Dr. Slaa amteua Mnyika kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Chadema sasa mnachosha.... kwa nini mnawalimbikiza wabunge kazi zaidi wakati walizonazo tayari ni mzigo kwa chama?.. Vijana wengine wapo kwa nini hawatumiwi hawa!..Sipingi swala la Mnyika kuteuliwa nafasi hii, bali nadhani wapo vijana wengi sana wenye uwezo ari na wamejikita ktk media wanaweza kuifanya kazi hii kila siku masaa 16 kwa malipo madogo sana kuliko kumshindilia mtu mmoja majukumu kibao.. Mtamzeesha huyu dogo kabla ya wakati wake.

Swali langu ktk uteuzi huu, Je, Hawa viongozi wa chama na ni wabunge pia hawapokei mishahara miwili kwa kutoa huduma hizi?.. mathlan Mnyika leo hii pato lake haliongezeki kwa kupewa jukumu hili zaidi maana twende mbele turudi nyuma. Kupinga posho pekee haitoshi ikiwa chama kinawapa madaraka kundi la watu wale wale tu hii inaashiria zaidi kwetu kama ni ULAJI zaidi kwao..
- Mtanisamehe nawakilisha mawazzo yangu.

Mi nadhani hiyo post inahitaji mtu anaejulikana na mwenye mvuto kwa wengi kutakana na umaarufu wake................
Usiwe na wasi wasi hata Mnyika amepiutia huko huko asingeweza kuwa katibu mwenezi mara tu alipo maliza shule....

Unajua CDM hawalazimishi mambo, wanaenda kwa mtiririko makini mno! Siyo kama CCM wliolazimisha KIAZI kabisa kuongoza nchi!
 
Hatimaye katibu mkuu wa chadema dr slaa amemteua rasmi mbunge wa jimbo la ubungo JOHN MNYIKA kuwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa CHADEMA taifa na kumshusha ndg ERASTO TUMBO KUWA afisa ndani ya kurugenzi source TBC TAARIFA
Kwanini Mnyika? inamaana CDM hamna watu wengine wanaofaa kuchukua hiyo nafasi? Vyeo vyote kwanini wanajilimbikizia wenyewe?
 
Kwanini Mnyika? inamaana CDM hamna watu wengine wanaofaa kuchukua hiyo nafasi? Vyeo vyote kwanini wanajilimbikizia wenyewe?

Mkuu Rejao,
Siku zote nimekuwa nikikusoma ukimsifu Mnyika kama kiongozi makini.Vipi Leo tena?
 
Malalamiko yamekuwa yakirushwa humu kuhusu utendaji wa hii kurugenzi ya mawasiliano hivyo pengine mnyika anaweza kuipaisha kufikia viwango tunavyotarajia. Lakini, ile kurugenzi ya mambo ya nje itaongozwa na nani? Au Mnyika ataongoza kurugenzi mbili?
 
Mnyika ni:
-Mbunge wa Ubungo.
-Waziri kivuli wa nini sijui...
-Diwani wa Manispaa ya Kinondoni na Jiji.
-Mkurugenzi wa ki-Foundation chake.
-Baba wa familia bila shaka?
Kama kweli ameamua kuwatumikia WATU hatoweza. Mnataka aonekane hafai. Ajabu na yeye anayakubali yote haya!
 
Namkubali Mnyika ni kijana mwenye uwezo mkubwa sana kwa hakika pengo la Dr Slaa mjengoni limezibwa na huyu kijana ingawa nilitegemea Lisu angeliziba.

Kwakuwa Mnyika ni jembe basi tumrundikie kazi !.Hapana hii kazi ya uenezi atafutwe kijana mwengine mwenye uwezo kama Mnyika nina hakika wapo vijana wengi labda kama kuna ajenda nyingine tusizozifahamu.
 
JJ kama JJ Okocha,kaka unishine hata gizani bado unashine

Tunakutegemea sana katika kuimarisha mawasiliano na kuzifafanua sera za chama hasa kuelekea ngazi za chini za chama,tunakuomba sana ukishakaa vzuri utafute njia bora zaidi ya mawasiliano kwa walioko ngazi za chin mpaka kwenye vitongoji katika kujua CDM ni nini na kinafanya nini kwa ajiri ya wananchi na nchi yetu kwa ujumla..Hongera sana.

Katika kazi,
Ndimi,Rweye.
 
Hapa JF wamejaa tele yaani siwezi hata kuwamaliza... na wameonyesha uwezo mkubwa sana ktk kukitetea chama. Na tuache siasa za makundi wapo kina Ben, Lwakatale, Feedback, Sikonge, Lunyungu, Mwita Maranya na wengine watu wazima wapo ktk media kila kukicha...

mkandara
sidhani kama dr slaa atakuwa amefanya badiliko moja tu la kurugenzi ya mambo ya habari, naimani kabisa itakuwa reshuffle na hiyo mambo ya nje kutakuwa na mtu mwingine...

tukubali 2015 ni mwaka muhimu sana kwa chadema
hao vijana uliowataja wanaweza wakawa wazuri kupita mnyika au wabaya kupita mnyika, kutokana na umuhimu wa 2015 sidhani kama chadema wako tiyari kufanya majaribio na hao vijana, washafanya majaribio na erasto tumbo na hata erasto tumbo akiwa hapa JF anajibu maswali vizuri tu. sasa hivi sio wakati wa majaribio, mnyika ni uhakika.

Mnyika- he is presentable, organised, young, he is got the brain,speaks clearly and precisely, and the media likes him which is very important. why try somebody else while you have got somebody that fits the bill?

MKANDARA HAO VIJANA WENGINE ULIOWATAJA WAPEWE POSITION ZINGINE KAMA KURUGENZI YA MAMBO YA NJE NK
 
Hapa JF wamejaa tele yaani siwezi hata kuwamaliza... na wameonyesha uwezo mkubwa sana ktk kukitetea chama. Na tuache siasa za makundi wapo kina Ben, Lwakatale, Feedback, Sikonge, Lunyungu, Mwita Maranya na wengine watu wazima wapo ktk media kila kukicha...

hapo kwa Ben nakubaliana na wewe,alikuwa ana fit hapa.ila tatizo lake uyu jamaa inapofika maamuzi ya pamoja ambayo yeye alikuwa na mtazamo tofauti,huwa hajari maamuzi ya wengi.
 
Hatimaye katibu mkuu wa chadema dr slaa amemteua rasmi mbunge wa jimbo la ubungo JOHN MNYIKA kuwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa CHADEMA taifa na kumshusha ndg ERASTO TUMBO KUWA afisa ndani ya kurugenzi source TBC TAARIFA

Looooo!Dr wa ukweli ni msikivu sijapata kuona!Heko Raisi wa moyoni mwa wananchi!
 
Mkuu Rejao,
Siku zote nimekuwa nikikusoma ukimsifu Mnyika kama kiongozi makini.Vipi Leo tena?
Namkubali mnyika, but CDM kama chama kinachokua inabidi kiwape nafasi ya uongozi wanachama wengine ile waendelee kuibua wakina Mnyika wapya! Siamini kama hiyo nafasi ndani ya chadema ni Mnyika peke yake ndiye anayeimudu.
Chadema pia mfumo dume naona umetawala...wawape pia kina mama nafasi kama hizi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom