliwa wanachadema wengine na kuuawa kama itambidi afanye hivyo.

(vi) Kwamba Chadema ni Chama kinachosubiri kuingia Ikulu isipokuwa tu watu wajiandikishe, wapige kura na walinde kura.
(vii) Nae alimalizia kwa kusema “Kwa msaada wa Mungu Tanzania mpya inakuja.”Dr Slaa alitiwa moyo sana na ujasiri ulioonyeshwa na vijana hawa pamoja na maneno ya kizalendo waliyoongea na akawakarisha kwenye uwanja wa mapambano ya M4C.


Peopleeeeeeeeeeeeees poweeeeeeeeeeeeeeer

Hii siyo issue kabisa. Usijekuta wanaingiza mamluki
 
Mzee Wasira upo? narejea maneno yako pale jangwani 10.06.2012 kwamba 'Mbowe ATAPATA LAANA YA WAZEE' kwa kuwa hatambui kazi nzuri iliyofanywa na Mzee Aikael Mbowe pamoja na Nyerere (akimaanisha kwa nini Mbowe yuko CDM) Je Wasira utawalaani na hawa watoto kwa kuwa hawaitambui kazi yako na ccm?
anayeichimbia CDM kaburi atatumbukia mwenyewe.....

Hata mm mkuu, nina hamu sana ya kusikia kauli ya Wasira kwani alitamka haya maneno makali kwa urahisi sana, haya ndo mambo ya kuongea kwa kukurupuka
 
Karibuni sana makamanda tujenge nchi yenye kuzingatia haki na utu wa mwanadamu. Mungu awape maisha marefu.
 
Kweli nimeamini Wasira ni kichwa ameangalia upepo wa ccm ameona lazima 2015 cdm ichukue nchi hivyo amewashauri wanae wajiunge cdm ili 2015 waweze kuingia kwenye system. Nadhani hta baba riz1 karibu atawashawishi watoto wake wawahi nafasi cdm
 
Kama siyo tamaa ya madaraka MH. Steven Wassira angekuwa upinzani mpaka sasa. Kwa wale wasiojua, Wassira ambaye ni mbunge na waziri kupitia CCM alishawahi kuhamia NCCR MAGEUZI na akagombea ubunge kwa kupitia NCCR na akashinda then kwa tamaa akarud CCM
 
Habari njema sana . Ndio ccmweli wajue sasa nguvu ya cdm!
*******************
Cdm haitafikisha mwaka-wassira

Inaonekana wewe hufanyi kabisa research wewe, watoto wengi tu wa wakubwa, wengine wakubwa wa usalama wa taifa, wazazi wao wanawakati mgumu sana majumbani mwao, watu hawataki kuwa wanafiki kabisa, wanaona wafanye/waseme kile kinachowasukuma toka ndani ya mioyo yao, binafsi nimefanya kautafiti kadogo tu na nimegundua hilo, nilikuwa nasoma mara nyingi gazeti la Raiamwema ile makala ya Hidaya na mpenziye Frank, mara nyingi nilikua simwamini mwandishi kuhusu maisha ya waziri yule wa serikali ya mikiki, tena inaelekea wakati fulani mwandishi ni kama alikua anamsema Wasira huyu huyu, binti siku moja akabandika picha ya babaye akiwa anauchapa usingizi kikaoni kwenye wall ya face book, waziri aliye recordiwa akifanya hayo alikua huyu huyu Tyson, nilipo sikia suala la yule mwanae aliopo US nikajua kumekucha, so mkuu, usijidanganye ka eti ni ma spy, hii ndio hali halisi ya Tanzania kwasasa, nimalizie kwakusema hivi; Ukiona mtu anaipenda ccm ujue aidha ni mjinga, haelewi uhusiano wa maisha ya kila siku na siasa au mtu huyo ni fisadi/anafaidika na mfumo wa kifisadi nje ya hapo, huwezi kuipenda ccm hata kidogo, hata hao wanaipenda ccm kwasababu viongozi wengi ni wa dini yao, ni ujinga tu ndio unaowasumbua, sio kitu kingine!
 
Tunakaribia kupata ukombozi sasa.Ninachojua ni kwamba hao si watoto wa Wasira maana hawafanani naye hata kidogo. Hao watoto wa baba mwingine kabisa kwa hiyo wasira hatasema kitu zaidi ya kukubaliana na mawazo yao maana ni watu wazima.
Kama ni watoto wake, basi walichukizwa na kitendo cha baba yao (WASIRA) kusinzia sinzia kila wakati kama ana sleeping sickness (UGONJWA WA KUSINZIA SINZIA KILA MARA).
Hawa mabinti ni watoto wa KAKA YAKE Steven Wassira (Mzee wa Gombe), Baba yao anaitwa George Wassira, kwa hiyo ni familia ya Wassira na kusema 'Watoto wa Wassira" ni sahihi na wala sio upotoshaji kama magamba wanavyojaribu kupotosha. Nakumbuka wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru suala la Vicent Nyerere lilivyowatoa jasho magamba lakini bado wakaangukia pua
 
Sio watoto hasa wa tyson,kama sikosei wanamwita tyson baba mkubwa or something.
Ni kweli Bushloiyaiz. Si watoto wa Steven Wassira. Hebu na wataje majina matatu. Inaonekana ( it appears) ni watoto wa ndugu yake tyson na inaonekana ( it seems) familia hizo mbili hawaelewani
 
Ni kweli Bushloiyaiz. Si watoto wa Steven Wassira. Hebu na wataje majina matatu. Inaonekana ( it appears) ni watoto wa ndugu yake tyson na inaonekana ( it seems) familia hizo mbili hawaelewani
Nani amekuambia familia hazielewani? Labda kama hawaelewani kwa kutofautiana kimtazamo kuhusu ni chama kipi chaweza kujengaTanzania tunayoitaka. Usibuni tu mambo kwa kusema vitu ambavyo havipo
 
Hili linatoa changamoto kwa watoto wa waakubwa kuwa fikiria kwa kichwa chako unga mkono ukombozi badala ya kufuata mkumbo wa wazazi wako
 
Ni watoto wa wassira mwingine and not steven,baba yao ni wakili,george wassira,
 
Ni kweli Bushloiyaiz. Si watoto wa Steven Wassira. Hebu na wataje majina matatu. Inaonekana ( it appears) ni watoto wa ndugu yake tyson na inaonekana ( it seems) familia hizo mbili hawaelewani

ni wa George Wasira! Baba yao anaishi kibaha,na aliwatelekeza toka wakiwa wadogo akaoa mke mwngne! So wao hawaelewan na ding yao! Wanaishi ukonga.
 
ni wa George Wasira! Baba yao anaishi kibaha,na aliwatelekeza toka wakiwa wadogo akaoa mke mwngne! So wao hawaelewan na ding yao! Wanaishi ukonga.

We are missing a point. Tujadili sababu wanazosema zimewapeleka kwenye chama cha ukombozi badala ya hizi hadithi ambazo mbali na kwamba hazina ushahidi hazitusaidii katika hoja iliyopo mbele yetu
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom