Dr. Slaa AMKIMBIA Wilson Mukama katika mjadala?

kuna kitu mmesahau wadau kuhusu mijadala ya wazi ya CDM na Mabunduki aka Magamba. Nani anakumbuka mjadala kati ya Wassira na Mbowe! Kama mnakumbuka basi. Dr. kasoma alama za nyakati Mabunduki hawachelewi kupandisha Jazba mjadala wanapokutana na kitu cha ukweli hasa joto la mjadala linapopanda.

sasa kwa mazingira kama yale nani ALISHINDA? si Mbowe alipongezwa na kila mtu humu ndani? Slaa angeenda naamini mkama angeumbuka, tungekuwa tunazungumza mjadala mwingine sio huu
 
Usimshawishi modes kufuta kwa kuwa katajwa Dr. slaa.
kama aliahidi kuhudhuria, ikatangawzwa kuwa kwenye mjadala atakuwepo halafu ikatokea hajahudhuria, taswira yake kwa jamii itaharibika. Kuna ukweli kaukimbia. Viongozi kama hawa hatuwahitaji tz, kwani kama anakimbia media akiwa katibu wa chama, Je akiwa rais si atazifuta kabisa?
This colour is so GAY!!!
 
Inawezekana kabisa alikuwa tayari kuongea na wananchi. Tena ingekuwa fursa nzuri ya kuongea mengi na watanzania wengi kwa wakati mmoja lakini bila shaka alikuja kugundua kwamba it won't work because he was invited to a WRONG place.

angekataa mwaliko na sio kuahirisha mwaliko pasipo na taarifa kwa uma. au yawezekana alitoa, lakini TBCCM wakabana taarifa hiyo ila wakaona warushe ya kukacha
 
kama haridhiki na waongozaji si angeweka masharti? na sisi tunaompenda, wenye uwezo wa kufikiri, si tungejua kabaniwa kutoa aliyonayo? si baadae tungeanzisha mjadala kuwalaani TBC?

UKIPENDA KITU Padre, kisikunyime nafasi ya kutafakari. kosa lingine hilo

Sasa kama unagundua mapema kwamba mambo hayatakwenda sawa kwa nini uende halafu uje kulaani baadae??
Huku ni kufikiri kwa masaburi.
 
Inteligensia ya cdm imefanya kazi nzuri. mukama ni gamba sawa na tbc1. wote ni magamba, then what should you expect???
Hakuna intelijensia wala nini CDM wameishiwa. Ingekuwa Mukama kaingia mitini ungechoka kusoma mipasho ya wanaCDM.
 
nakuunga mkono lakini kwenye nyekundu sijakuelewa....

Wengi kuhusu hili la Slaa, wanaonekana kuongozwa na ule upenzi wa mtu bila kufikiria beyond. ndo natahadharisha. kuwa Slaa tunamkubali. Kama alialikwa akakubali kushiriki, halafu dakika za mwishoni akasusa bila kutoa taarifa ya kwa nini hatohudhuria, lazima lijenge maswali.

badala ya watu kuhoji kwa nini, wengine humu ndani tunaongozwa na ile kumpenda mtu hata kama amekosea , tunamtetea tu.
 
Tusubiri majibu ya Dr Slaa

nakubaliana na wewe.....inawezekana CCM wamezusha tu. kwani ikizingatia taarifa hiyo imetolewa kwenye front page ya UHURU. inawezekana magazeti mengine yametarifu suala hili lakini UHURU ndo imebeba Ukrasa wa mbele
 
SAMMOSSES:Yes much better,hata mimi nam support kwa sana fisi akiwa hakimu mbuzi hana haki ,big up sana mzee Dr. Slaa
.
 
Hakuna intelijensia wala nini CDM wameishiwa. Ingekuwa Mukama kaingia mitini ungechoka kusoma mipasho ya wanaCDM.

nakupa ushauri siku nyingine mkiandaa kitu kama hiki angalieni kama watu wanaoalikwa wanaenadana.Kwa mfano Mukama type yake ni Mtatiro.Usidhani Mukama kuwa Katibu mkuu basi hadhi yake ni Dr. Slaa.Umekosea sana.Lakini usijali kwani kukosea ndio kujifunza.
 
nakubaliana na wewe.....inawezekana CCM wamezusha tu. kwani ikizingatia taarifa hiyo imetolewa kwenye front page ya UHURU. inawezekana magazeti mengine yametarifu suala hili lakini UHURU ndo imebeba Ukrasa wa mbele

Kuuuuumbe!! source ni uhuru magamba wenyewe. Kama hivyo kwa nini kupoteza muda kuongea pumba??
leteni mjadala mwingine huu hauna maana tena
 
Kumbe source ni UHURU? UHURU=MZALENDO=HABARILEO=DAILY NEWS= TBC= JAMBO LEO=CCM= TAZAMA TANZANIA= FREEMASONS= SATAN= HELL.
 
Back
Top Bottom