Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,178
Reaction score
162,659
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

"Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo," alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


CHANZO: NIPASHE
 
Mkuu, kama umeisoma hii story kwa urefu wake, basi tuwekee story nzima. Nimesoma habari hizi kwenye title ya gazeti la Tanzania Daima, but sijajua undani wa habari yenyewe. Tafadhari tusaidie kwa kutuwekea story nzima ili tujue kwa undani hayo aliyoyasema Slaa.
 
Huwezi kutenganisha HELLEN KIJO BISIMBA na RWANDA na Vile vile huwezi kutenganisha huyu mama na SLAA , kwa hiyo siwezi kushangaa anamkosoa JK
 
Jk anatuabisha tu. Rwanda is just too a small country to argue with. Wote tunaoneka wehu kama wao. what is the difference ?
 
Nadhani Dr. Slaa hapa kakurupuka naye anasema mbona yeye kashindwa kushughulikia mambo yake ya ndani?? Mimi kwa uelewa wangu hii aimzuii kuongelea amani ya east afrika...mimi nadhani si kila kitu tupinge usalama wa east afrika una maana usalama wa tanzania...

J.K alikua sawa tu mtutu ukishindikana haina budi kurudi mezani.

I stand to be corrected

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Sidhani kama kuna haja ya kulumbana juu ya suala hili., kama watanzania yatupasa tuwe na msimamo m1 juu ya jambo hili nalo ni uzalendo.,,kama JK alivyosema kama ushaur wake ni mmbovu uachwe na kinyume chake utekelezwe.....
 
Kwa namna Wanyarwanda walivyoupokea ushauri wa JK bila shaka kuna walakini.Lakini hata kwa logic ya kawaida mfano; Jirani yako anapokushauri ukae chini mzungumze na watu waliowaua wazazi wako,ndugu na jamaa utajisikiaje?
 
Slaa nae asidandie gari kwa Mbele.Aweke mbele uzalendo,pia afahamu kuwa Rais KIkwete hakutamka nje ya guidance ya sera ya mambo ya nje ya nchi yetu kwa kuwa ameiva ki diplomasia,SLaa si mwana DIplomasia,yeye amekuwa addicted na maandamano.Asubiri karata yake 2015,kuongoza nchi si lelemama.Kwa muda huu ajifunze diplomasia na si against each and every step taken by Mr President.Kwa hili nitamchukia.
 
Aliyoyaongea Dr Slaa ndio yalikuwa kichwani mwangu.Namuunga mkono Dr Slaa kwa hili.Tanzania hatuwezi kuingizwa Vitani kwasababu ya matatizo binafsi ya JK na Kagame.
 
Dr.Slaa anaweza kuongea hivyo kwa sasa. Lakini hata Dr. Slaa angekuwa Rais wa nchi,maisha yake binafsi na mipaka ya nchi yake ikitishiwa,angeanza kwanza ku deal na wanaotishia mipaka ndipo angekuja kutatua ya ndani.

Ukiwa unagombana na mkeo/mumeo ndani,ukasikia watu wanataka kuvunja gate wavamie kwako,cha kwanza utaenda kupambana na wanaivunja gate lako ukisha wasambaratisha ndio utarudi ndani kupatana na mkeo/mumeo.
 
Dr. Slaa sio kosa lake. Uwezo wake wa kufikiri umekuwa wa kiwango cha Josephine Mushumbusi.

Anasema Kikwete haongei na wapinzani wakati Slaa ameonekana mara kadhaa Ikulu akinywa juice. Sasa sijui walikuwa wanakunywa juice kimyakimya!!!

CHADEMA-Ikulu-leo.jpg
 
The crux of the matter here ni hii kitu inayoitwa HEKIMA.

mathalani, jirani yako akiwa ana ugomvi na mkewe. ukiambiwa kumshauri, wewe utafanyeje?

1. je, utasimama barabarani na kuanza kutangaza ushauri kwa jirani yako?

AU

2. utamfuata jirani yako nyumbani kwake (au hata kumwita kwako) na kumshauri?
 
Inaonekana Slaa anataka mpaka apangishwe chumba magogoni wakae na Mushumbusi ndio aone kwamba Rais wetu ni mwanasiasa wa kisasa anayeongea na mtu wa itikadi yoyote kwa lengo la kufikia makubaliano ya amani bila shuruti.

Hivi Slaa haoni aibu kusema UONGO at his age?

Uroo wa pesa na madaraka unampeleka kubaya sana Slaa...

Rais-Kikwete-akifanya-mazungumzo-na-viongozi-wa-Chadema.jpg
 
Kinadharia ushauri wa Kikwete unaweza kuonekana kama mzuri lakini haukuwa na action plan au road map ya utekelezaji kushauri bila action plan ni sawa na kuropoka hasa unapomshauri mkuu wa nchi nyingine.

Kama Kikwete ataanzisha vita na Kagame binafsi nitakuwa wa mwisho kwenda vitani, kwa sababu naamini Kikwete hakuwa sahihi kuwaambia Rwanda wakutane na waasi alichotakiwa ni ku-mediate mkutano kwa kuwakutanisha mahasimu na sio kuwaambia wakutane, kwanza wakutane wapi na nani awe mlalamikaji na mlalamikiwa.
 
Hapo Katibu Mkuu anatia aibu kama kweli kasema maneno hayo, hata Zitto recently akichangia kwenye mjadala huu katika twitter aliweza kusema kiukweli kuwa sio FDLR wote walihusika na genocide, wapo waliozaliwa ukimbizini na wapo ambao wakati huo 1994 walikuwa watoto wadogo lakini kwa sasa wanakuwa forced na reality kushika silaha...! Pia sio wote katika FDLR ni FOCA
 
Hata kama ni wewe utajisikia pale unapoambiwa ukae meza mmoja na wauaji wa familia yako? Jamaa yetu angemwita pembeni na kumwambia peke yake na siyo kwenye mkutano wa AU.
 
Inaonekana Slaa anataka mpaka apangishwe chumba magogoni wakae na Mushumbusi ndio aone kwamba Rais wetu ni mwanasiasa wa kisasa anayeongea na mtu wa itikadi yoyote kwa lengo la kufikia makubaliano ya amani bila shuruti.

Hivi Slaa haoni aibu kusema UONGO at his age?

Uroo wa pesa na madaraka unampeleka kubaya sana Slaa...

View attachment 105629

Hivi inaingia akilini kweli kumuona baba yako anayemtukana na kupiga mama yako kila siku nyumbani,Akiwanyanyasa nyinyi watoto wake kwa kila namna kwenda kumuhubiria jirani yake jinsi ya kuishi kwa amani na familia na nyinyi watoto pamoja na mama yenu eti mumuunge mkono?
 
Back
Top Bottom