sexologist
JF-Expert Member
- Dec 5, 2010
- 2,283
- 976
Hongera John Mnyika.. Sasa ni mapambano na mafisadi kwa kwenda mbele.. Anza na hiki kifisadi mtoto cha siri siri kinaitwa Nape Nauye..
Hao uliowataja wamekuambia wanaiweza hiyo nafasi? Je wamekumbia hawana majukumu kiasi hawatatingwa kama wangeteuliwa kwenye hiyo nafasi?
Hatimaye katibu mkuu wa chadema dr slaa amemteua rasmi mbunge wa jimbo la ubungo JOHN MNYIKA kuwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa CHADEMA taifa na kumshusha ndg ERASTO TUMBO KUWA afisa ndani ya kurugenzi source TBC TAARIFA
Kumbe ulikuwa unakuja huku, mwanzo umepongeza uteuzi wa Mnyika sasa unaponda aliyemteua can you declare your interest.Wee waulize hawa hawa kama wananjua Robert Gibbs ktk siasa za Marekani..wachache sana wanamjua, wengine utaona wanakimbilia Google kwa sababu tumezoea siasa za kujuana...
I'm Sorry Dr.Slaa nadhani ktk hili kachemsha maana uwezo pekee hauwezi kuwa kigezo bali nafasi muda na kuelewa vyanzo vipi unatakiwa wakati muafaka na sii kusubiri vitu vimekwisha tokea kama zilivyo siasa za Bongo. Unaanda mikakati mbele ya safari na inahitaji muda mkubwa sana na ujuzi wa kazi hiyo jambo ambalo vyama vyetu vina mapungufu sehemu zote hizi.
Anashindwa kuwa available wapi.Japokuwa watu wengi wanaweza wasielewe unachokisema Mkandara kwa ajili ya mapenzi waliyonayo juu ya Mnyika lakini ni jambo muhimu sana ambalo lilitakiwa kutafakariwa kwa undani na Chadema kabla ya kufanya uteuzi.
Mnyika mara kadhaa anasema kwamba yuko busy anashindwa kuwa available, kwa maana hiyo kumuongezea majukumu mimi naona ni kumpunguzia ufanisi.
Kila la kheri Mnyika kwenye majukumu yako mapya
Kwa nini naitwa mimi mbishi ikiwa nilichokiona nyie hamkukiona?.. hatuzungumzii kitu kimoja hapa. Mbishi ni yule anayekataa kwamba Mnyika hana uwezo na ha qualify bali nachosema Vyeo hivi vinawabana viongozi ktk utendaji kazi wao kiasi kwamba watakuja shindwa jambo muwaone wao wabovu kumbe sisi wenyewe ndio tumekosea...Nini hizi kofia 10 maana mbili pekee mmeona hazitoshi? hawa ni miungu watu wana nguvu za ajabu?Mukandara acha ubishi Kijana,Wewe ni mtoto wa yule mzee wa udsm nini?Mbona mbishi sana.Maana yule mzee kashindwa kazi sasa ni kufukuza tu watoto wa masikini,eti wanaendekeza siasa wanapodai haki!!!
Mada sasa:Unafahamu Marketing "strategic plan",especially katika Siasa?Hawa watu wa hapa JF nani anawajua zaidi yako?Bavicha hapa Kijijini anajulikana Heche Peke yake maana kila siku wanamuona Star TV.Sasa kazi ya Uenezi unaona kama nyepesi ya kupewa tu mtu sio?Poor marketing plan hiyo.PSG wanapotaka kumsajili Beckham sio kwamba sasa anamzidi Ronaldo au Rooney,au Ile timu ya Uchina sio inamtaka Drogba na imemchukua Anelka kwa sababu wataibebesha ubingwa la hasha,Anzhi Makachakala ilipomchukua Etoo ilikuwa na ajenda nyuma sio ubingwa.Ni kweli Mnyika majukumu mengi sana,lakini kwa faida ya chama,ni lazima awe yeye TU for the time being.Hivi huyo tumbo zaidi ya Igunga,huku kwetu swekeni unafikiri nani anamjua?Hata mijini kwenyewe nani anamjua?Hapa Chadema imelenga kuwashika masikio Wananchi wengi,lakini hizo kazi si anaweza kuwa na wasaidizi lukuki ili kumrahisishia majukumu,kama alivyokuwa na yeye anakaimu nafasi ya Dr.wakati wa kampeni.Hapana,kwa hili una lako jambo,Dr.Slaa hajawahi kukosea uteuzi baba,Mnyika ni sahihi kabisa kwa sasa,otherwise Hueleweki Bro.Nafasi nyingine huhitaji zaidi "Celebrities" ili ku-capture MARKET hasa Vijijini,maana ndiko Mnyika anajulikana kuliko sisi wa mjini tunaoshinda hapa JF,you know kuna watu hapahapa mjini tena wanafunzi wa vyuo vikuu hawajui JF ambako unawataja Kina Lunyungu et al.Hawa kina Lunyungu Kama uteuzi wa Uenezi hapa JF,kama wasipoteuliwa wao hapo tutaandamana na kusema kweli kuna upendeleo.Nakumbuka Lema alipokuwa anazindua Tawi la Chadema Pale Chuo Cha Uhasibu Njiro,alituambia kwamba,Sisi tunaojiita wasomi kazi yetu kubwa ni kueneza chama kupitia Mitandao,kazi nzuri sana inafanywa na hao uliowataja Mukandara.Na ndio sehemu yetu sahihi kabisa.
