Dr. Slaa alikuwa CCM kabla ya kujiunga na CDM, kilitokea nini pale karatu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa alikuwa CCM kabla ya kujiunga na CDM, kilitokea nini pale karatu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DASA, Oct 18, 2011.

 1. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nadhani katika mambo ambayo CCM haitakaa kusahau na itaendelea kujuta mpaka siku kitakapokuwa chama cha upinzani ni pamoja na kuleta mizengwe pale karatu wakati wa kura za maoni kati ya Dr Slaa na aliyekuwa mbunge wa karatu enzi hizo aliyekuwa anaitwa Qoro kupitia CCM. kulikuwa na mizengwe ambayo ilimpelekea Dr. Slaa kuhamia CDM.

  Ilikuaje, ni kilitokea, hebu tukumbushane hii historia nzuri kwa CDM na upinzani kwa ujumla, kama kuna mtu anaelewa vizuri nini kilitokea.
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ccm walimtupa kwenye dampo
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Ilikuwa hivi;
  Wananchi wa Karatu walichoshwa na mbunge wao wa wakati huo ambaye alikuwa anaitwa Matheo Quaresh kama sijakosea jina. Wakatuma ujumbe kumfuata Dr. Slaa ambaye alikuwa anaishi Dar kumwomba akagombee ubunge Karatu. Alikubali na akaenda kuchukua form kwenye chama chake cha CCM kuomba ateuliwe kuwa mgombea ubunge jimbo la Karatu kwa tiketi ya CCM.

  Katika kura za awali ambazo ni kura za maoni Dr. Slaa aliibuka kidedea mshindi dhidi ya Matheo Quoresh. Mizengwe kama kawaida ya CCM iliibuka kwenye kupitia kura za maoni kitaifa ambako jila la Dr. Slaa lilitupwa nje ya uringo kwa hoja iliyozoeleka kwamba si mwenzao, na wakapitisha jina la mbunge wa zamani kuendelea kutetea kiti hicho na Dr. kutupwa nje bila ridhaa ya wananchi bali na kikundi kidogo cha vigogo wa CCM wenye hulka ya kulinda.

  Wananchi wa Karatu waliporudishiwa jina la mgombea ambaye wao hawakumtaka, walilikiataa katakata na kumwomba Dr. Slaa agombee kupitia chama kingine cha siasa na kumwahidi kumpigia kura si kwa mlengo wa kichama ila uwezo wake. Na tukumbuke kabla yake Dr. alishafanya huduma nyingi za kijamii wakati yupo katika kofia nyingine. Dr. Akakubali na kuwa na mtihani wa chama gani agombee ubunge maana ni mambo ya papo kwa papo.

  Sera za Chadema zilimvutia na hivyo kuamua kuwasikiliza wananchi Karatu kilio chao na kugombea ubunge. Na kwa mshangao mkubwa katika uchaguzi huo alimtupa mbali sana mpinzani wake kutoka CCM na hivyo kuanza kuliongoza jimbo la uchaguzi la Karatu na kugeuka kuwa ngome ya upinzani wakati ilikuwa bustani ya uhakika ya CCM kwenda chuma matunda mazuri wayapendayo.

  Nyerere alitoa kauli yake kwa yaliyojilia kwa kusema, watu hawa nawafahamu, na kwamba siku za nyuma jambo kama hili lilishatokea kwa kutoa mfano ambao kwa sasa siukumbuki. Alisema watu hawa wakishaamua juu ya mtu wao wanayemtaka, waachieni vinginevyo ni kuumbuka kama ilivyotokea.

  Ukweli ni kwamba CCM hawapendi kuongelea jambo hilo, kinachofanyika ni kufunikafunika ukweli, lakini kwa sasa kinachoendelea ni kile tunachoweza kujifunza toka Biblia kwamba "Jiwe la pembeni lililokataliwa na waashi limekuwa jiwe kuu la msingi.  "Jiwe lililokataliwa na waashi limekuwa jiwe kuu la msingi!"

