Dr.Slaa ashinda kesi ya uchaguzi!

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,575
Kwa mujibu wa makahama kuu kanda ya Arusha iliyoketi kwenye kesi ndefu zaidi ya uchaguzi kuliko zote kuwahi kufanyika kwenye historia ya taifa hili la Tanzania ni kuwa Jaji Makaramba ametoa hukumu muda mfupi uliopita na kuwa Dr. Slaa ameshinda kesi hiyo.

Hukumu hiyo inasema kuwa Slaa ameshinda .

Kwa sasa wapambe wa CCM waliokuwa wamekuja jijini Arusha kwa magari aina ya FUSO ili kuja kushangilia hawaonekani na mafuso yao pia hayyajulikani yalikoelekea.

Nitawapa taarifa zaidi.
 
Hukumu hiyo ilisomwa kwa muda wa masaa manne na ameswhinda kwenye vipengele vyote vya kesi hiyo.

Hapa Arusha ni vifijo na nderemo japo wananchi wanataka kuandamana ili kufikisha ujumbe ila Dr sLAA NA lISSU pamoja na viongozi wengine wanajitahidi kuwatuliza ili wasiweze kupigwa na polisi.
 
Kwa hio mheshimiwa Dr Slaa sasa ana goli 1-0.

Kurudisha goli moja si mchezo kama walioshinda wanacheza "10 men behind the ball"

Natamani kuona "independent opinion polls" (sio za REDET) zinafanywa kuanzia sasa kuelekea 2010.
 
Unganisha hii na ile nyingine ya 'Hatima ya Slaa kujulikana kesho'
Hongera Dr. Slaa
 
Kuna shangwe sana hapa pamoja na nderemo kwani wananchi wanashangilia sana sana na redio zote za hapa zinarusha tukio hili pamoja na vijana wengine ambao wamekodi gari na vipaza sauti wanapita mtaani kutangaza tukio hilo ambalo limepokelewa kama mlipuko mkubwa wa shangwe na nderemo ,hoihoi na vifijo.
 
Aibu nyingi sana za namna hii zinawajia CCM, ujanja ujanja wao umeanza kukosa nafasi sasa

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Dr. Slaa,Mwanasheria Lissu,Chadema, Wanajimbo la Karatu na Wapenda haki wote nchini Tanzania. Hongereni sana.
 
Mambo yametulia na shagwe zinaendelea kwa nguvu sana hapa .

Kuna mambo mengi sana yanaendelea ila wengine wanalia kwa furaha na wengine ndio hivyo wanahuzunika kwani walitaka kushinda , japo hizo ndio pande mbili za maisha ya binadamu.
 
Hii habari ni nzuri sana kwa wapenda mageuzi wote. Dr Slaa ni mtu jasiri asieyumbishwa na lolote. Pia Tundu Lissu ni shujaa asieogopa mapambano na dola wala mtu yeyote. I am proud to have this people in this Country. Yaani tungekuwa na akina Slaa na Tundu 200 lazima nchi ingebadilika!!!
 
Hongeraaa Dr Slaa...najua Watakata Rufaa......ila Always Truth Will Prevail
 
Mpaka Kielewe..... Asante sana kwa habari hii..... Hongera Dk Slaa kwa unshindi huu sababu ni chachu kubwa sana kwa wote wanaopenda maendeleo ya nchi yetu!!!

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake...............
 
naenda supermarket kuchagua whisky je ninunue techers au VAT 69...nishaurini jamani kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwiiiii
 
Back
Top Bottom