Dr Slaa atingisha Kigoma Kaskazini


DR SLaa...kweli ni tishio halisi kwa CCM!!! Mzee huyu utadhani anamiaka 18!! Mungu mlinde President wetu huyu!
 
itabidi makamanda tubadili mbinu za vita hii sio vita ya damu na nyama tena maana uko wameshindwa sasa ni vita katika ulimwengu wa roho juu ya wakuu wa giza juu ya wachawi,waganga,prof.maji malefu na wengine wengi
 
Kila la heri dr. Slaa, tunaombeni endeleeni kutupa updates za kutosha wakuu!
 
Well done Chadema. Vita na vikwazo ni vingi lakini hatimaye sisi wote Watanzania tutashinda. Magazeti yaliyo mengi kama vile MWANAINCHI,HABARI LEO na mengineyo, yote yako kinyume na harakati halali za Ukombozi dhidi ya UDHALIMU na UKANDAMIZAJI wa serikali ya CCM.
Vilevile vituo vya Televisheni haswa pia ITV sio rafiki wa kuzungumzia UKWELI kuhusu mikutano na matukio ya kisiasa ya Chadema haswa juu ya mikutano inayofanywa na Dr Slaa kule Kigoma.
Wote hao hawaoni uchungu wa UDHALILISHWAJI wa WANAINCHI unaofanywa na UFISADI wa CCM na serikali yake.

CHADEMA tusichoke kuwatetea Maskini na Wanyonge wa Nchi hii,na kuwapigania katika yale yote wanayoyaamini katika ustawi wa Maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.

VIVA Dr.SLAA;VIVA CHADEMA:
 
Si bora yeye kuliko yule aliyejaladia hadi ulinzi wa majini kwenye kampeni za urais 2010? Nimekumbuka jinsi Kiongozi wa Brigedia ya ulinzi wa Majini alivyotishia hadi wagombea urais wengine kuwa atakayempinga JK atakufa ghafla......

Nilicheka sana kipindi kile nikasema kama presidaaa anaamini majini na ushirikina je wananchi ambao hatujaenda shule
 
wakuu kuna mtu ana habari alipo TUNTEMEKE?nataka aje aniambie mwaka hiyo picha ilipopigwa na wapi
 
Last edited by a moderator:
John Mrema, vipi kile kikao cha jana kilichoazimia kumdhuru kimwili Alex Kitumo? Kidahwe si mmekimbia baada ya mkutano kushindikana, ndio mmeamua kupika hizi picha? Pole sana. Hamna haja ya kuhangaika kuonyesha mafanikio ya ziara ya Dk Slaa Kigoma. We know Kigoma. Nyie mvueni uanachama Zitto ili uchaguzi mwingine uitishwe ili tuone nani mjanja.
 
Hakuna kurudi nyuma. Huu ni ujumbe tosha kwa mahasimu wa haki na maendeleo ya Watanzania
Hii nchi ni ya Watanzania na Watanzania wenyewe ndio sisi tulioamua kusimama nyuma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Bravo Dr Slaa
 
Reactions: MC
Tumeanza kuchanganyikiwa. Yaani badala ya kupambana na akina Kinana tupo busy kupambana na Zitto. Ni nani huyo aliyeturoga? Yaani Zitto amekuwa taasisi?
 
Hakuna kurudi nyuma. Huu ni ujumbe tosha kwa mahasimu wa haki na maendeleo ya Watanzania
Hii nchi ni ya Watanzania na Watanzania wenyewe ndio sisi tulioamua kusimama nyuma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Bravo Dr Slaa

Kwa hiyo sasa hivi mpinzani wetu ni Zitto na sio CCM tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…