Dr Slaa awakabidhi Kadi Makamanda Ester Wassira na Lilian Wassira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa awakabidhi Kadi Makamanda Ester Wassira na Lilian Wassira

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by clementi, Sep 29, 2012.

 1. c

  clementi New Member

  #1
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 27, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kamanda Makongoro Wasira kujiunga na M4C siku chache zilizopita, leo tena watoto wengine wa Wasira wamejiunga na M4C na kukitupia virago Chama cha Baba yao CCM. Waliojiunga leo katika Makao makuu ya Chadema na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa ni kamanda Ester Wasira na Lilian Wasira.

  Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa kadi walikuwa na haya ya kusema:
  Ester wasira: (Ni mwanasheria, graduate wa UDSM)

  (i) Chadema ni Chama cha kizalendo na mkombozi wa dhati wa Mtanzania.
  (ii)
  Chadema kinaleta matumaini mapya kwa Watanzania hasa vijana wasio na kazi na matumaini, Watanzania wenye maisha magumu hata kushindwa kumudu milo miwili kwa siku, akina mama wanaohangaika vijijini bila matibabu ya uhakika, maji, umeme, nyumba bora nk

  (iii)
  CCM imedumaza nchi, nchi imekuwa kama mtu aliyedumaa kwa kukosa protein, haikui tena, Chadema ni damu mpya yenye kuweza kuingiza protein kwenye mishipa ya nchi iweze kufufuka na kukua tena.

  (iv)
  Chadema kina viongozi imara na kwa maneno na matendo yake wanawadhihirishia watanzania kuwa ni waadilifu na wana nia njema ya kuipeleka Tanzania mbele. Alimalizia kwa kuwaasa vijana, akina mama na wazee wajiunge na M4C ili kuijenga Tanzania mpya. Alimalizia kwa kusema, "Kwa msaada wa Mungu, Tanzania Mpya inakuja.


  Lilian Wasira (Mwanasheria, graduate wa TUDARCO)
  :
  (i)
  Alielezea furaha yake kwa kujiunga na Chama makini na chenye kuleta matumaini mapya kwa mtanzania

  (ii)
  Aliwaasa vijana, akina mama na wazee wajiandikishe kwa wingi nafasi itakapotokea na 2015 wakamalizie kazi ya ukombozi kwa kuipigia Chadema kura

  (iii)
  Amewaasa Watanzania kuacha kulalamikia maovu ya CCM na kuchukua hatua ya kuiweka CCM pembeni na kuleta Chadema kama chama mbadala. Alisema hakuna sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama watanzania hawathubutu kuchagua chama mbadala na badala yake kuendelea kuichagua CCM na kulalamika kila siku kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi
  (iv) Kwamba CCM imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 hivyo ni wakati sasa wa kuiweka pembeni na kuingiza chama kipya, mawazo mapya na kujenga mfumo mpya wa uongozi. Hakuna kitu CCM imeshindwa kufanya kwa miaka 50 inaweza kufanya kwa miaka 5 au 10 ijayo.
  (v)
  Anasema ana imani na sera za chadema kuwa ndizo zitatukomboa. Amewapa moyo viongozi wa Chadema wasitishwe na vitisho na mauaji yanayofanywa na dola na kusema yupo tayari kwa M4C na yupo tayari kulipuliwa kama walivyolipuliwa wanachadema wengine na kuuawa kama itambidi afanye hivyo.

  (vi) Kwamba Chadema ni Chama kinachosubiri kuingia Ikulu isipokuwa tu watu wajiandikishe, wapige kura na walinde kura.
  (vii) Nae alimalizia kwa kusema "Kwa msaada wa Mungu Tanzania mpya inakuja."Dr Slaa alitiwa moyo sana na ujasiri ulioonyeshwa na vijana hawa pamoja na maneno ya kizalendo waliyoongea na akawakarisha kwenye uwanja wa mapambano ya M4C.


  Peopleeeeeeeeeeeeees poweeeeeeeeeeeeeeer
   
 2. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Vema wasije tu wakawa wametumwa watajuta kuifahamu!
   
