Dr Slaa amaliza ziara Marekani

Dr Slaa amaliza ziara Marekani

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amemaliza ziara ya wiki tatu nchini Marekani aliyoalikwa na Umoja wa vyuo vikuu vikubwa nchini humo.

Ziara hiyo iliyomchukua kiongozi huyo majimbo mbalimbali ilipewa jina la 'Vision Tanzania' na ilikuwa ya manufaa makubwa kwake,kwa chama chake na kwa Taifa lake.

Akizungumza jana Jumapili akiwa uwanja wa ndege Marekani kabla ya kuondoka Dr Slaa alisema amejifunza mambo mengi sana ambayo ni faida kubwa kwa Watanzania.

Dr Slaa amekuwa gumzo Marekani katika majimbo kadhaa aliyotembelea kutokana na hotuba alizokuwa anatoa katika vyuo vikuu na sehemu nyinginezo alizotembelea ikiwemo shirika la Anga.

Katika hotuba iliyotikisa wazungu ni pale kiongozi huyo nyota wa Tanzania aliposema CHADEMA haitaki pesa za wamarekani bali wanachokitaka kutoka kwao ni Utaalamu wao (Skills).Hotuba ya Dr Slaa na uthubutu wake mbele ya wazungu imesababishwa kufananishwa na Hotuba za Mwl Nyerere aliyekuwa anawakemea wazungu bila woga.

Wiki hii mitandao ya kijamii nchini Kenya ilitawaliwa na Hotuba ya Dr Slaa iliyosambazwa na kuchukuliwa kama 'The greatest speech from African Politician'

Dr Slaa anawasili nchini huku Muungano wa Upinzani ukitarajiwa kukutana na Rais Kikwete kesho kujadili mustakabali wa Katiba mpya.

Source:http://m.mjengwablog.com/siasa/item/6338-dk-slaa-arejea-tanzania-baada-ya-kumaliza-ziara-nchini-marekani.html
 
Katika hotuba iliyotikisa wazungu ni pale kiongozi huyo nyota wa Tanzania aliposema CHADEMA haitaki pesa za wamarekani bali wanachokitaka kutoka kwao ni Utaalamu wao (Skills)l

Hapo kachemka wasitoe misaada ya pesa na watu wao wakale wapi? Unaipa msaada nchi pesa halafu unaleta watu wako waje kuzibomolea huku kama wasimamizi wa hizo pesa na hayo uliyotolea msaada.Misaada ya pesa haiji kukoma ng`o.Na ambao hataki ikomeshwe kama hajui ni hao wanaotoa wenyewe.Hiyo hotuba aliyotoa ni mwiba kwa CHADEMA.Hawajaangalia wanaowahutubia huwa wanapenda nini.Saa hii watakuwa wamejifungia ndani wanaichambua kama karanga.Take it from me CHADEMA isahau misaada ya fedha toka kwenye nchi hizo walikohutubia.CHADEMA misaada ya fedha toka nje ikipungua wasishangae hotuba zao zimewaponza.
 
Kwa hiyo ulitaka aseme ukombozi wa Tanzania utapatikana kwa pesa ya wamarekani? Dont be serious!
 
East Africa Eagle:

Msaada wa nchi yaani bajeti tegemezi, soma vyema na pia elewa hotuba husika.
 
Kwa hiyo ulitaka aseme ukombozi wa Tanzania utapatikana kwa pesa ya wamarekani? Dont be serious!

Kwani hakuwa na kitu kingine cha kuongelea ilikuwa lazima aongelee hilo tu? Au mlimwandikia na akashindwa kuchukua hoja achanganye na akili za kwake ili apate cha kuongelea kingine?
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amemaliza ziara ya wiki tatu nchini Marekani aliyoalikwa na Umoja wa vyuo vikuu vikubwa nchini humo.
Hivi wewe unavifahamu vyuo vikuu vikubwa Marekani kama siyo kuonyesha jinsi usivyofahamu kile unachoandika.

