Na ndio sifa ya kiongozi anaefaa kuliongoza taifa la watanzania bila kujali imani ya kidini,rangi,ukanda wala kabila.Na kwa kukosa sifa hizo Chadema hawatokuja kuliongoza taifa la Tanzania milele kwa kuwa tunawafahamu na dhamira waliyoibeba inatambulika.JK ni kiongozi wa taifa la watanzania kwenda kanisani kushiriki na watanzania wenzake katika ibada wala sio tatizo.Lakini jiulize kama ingetokea padri Slaa watanzania wangejaribu kumpa uongozi wa nchi angeshirikiana na watanzania wenzake wenye imani tofauti na yeye?
Ni aibu kwa mtu unayetukana matusi badala ya kujenga hoja kujinasibu kuwa mfuasi wa falsafa za Mwalimu Nyerere.Ndiyo akili kubwa ya kumuenzi Mwalimu Nyerere hii?Na hilo la kusema CHADEMA haiwezi kuchukua Dola linapingana na mtazamo wa mwalimu.Vipi Kumuenzi Nyerere ni kwa kuhudhuria Ibada na kufunga mbio za Mwenge?
Leo ni siku ya wanafiki kumuenzi Nyerere bila dhamira ya dhati.Hata wale waliolizwa kuwa mali walizokuwa nazo mwaka 1995 walizipata wapi hadi leo baada ya kifo cha Mwl.Nyerere bado hawajatoa majibu ila wameona fursa kupitia kifo chake na sasa wanajiandaaa kutekeleza dhamira yao ovu iliyozimwa.Wapo wachache wanaoienzi misingi ya Mwl.Nyerere na fikra zake,yaani yale yaliyokua mazuri.Njia bora ya Kumuenzi sio kujenga sanamu au kufunga na kufungua mbio za Mwenge.Ni kuziishi fikra zake.Njia bora kwetu vijana ya kumfufua Mwalimu Nyerere na kulifuta machozi taifa letu lenye majonzi ni kupigania haki,usawa na kupinga ubaguzi na uonevu popote pale huku tukizifanyia kazi falsafa za Mwalimu
Nimeweka baadhi ya nukuu za Mwalimu Nyerere na za Rais wa Sasa Jakaya Kikwete.Je tunasonga mbele kifikra ama tunarudi nyuma kwa kasi?
Watanzania wanataka mabadiliko,wakiyakosa ndani ya chama hiki watayatafuta nje ya chama-Mwl.Jk Nyerere(1995 Ndani ya Mkutano Mkuu wa CCM)
CCM si mama yangu-J.K Nyerere
Small nations are like indecently dressed women. They tempt the evil-minded. -J.K Nyerere.
Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: taabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni"J.K Nyerere
'Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya sana' 01/5/1995
'Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu -ukalikubali, anakudharau!' 01/5/1995
Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika MwalimuNyerere (Januari, 1966)
"Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka rais ambaye atalitambua hilo na ataichukia rushwa hata ukimuangalia anaonyesha kweli anaiichukia rushwa, sio rais ambaye anayesema kweli rushwa ni adui wa haki....lakini ukimuangalia usoni unashangaa na kusema.... aaaah kweli huyu?Mwl.J.K Nyerere
"Poverty is not the real problem of the modern world. For we have the knowledge and resources which could enable us to overcome poverty. The real problem--the thing which causes misery, wars, and hatred among men--is the division of mankind into rich and poor." Mwl.J.K Nyerere
Source inapatikana kwenye hiki kitabu
Reflections On Leadership in Africa' VUB University Press, 2000.
Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?
Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii.
Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga.
Kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ni wajinga tu.
Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe....
Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao (wananchi) na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili.
Kwa mtu msafi kabisa,Ikulu ni Mzigo sio mahali pa kukimbilia- J.K Nyerere
Igeni yale mazuri,yale mabaya muyaache maana katika kipindi cha miaka 25 ni lazima tulifanya makosa,kwani sisi Malaika Tusifanye Makosa?-J.k Nyerere
Tuangalie Nukuu za Rais wa Sasa Jakaya Kikwete
1. Urais wangu hauna ubia.-Jakaya Kikwete
2. Tatizo la umeme ni ukame, mimi siwezi kuilazimisha mvua inyeshe-Jakaya Kikwete.
3. Hawa wanaopata mimba ni kiherehere chao.-Jakaya Kikwete
4. Kama hawa watuhumiwa wa EPA wanasema fedha hizo walizitumia katika uchaguzi, watuenyeshe walizitumiaje(stakabadhi).- Jakaya Kikwete
5. "Mie ndie rais wa kwanza wa Africa kukutana na rais Obama" Jakaya Kikwete
6.......hili ni panga la zamani, haliishi makali ! Jakaya kikwete (wakati anamnadi Basil Pesambili Mramba)
7: Ukitaka Kula ni Lazima nawe uliwe-Jakaya Kikwete
8: Mie ndio mwajiri mkuu...... hata mkigoma miaka 8...... mshahara haungozeki ng'o' Jakaya Kikwete(Akihutubia TUCTA)
10: Uchumi unakua sasa tazama foleni za magari,Maendeleo yana changamoto zake-Jakaya kikwete
11: "Mzee mwinyi alikaa miaka 10 hakuyamalza, mzee Mkapa miaka 10 hakuyamalza, mie miaka 5 sijayamalza na mingne 5 sitayamalza, hvyo basi (kicheko) matatzo hayawezi kwisha" Jakaya Kikwete
12:"Kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi" J. K. (akimtetea mbunge Chitalilo aliyegundulika kuwa kughushi vyeti vya elimu yake. )
13:"Nafikiri imefika wakati Tuwaombe Rafiki zetu wa Scandinavia,Watufundishe kuandika na Kusoma Mikataba haswa ya MADINI,kwani sie hatuna wataalamu hao" - JK Kikwete May'2007
14:Hata mimi nashangaa kwa nini Tanzania ni masikini-Jakaya Kikwete
15: Sipendi Kusutwa - Jakaya Kikwete(Akiwa Kigoma Mwezi February,2013)