DASA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 1,031
- 301
- Thread starter
- #21
Ilikuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, ambapo katika kura za maoni za ccm, dr. Slaa alimshinda mpinzani wake Patrick Qoro ambaye kwa wakati huo alikuwa mbunge anayelitetea nafasi yake ya ubunge, na dr. slaa alikuwa diwani kupitia ccm pia kwa wakati huo.
Kama kawaida ya ccm huwa wanautaratibu wa kupeleka majina ya wagombea kuanzia mshindi wa kwanza mpaka wa tatu kwenye kamati kuu, ambayo ndiyo itakayoamua nani awe mbunge.
Majina yalipopelekwa dodoma, kamati kuu ya ccm waliamua kulirejesha jina la Patrick Qoro kutetea nafasi yake ya ubunge kwenye uchaguzi mkuu, kwa kigezo kwamba Dr. Slaa alikuwa hauziki kwa wananchi wa karatu.
Matokeo hayo yaliwakasirisha sana wananchi wa karatu, mpaka wakaamua kuandamana mpaka nyumbani kwa Dr. Slaa, wakamwambia chagua chama chochote cha siasa tutakuchagua. Kabla Dr. Slaa hajaamua nini cha kufanya, wazee wakawa wamemletea fomu ya kugombea ubunge kupitia chadema, wakamwambia saini hapa na usipige kampeni kaa nyumbani sisi tutamaliza kazi. Dr. Slaa hakuwa na lakufanya, ilibidi akubali sauti ya wengi, ambayo ni sauti ya mungu.
Mkuu hapo kwenye red uhakika ukoje, maana ndio mara yangu ya kwanza kusikia.