 3. Pangaea

  Pangaea JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 14, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hiyo bab kubwa. Karibuni vijana tuikomboe nchi yetu.
   
 4. i

  ibange JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Safi sanaaaaaaaaaa. Kweli hayo ni maneno ya ukombozi nimeyapenda sana
   
 5. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hongera zao! Lakini wasira anahuyunika kwa vile watoto wamemjeuka na kuwa mrengo wa kati kulia
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Karibuni vijana.
   
 7. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Kweli Watoto wa siku hizi, nakulipia Ada yote una soma mwisho unanifanyia hivi, nitaanza upelelezi wangu kujua kwa nini wasira anakosana na Watoto wake, katika research yangu kwenye Eneo la research hypothesis naweka muktadha wa wasira kuwa na mwnamke mwingine aliyekuwa mke wa marehemu ndege na hivyo pesa zote za familia kueleka huko hivyo Watoto hawana kitu home, hii ni hypothesis tu subiri utafiti.


  phd .
   
 8. Kocha

  Kocha JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 2, 2008
  Messages: 375
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Safi sana hizi ni habari zenye kuleta matumaini
   
 9. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Hao ma-spy wetu na tunashukuru kwa chadema kuwapokea.
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,827
  Trophy Points: 280
  Habari njema sana . Ndio ccmweli wajue sasa nguvu ya cdm!
  *******************
  Cdm haitafikisha mwaka-wassira
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,827
  Trophy Points: 280
  Hakika nilijua lazima mseme hivi, sasa kama mmewatuma si umesha toboa siri!
  Uzuri cdm hatukai na nyoka ndani kama watabainika watapata haki yao kama wengine!

   
 12. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kweli!!! Nina mashaka!!! Wakae tu pembeni kama wanachama ili mienendo yao ichunguzwe!! wasiingie sebuleni kwanza!! Wakae barazani ili wafahamike motive yao!!! Karibuni sana makamanda!!
   
 13. P

  Pumb JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 296
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Du ila wanauvumilivu! Wataweza kweli kuhimili mikikimikiki ya matusi ya vijana wa chadema dhidi ya baba yao wasira...tyson...mzee wa gombe!
   
 14. Miaghay

  Miaghay JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Infitlation...
  Inftralatio...
  Inftrate.
  I just cant spell this word.
  INFTRATE AND DISTABLISE
   
 15. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #15
  Sep 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Baada ya kamanda Makongoro Wasira kujiunga na M4C siku chache zilizopita, leo tena watoto wengine wa Wasira wamejiunga na M4C na kukitupia virago Chama cha Baba yao CCM. Waliojiunga leo katika Makao makuu ya Chadema na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa ni kamanda Ester Wasira na Lilian Wasira.

  Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa kadi walikuwa na haya ya kusema:
  Ester wasira: (Ni mwanasheria, graduate wa UDSM)
  (i)
  Chadema ni Chama cha kizalendo na mkombozi wa dhati wa Mtanzania.
  (ii)
  Chadema kinaleta matumaini mapya kwa Watanzania hasa vijana wasio na kazi na matumaini, Watanzania wenye maisha magumu hata kushindwa kumudu milo miwili kwa siku, akina mama wanaohangaika vijijini bila matibabu ya uhakika, maji, umeme, nyumba bora nk

  (iii)
  CCM imedumaza nchi, nchi imekuwa kama mtu aliyedumaa kwa kukosa protein, haikui tena, Chadema ni damu mpya yenye kuweza kuingiza protein kwenye mishipa ya nchi iweze kufufuka na kukua tena.

  (iv)
  Chadema kina viongozi imara na kwa maneno na matendo yake wanawadhihirishia watanzania kuwa ni waadilifu na wana nia njema ya kuipeleka Tanzania mbele.
  Alimalizia kwa kuwaasa vijana, akina mama na wazee wajiunge na M4C ili kuijenga Tanzania mpya. Alimalizia kwa kusema, “Kwa msaada wa Mungu, Tanzania Mpya inakuja.
  Lilian Wasira (Mwanasheria, graduate wa TUDARCO)( Alielezea furaha yake kwa kujiunga na Chama makini na chenye kuleta matumaini mapya kwa mtanzania(ii)
  Aliwaasa vijana, akina mama na wazee wajiandikishe kwa wingi nafasi itakapotokea na 2015 wakamalizie kazi ya ukombozi kwa kuipigia Chadema kura
  (iii)
  Amewaasa Watanzania kuacha kulalamikia maovu ya CCM na kuchukua hatua ya kuiweka CCM pembeni na kuleta Chadema kama chama mbadala. Alisema hakuna sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama watanzania hawathubutu kuchagua chama mbadala na badala yake kuendelea kuichagua CCM na kulalamika kila siku kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi
  (iv) Kwamba CCM imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 hivyo ni wakati sasa wa kuiweka pembeni na kuingiza chama kipya, mawazo mapya na kujenga mfumo mpya wa uongozi. Hakuna kitu CCM imeshindwa kufanya kwa miaka 50 inaweza kufanya kwa miaka 5 au 10 ijayo
  .
  (v) Anasema ana imani na sera za chadema kuwa ndizo zitatukomboa. Amewapa moyo viongozi wa Chadema wasitishwe na vitisho na mauaji yanayofanywa na dola na kusema yupo tayari kwa M4C na yupo tayari kulipuliwa kama walivyolipuliwa wanachadema wengine na kuuawa kama itambidi afanye hivyo.
  (vi) Kwamba Chadema ni Chama kinachosubiri kuingia Ikulu isipokuwa tu watu wajiandikishe, wapige kura na walinde kura.
  (vii) Nae alimalizia kwa kusema “Kwa msaada wa Mungu Tanzania mpya inakuja.”Dr Slaa alitiwa moyo sana na ujasiri ulioonyeshwa na vijana hawa pamoja na maneno ya kizalendo waliyoongea na akawakarisha kwenye uwanja wa mapambano ya M4C. Peopleeeeeeeeeeeeees poweeeeeeeeeeeeeeer
   
 16. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,665
  Likes Received: 21,888
  Trophy Points: 280
  Wako watoto wengi ambao hawakubaliani na CCM hii ya baba zao au mama zao ila wanakosa ujasiri wa kuwakana kwa vile wanaogopa kukosa utamu wa sukari. Nadhani hawa ni mfano bora na wanastahili kupongezwa na kutiwa moyo.
   
 17. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hapo kuna mawili
  1.Hawana uhusiano mzuri na baba yao mzee tyson so wameamua kumkomoa kwa kujiunga na vyama pinzani
  2.publicity stunt.
  Nitakuwa wa mwisho kuamini kama kujiunga na Cdm ni kwa nia ya dhati
   
 18. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Kama CDM walivyomuweka NAPE Huko CCM
   
 19. rushanju

  rushanju JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 2,342
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  NINAANGALIA TV MLIMANI SASA HIVI NAONA WATOTO WA MZEE WASSIRA ANAPOKEA KADI TOKA KWA MZEE SLAA NA WATOTO HAWA WOTE NI WANASHERIA. WAMEKADHIWA KADI NA KATIBA YA CHADEMA KTK OFISI ZA CDM. IKUMBUKWE MTOTO MWINGINE ALIJIUNGA NA CDM MAJUZI TU HUKO MAJUU.

  source mlimani tv saa moja na nusu taarifa ya habari
   
 20. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Kwa hili naweza kumsifu wasira kwani hakuwaendekeza watoto wake na siasa kama tunavyoona watoto wa vigogo wengine wa CCM ambao wameanza kuwajenga watoto wao na siasa za CCM tangu wakiwa shule za Sekondari hadi vyuoni na matokeo yake tunayaona wengi wamekimbilia kutafuta uongozi ndani ya CCM huku wakiwa na elimu zao ambazo wanashindwa kuzitumia katika ujenzi wa taifa hili na kuendekeza siasa ili wawe kama baba zao
   
Loading...