Wana Ukumbi,
Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa, yupo ziarani nchini Marekani akiwa ameambatana na mke wake, bibi Josephine.
Katika ziara hiyo, pamoja na mambo mengine, Dr Slaa amewasilisha mada mbalimbali zikiwemo zenye kuhusu katiba mpya, haki za binadamu nk
Kama ilivyo ada katika mijadala ya namna hii, baada ya mgeni rasmi kumaliza kuhutubia, nafasi utolewa kwa wageni wengine pia kutoa maneno mawili matatu, na hapo ndipo alipoibuka Josephine!
Josephine, ambae anatarajiwa kuwa "the next first lady" baada ya mama Salma Kikwete, ameboronga kabisa kwenye kuzungumza lugha ya kingereza (kutema yai) na badala yake ameishia kujiaibisha mbele ya Wamarekani!
Katika maneno yake amekaririwa akisema "the woman is a source of wealth for man in our lifes", kitu ambacho Wamarekani hawakuelewa alitaka kumaanisha nini. Vilevile, Josephine alishindwa hata kutoa 'a simple good evening' wakati wa dinner party badala yake alisikika akisema " me good, me good" wakati wa salamu!
USHAURI KWA CHADEMA: kama kweli mpo makini katika kuitaka Ikulu, hakikisheni mnaandaa mazingira yote yawe sawa. Ikiwemo hata kumuandaa our next first lady! Nasema hivyo kwa kuwa hata Bukhali wa Nigeria aliandaliwa yeye sambamba na mke wake.