Nyenzo zote za kutafiti, kujifunza na uelewa umepewa lakini kwa uvivu au kutokuelewa kutumia inakufanya uonekane bado uko gizani na hufahamu kile unachokiandika.

Hata kutumia google search engine napo mpaka tukufundishe?.

Akili za kibavicha ni hasara tupu.
 
Huwa huna hadhi ya kujibu post yangu.You are in my Ignore List!
 
Hivi wewe unavifahamu vyuo vikuu vikubwa Marekani kama siyo kuonyesha jinsi usivyofahamu kile unachoandika.

Nyenzo zote za kutafiti, kujifunza na uelewa umepewa lakini kwa uvivu au kutokuelewa kutumia inakufanya uonekane bado uko gizani na hufahamu kile unachokiandika.

Hata kutumia google search engine napo mpaka tukufundishe?.

Akili za kibavicha ni hasara tupu.
Viwe vyuo vidogo au vikubwa lakini kilicho muhimu ni kuwa ujumbe umefika.
 
Hivi wewe unavifahamu vyuo vikuu vikubwa Marekani kama siyo kuonyesha jinsi usivyofahamu kile unachoandika.

Nyenzo zote za kutafiti, kujifunza na uelewa umepewa lakini kwa uvivu au kutokuelewa kutumia inakufanya uonekane bado uko gizani na hufahamu kile unachokiandika.

Hata kutumia google search engine napo mpaka tukufundishe?.

Akili za kibavicha ni hasara tupu.
Mwambie wewe maana hawa jamaa akili wameshikiwa hata milango ya faham pia hebu ZINDUKA kijana Molemo
 
Last edited by a moderator:
Wiki hii mitandao ya kijamii nchini Kenya ilitawaliwa na Hotuba ya Dr Slaa iliyosambazwa na kuchukuliwa kama 'The greatest speech from African Politician'
Kweli kipofu akiona mwezi inakuwa ni balaa. Inavyoonekana Dr.nSlaa hakuwahi kusafiri na kukaa Marekani hata kwa wiki moja. This was beyond his aura.

Ulaghai wenu CHADEMA utawamaliza.

Tanzania kuna blogs kwa makumi kama siyo mamia. You can start blogs within a minute and you don't need to acquire legal document.

Kwa akili za kibavicha kuonekana neno Dr. Slaa kwenye blog inayo copy & paste Kenya affairs imekuwa ni exposure.

Akili za bavicha n hasara tupu.
 
Next time jaribu kujitunzia heshima uko huru kusema chochote lakini si kwa kiwango hiki. This is too low Mwigulu.

Pls Mods angalieni maadili ya jukwaa hili.

Nafikiri alichotaka kusema Slaa kama padri mfukuzwa anayejua maadili ya ndoa aliyokuwa akifundisha wakati padri alitakiwa asafiri na mke wa ndoa aliyefunga naye kwa kanuni za kikatoliki.Lakini huyo aliyeenda naye (of-course walikuwa wanalala naye) kachemka.Ila lugha aliyotumia mwandishi kali lakini ujumbe ndio huo.
 
Next time jaribu kujitunzia heshima uko huru kusema chochote lakini si kwa kiwango hiki. This is too low Mwigulu.

Pls Mods angalieni maadili ya jukwaa hili.

Naunga mkono- Mod- hii ni kashfa katika maisha binafsi ya mtu. HAIFAI KABISA! MADA NI YA UJUMLA WAKE, HUYU ANATUKANA! PLEASE MWONDOE!
 
.....Misaada ya pesa haiji kukoma ng`o.
.....Take it from me CHADEMA isahau misaada ya fedha toka kwenye nchi hizo walikohutubia.
.....CHADEMA misaada ya fedha toka nje ikipungua wasishangae hotuba zao zimewaponza.
Hebu soma tema post yako uone usivyokuwa makini kiuandishi.

Inavyoonekana wengi wenu hamjui malengo na madhumuni ya ziara ya Slaa mnajiandikia tu.
 
Mkuu Feedback huo msukule wa Lumumba usikupotezee muda.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom