MAPUMA MIYOGA
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 3,792
- 2,369
Hapo kachemka wasitoe misaada ya pesa na watu wao wakale wapi? Unaipa msaada nchi pesa halafu unaleta watu wako waje kuzibomolea huku kama wasimamizi wa hizo pesa na hayo uliyotolea msaada.Misaada ya pesa haiji kukoma ng`o.Na ambao hataki ikomeshwe kama hajui ni hao wanaotoa wenyewe.Hiyo hotuba aliyotoa ni mwiba kwa CHADEMA.Hawajaangalia wanaowahutubia huwa wanapenda nini.Saa hii watakuwa wamejifungia ndani wanaichambua kama karanga.Take it from me CHADEMA isahau misaada ya fedha toka kwenye nchi hizo walikohutubia.CHADEMA misaada ya fedha toka nje ikipungua wasishangae hotuba zao zimewaponza.
sidhani kama uko serious katika hili. Unataka nchi yetu iwe tegemezi tena kwa kiwango hiki hadi lini?? Kuna tofauti gani ya sasa na wakati ule nchi inaongozwa na malkia wa uingereza akiwa huko huko UK??
HATA KAMA NI UCCM, JARIBUNI KUWA SERIOUS BASI HATA KWA HAYA MACHACHE. Tanzania tunalima chakula kinatutosha kujilisha ,na tena tunaweza kuboresha tukapata zaidi. Misaada tunaenda kuomba kila kukicha ni hela,au walishawahi kuleta na mahindi au mchele kama chakula cha njaa ili tusife?? Siku zote viongozi wetu huomba pesa, nayo huigawana na kuficha uswisi. Uhuru wetu na tanzania yetu ni muhimu mno sasa hivi kuliko ccm na misaada ya hao mabeberu.