Dr Slaa atingisha Kigoma Kaskazini

Dr Slaa atingisha Kigoma Kaskazini

Slaa aliambiwa na Wanakigoma, kuwa hali haijatulia, asiende, akataka kushindana Ubavu na Zitto kwa kumuonesha kwamba yeye yuko Juu, sasa ona anaibika anahutubia upepo!. HUYU MZEE HAAMBILIKI, HAFAI HATA KIDOGO!


Hao watu kiduchu bora angewatumia ujumbe kwa SMS kuliko kufunga safari ndefu kuongea na watu wawili na robo...
 
Mungu anasema mkusanyikapo watu nami nitakuwepo.haijalishi wangapi wamefika ila hata wewe kusikia kilichoendelea, tunasema umefana.kufuatiloa kwa ccyenu kunatuonesha kuwa dr slaa ni muhimu xana.
 
Slaa alisema nchi hii haitatawalika tena, lakini sasa anachekelea ulinzi wa FFU kwa hisani ya serikali ya CCM.


Acha upotoshaji mjinga wee.......polisi wapo kwa ajili ya raia na mali zao ni hali ya kisiasa ndiyo inayumbisha na wao kujikuta wanaitumikia viongozi wao hawa mafisadi bila kujijua.

Na wote tupo chini ya sheria mjinga wee!
 
Daa slaa uwashukura police ccm ndio wamekuokoa sasa sijui watakua police cdm aaaahaaaa

Mlisema asikanyage Kigoma,hiyo aliyofika na kuizungukia kwa takribani siku nne ni wapu?Burundi au,na hata hivyo hamjui kwamba hamjui,hapo ndo tunachukua ushahidi wa kumfukuzilia kwa mbali huyo ZZK,na inavyoonekana yy ndo ana- think short,kama CCM wanamuona anafaaa,kuna haja gani kula njama za kuvuruga mikutano ya Dr Slaa,hizo fedha mnazo-invest ni bora mngemlipa per day Zitto ili azunguke nchi nzima na mmnadi kuwa sasa ni mwanachama wa CCM,na mmpe uenyekiti wa taifa.
 
Msafara wa Gwiji wa siasa Tanzania na Katibu mkuu CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa ndo unakatiza hapa Kigoma mjini, ishara ya vidole viwili inatanda kila mahali na maneno ya ''Dkt. Slaa huyo huyo...Chademaaaa....Chademaaaa''.

Msafara unaelekea Jimbo la Kigoma Kaskazini Mkutano wa Kwanza utakuwa Nyarubanga, kisha utaelekea mkutano wa pili.


Updates.....

Ndo twawasili Nyarubanga hapa. Akina mama wamejipanga barabarani pembeni kdg ya uwanja wanaimba kumpokea Katibu Mkuu Dkt. Slaa. Msafara umeshaingia uwanjani.

Red Brigade wako imara kweli kweli leo hapa. Wananchi wanasogea sogea. Naona ngoma hapa inachezwa na akina mama.

Updates No 2:

Dkt. Slaa anaingia kucheza ngoma na wenyeji hapa. Ngoma hii inachezwa na kikundi cha ngoma cha akina mama wa CHADEMA kuhamasisha wananchi kujiunga na CHADEMA hasa akina mama na vijana.

Naambiwa inaitwa Denga. Wananchi wanashangilia kumuona Dokta anaungana na akina mama kucheza Denga!

Updates No 3.....

Mkutano umeshafunguliwa na Mkiti Issa Kibaba. Waitara amemkaribisha Mratibu wa Kanda ambaye amezungumzia namna Kanda inavyojipanga kuhudumia wanachama na wananchi kwa ujumla.

Sasa anapanda Mkiti wa Kanda Shaaban Mambo, anazungumza kidogo kwa sbb ya dalili ya mvua kubwa. Sasa amepanda Dkt. Slaa.

Mvua imekuwa kubwa hapa. Wav wamevumilia kumsikiliza Dkt, ambaye ameamua kubadili kubadili mbinu ya mkutano badala ya kuendelea kuhutubia, anatoa nafasi ya maswali kwa wananchi ili wasiende mbali

Updates No 4.....

