Oooohooo! Sasa haya maswali ndio ya wafungwa Segelea..nilichosema mimi Chadema ina vijana wengi sana wanaoiweza kazi hiyo sina sababu ya wao wanambie...Na kibaya zaidi nawashangaa sana wana Chadema siku zote siasa zenu ni za makundi tu... Yaani hapa tayari nimekwisha wasoma kwamba mnafikiri mimi niko against Mnyika, siwezi kuwa hivyo maana simjui wala sina makundi isipokuwa ukinambia kwamba Zitto ndio kapewa nitasema hivyo hivyo.Hao uliowataja wamekuambia wanaiweza hiyo nafasi? Je wamekumbia hawana majukumu kiasi hawatatingwa kama wangeteuliwa kwenye hiyo nafasi?
Hawa jamaa zetu ambao leo ni Wabunge wamekosa muda wa kukitumikia chama ipaswavyo baada ya kurundikiwa majukumu wao..Fact hiyo huwezi kuikimbia kwa kuuliza maswali bali kutafakari na kufanya maamuzi yanayokijenga chama.
Nakumbuka nilibahatika kuhudhulia kilkao kimoja cha Friends of Slaa (FoS) wapo vijana wengi pale vichwa safi sana tena wanajua sana kujenga hoja na wenye kutazama nje ya box, wana muda na sifa zote uzitakazo..JF ndio usiseme..Kwa nini vijana kama hawa wasitumiwe kukikuza chama badala yake tunawapa watu hao hao kama vile chama hiki kina wenyewe? - Au unataka nifukuzwe Uanachama mkuu wangu..