Kwa kuzingatia majukumu mengine alokuwa nayo Mnyika na sii vinginevyo!...Nilijua tu mawazo yenu yameganda sana ktk mitandao. Nina hakika kabisa ndivyo wengi hapa wanafikiria hivyo lakini amini maneno yangu nampenda sana Mnyika japokuwa sikufurahia sana kutokuwepo hapa JF baada ya kuwa mbunge na yeye akanambia ametingwa sana na majukumu.Kumbe ulikuwa unakuja huku, mwanzo umepongeza uteuzi wa Mnyika sasa unaponda aliyemteua can you declare your interest.
Tatizo lako unafananisha cheo cha katibu mwenezi na press secretary au mkurugenzi wa mawasiliano ikulu kama Soby anavyodhani, katibu mwenezi si mtu wa kumjibia Mbowe emails zake au tweets za Katibu mkuu is a political position, is a lobbying post ni zaidi ya press secretary, Salva haandiki speech na kuipeleka jukwaani anampa mwanasiasa akaisome aisome vipi ni juu ya mwanasiasa si juu ya Salva au secretary wa Obama. Tofauti yake na post ya Mnyika, Mnyika anatakiwa aandae speech yake halafu akaiuze mwenyewe kwenye majukwaa uenezi ni zaidi ya kutweet ndugu yangu.Hapana mkuu wangu wewe nadhani ndio unapotoka maana hata Rais anapotoa hotuba huandikwa na watu ambao hawapo ktk siasa. Press Scretary wa Obama au Romney, Ron Paul na wengineo hawa sii wanasiasa kwa jinsi unavyowafikiria bali hawa ni watu wanajua mbinu za kupanga vitu kisomi na utaalam maana kiongozi wake tayari anazo nyenzo za kisiasa..
Mnyika ni mwanaSiasa, mbunge mwenyekiti sijui waziri kivuli hivyo ni vigumu sana yeye kuweza kuwa na muda wa kuyafanya yote haya. Mathlan, Hivi Salva ni mwanasiasa kwa mtazamo wako au mapungufu yake yanatokana na kutokuwa mwanasiasa?...Sio lazima Mnyika ndiye awe anajibu kama alivyosema Soby bali kuandaa shughuli za chama iwe mahojiano, makutano na kadhalika. Na kwa mfano unapo chat na Obama Tweet au JK haina maana huyo ni Obama au JK mwenyewe bali ni imetokana na maadalizi yamefanya ktk idara yake ya mawasiliano..
Sina uhakika Mnyika atakuwa na muda huo wa kushinda makao makuu akiweka mikakati ya chama wakati ana majukumu Ubungo, bungeni sijui uwaziri kivuli wakati wapo watu Chadema wamesoma na hata kama hawaelewi somo hili, wataiweka kazi kama wataelekezwa vizuri kwani huyo Mnyika katokea wapi jamani?
Mkuu huku majuu maadam una elimu tosha, ari na uwezo unao kinachotakiwa ni maelekezo ambayo msomi anaweza chukua nyaraka akazisoma nyumbani kujua kazi zake. Wewe unaweza na wengine wote nilowataja wanaweza hata huyo Tumbo anayedharauliwa naweza ndio maana kachaguliwa nafasi nyingine.
Again why tunakazania hili? Mnyika kisha chaguliwa haina neno lakini nasema hivi mna mzeesha dogo mapema kwa kumpa majukumu makubwa wakati muda wenyewe hana.....Ni ushauri tu.
Kazi ya Mnyika si kupambana na Nape ni kujenga chama.Hongera John Mnyika.. Sasa ni mapambano na mafisadi kwa kwenda mbele.. Anza na hiki kifisadi mtoto cha siri siri kinaitwa Nape Nauye..
Mkuu siasa za bongo ndiyo zinatumaliza...Simply wewe huzijui siasa za bongo mwisho utasema anaweza akatuma hata mkanda wa video hata tape recoder kwenye mikutano na yeye asiende.
No sir,Tatizo lako unafananisha cheo cha katibu mwenezi na press secretary au mkurugenzi wa mawasiliano ikulu kama Soby anavyodhani, katibu mwenezi si mtu wa kumjibia Mbowe emails zake au tweets za Katibu mkuu is a political position, is a lobbying post ni zaidi ya press secretary, Salva haandiki speech na kuipeleka jukwaani anampa mwanasiasa akaisome aisome vipi ni juu ya mwanasiasa si juu ya Salva au secretary wa Obama. Tofauti yake na post ya Mnyika, Mnyika anatakiwa aandae speech yake halafu akaiuze mwenyewe kwenye majukwaa uenezi ni zaidi ya kutweet ndugu yangu.
Anyway kama ulivyosema Mnyika ameshachaguliwa binafsi nina imani naye tena sana, ila jaribu kuwa gentleman uwe na positive thinking kwa vijana badala ya kusema wana mzeesha dogo sema wana mkomaza.
Nakubaliana na Mkandara,tumepigia sana kelele mambo ya kurundikiana vyeo alafu tunafanya yale yale! Mnyika ni Mbunge,ni waziri kivuli sasa mwenezi! Kweli kuna ufanisi hapa! Uwezo anao ndio lakini mbona CDM ina vichwa kibao? Tukubali kujikosoa!sasa napendekeza cdm ianze mchakato wa kumtafuta mrithi wa mnyika ubungo kwani kazi za ubunge zinamshinda. Anafaa za kitaifa zaidi