Watu 4 hadi sasa wameshauliza maswali na Dkt. Slaa anaendelea kujibu maswali yote 5, 3 yanayuhusu maamuzi ya Kamati Kuu kuwavua madaraka Zitto, Kitila na Mwigamba

Mengine 2 yanayuhusu Chadema na misingi yake. Dkt, anaendelea kufafanua, masuala yote yaliyoulizwa.

Mvua inazidi kuwa kubwa hapa. Dkt. Slaa anawauliza wananchi aendelee au afunge mkutano, wananchi wanasema aendelee. Anaendelea hapa.

Mvua kubwa iliyotanguliwa na ukungu mkubwa sana ktk eneo la mkutano imezidi kuongezeka.

Sehemu ya umati wa wananchi wametafuta miamvuli na kubaki karibu na jukwaa. Wengine wako jukwaa kuu, wengine wamekimbilia upenuni mwa nyumba kuendelea kusikiliza.

Mvua ktk eneo hili la mkutano ni kubwa sana, ingawa mbali kdg tu kutoka hapa hakuna ukungu wala mvua.

Updates No 5....

Kutokana na mvua kuzidi kuwa kubwa Wananchi wamemruhusu Dkt. Slaa ashuke jukwaani baada ya kuhutubia kama dkk 45.

Msafara unalazimika kuondoka kwenda mkutano wa pili.

Kuna utani unazungumzwa na baadhi ya wananchi kwamba ''wameshindwa njia zote sasa wameamua kujaribu hii...''.

Lakini Dkt. Slaa kabla hajaondoka jukwaani, aliwaambia wananchi kuwa mvua ni baraka, hivyo wasilaumu!

Picha chini ni kabla mvua haijaanza kunyesha:
attachment.php



Source: Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene

IT DEPARTMENT yenu nambiwa ipo busy kuliko vipindi vyote ku-edit picha za zamani na ku-launch, ndo maana wanahakikisha mpaka sehemu ya DATE TAKEN wanabadili ili kuhakikisha uongo wa zamani hauonekani
 
Hako kadogo ka mzoga wetu, sidhani kama jana kalienda hata choo au kula maana kaliza kweli au ndio mtumishi mwema kazini.....mkuu Mungi mwambieni huyo dogo waliwahi kuwepo akina Chama siku hizi aweza kaa hata wiki asionekane humu

mkuu huyo binti Msoga yetu ana bidii sana huwa hatoki. Ila mchana leo tulimmiss labda alienda kubadilisha always ultra
 
Mpiga picha ni mwongo wa mchana..ukiangalia picha ya pili hapo juu yenye kamba, watu ni wengi sana,ila aliepiga picha kakata robo tatu ya watu..angalia mwisho wa kamba haionekan kushoto,ardhi haionekan,badala yake inaonesha watu wamekatwa....usitudanganye ndg.
Pili, mlileta habar hapa jion kuwa docta katimuliwa kwa mawe,et kashindwa kufanya mktn,sasa kama alikimbia,iweje tena aonekane yupo kwenye mktn? Mbn watu wametulia pamoja na mvua zilizokuwa zikinyesha??? Sisi si watoto mkawadanganye maccm.....
 
Picha zimepigwa kimtego,yaani mpigaji amejidanganya kwa kupiga kiupande upande ili tu kutimiza adhma yake...Bado Dr.Slaa ni mtu jasiri sana,mwanasiasa imara asiyeterereka!!!Hongera Sanaaaaa!!!
 
Slaa analindwa na askari saba ili afanye siasa kwa usalama, lakini analalamika na kusema kuwa mfumo wa siasa Tanzania ni sawa na ule wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini. Halafu anajifananisha na Mandela!

Mkuu hivi Dr Slaa amefika Kigoma na kufanya mkutano???!!!!
 
Nyie Mwaka huu mtaukalia tu. Mbinu za kishetani zimeshindwa toka juzi bodaboda hapa kigoma wanakula kodi yao kutoka kwa Mafisadi CCm buku 10 zinahusika

Pole sana Mkuu naona umeumizwa na huu ukweli!!lakini hakuna ujanja wa kukwepa hali halisi ndio hiyo,Tumaini MAKENE anawapa ahueni tu kwa picha za kuungaunga
 
Back
Top Bottom