Chakunyuma
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 810
- 152
Nashukuru kwa historia safi kabisa nataka kujua huyo mgombea aliye mpisha Dr yupo? anajisikiaje anapoona hakufanya makosa?Wakuu wote mmejitahidi kusema vizuri,isipokuwa tu 1995 katika majina yaliyoletwa na ccm kugombea ubunge wa jimbo la karatu yalikuwa Dr. Slaa na Patrick Qorro kura ya maoni ndani ya ccm dr Slaa alimshinda PQ lakini matokeo ya cc ya ccm jina la PQ likarudi kama mgombea wa ubunge kwa tiketi ya ccm.
Wazee wa Karatu kwa kuwa walishachoshwa na mbunge PQ. walienda kumwomba Dr Slaa agombee kwa ticket ya nccr mageuzi na haikuwa kazi rahisi kumtoa Dr. Slaa kwenye ccm,ilitumika tu HEKIMA.
Wale wazee walipoendelea kumwomba akawakubali lkn aliyekuwa anagombea kwa ticket ya nccr mageuzi akakataa kuondoa jina lake mpaka pale wananchi wa krt walipomwomba aliyekuwa mgombea kwa ticket ya CDM akakubali kumpisha Dr Slaa agombee. Naamini matokeo unajua ila ulitaka kufahamu ilikuwaje.
Hiyo ndiyo safari ya mageuzi ilivyoanza pale karatu. Wananchi ambao huwa hawachaguliwi nani wa kuwaongoza.