   
 4. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Walimtupa dampo au walimnusuru kuingia dampo!.
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Masahihisho

  Karatu hakuja wahi kuwa na mbunge anayeitwa quores

  Kulikuwa na mbunge anaitwa Matteo Qaresi (aliwahi kuwa waziri pia) alitokea Babati Vijijini

  Rafiki yake mkubwa na Mkapa
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Ilikuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, ambapo katika kura za maoni za ccm, dr. Slaa alimshinda mpinzani wake Patrick Qoro ambaye kwa wakati huo alikuwa mbunge anayelitetea nafasi yake ya ubunge, na dr. slaa alikuwa diwani kupitia ccm pia kwa wakati huo.

  Kama kawaida ya ccm huwa wanautaratibu wa kupeleka majina ya wagombea kuanzia mshindi wa kwanza mpaka wa tatu kwenye kamati kuu, ambayo ndiyo itakayoamua nani awe mbunge.

  Majina yalipopelekwa dodoma, kamati kuu ya ccm waliamua kulirejesha jina la Patrick Qoro kutetea nafasi yake ya ubunge kwenye uchaguzi mkuu, kwa kigezo kwamba Dr. Slaa alikuwa hauziki kwa wananchi wa karatu.

  Matokeo hayo yaliwakasirisha sana wananchi wa karatu, mpaka wakaamua kuandamana mpaka nyumbani kwa Dr. Slaa, wakamwambia chagua chama chochote cha siasa tutakuchagua. Kabla Dr. Slaa hajaamua nini cha kufanya, wazee wakawa wamemletea fomu ya kugombea ubunge kupitia chadema, wakamwambia saini hapa na usipige kampeni kaa nyumbani sisi tutamaliza kazi. Dr. Slaa hakuwa na lakufanya, ilibidi akubali sauti ya wengi, ambayo ni sauti ya mungu.
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkuu mateo Qaresi alikuwa mbunge wa babati siyo karatu.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mbunge wa Karatu alikuwa anaitwa Patrick Qoro
   
 9. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Wakuu wote mmejitahidi kusema vizuri,isipokuwa tu 1995 katika majina yaliyoletwa na ccm kugombea ubunge wa jimbo la karatu yalikuwa Dr. Slaa na Patrick Qorro kura ya maoni ndani ya ccm dr Slaa alimshinda PQ lakini matokeo ya cc ya ccm jina la PQ likarudi kama mgombea wa ubunge kwa tiketi ya ccm.

  Wazee wa Karatu kwa kuwa walishachoshwa na mbunge PQ. walienda kumwomba Dr Slaa agombee kwa ticket ya nccr mageuzi na haikuwa kazi rahisi kumtoa Dr. Slaa kwenye ccm,ilitumika tu HEKIMA.

  Wale wazee walipoendelea kumwomba akawakubali lkn aliyekuwa anagombea kwa ticket ya nccr mageuzi akakataa kuondoa jina lake mpaka pale wananchi wa krt walipomwomba aliyekuwa mgombea kwa ticket ya CDM akakubali kumpisha Dr Slaa agombee. Naamini matokeo unajua ila ulitaka kufahamu ilikuwaje.

  Hiyo ndiyo safari ya mageuzi ilivyoanza pale karatu. Wananchi ambao huwa hawachaguliwi nani wa kuwaongoza.
   
 10. Suip

  Suip JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,042
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Hapo penye herufi kubwa ni kuwa hajawahi kuwa DIWANI kaangalieni cv za humu jamvini,alikuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania na Mratibu wa Taasisi ya Wasioona.
   
 11. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sifa kubwa ya wana CCM ni kutoa majibu mepesi kama upepo,sikushangai unatoa majibu kama JK vile.
   
 12. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  mbona mnatuchanganyia habari hapa!mara alikuwa diwani,mara no,mara mbunge aliyekuwepo alikuwa qoro/querres/ qares nk.Sasa tuchukue zapi? .tunaomba wana karatu watupe habari nzuri na za uhakika.
   
 13. Chuck j

  Chuck j JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 1,987
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  Lowasa kama unataka URAIS TUBU
  uTUBU KWA WATANZANIA WOTE.Kwanza waeleze sababu ya kuacha uwaziri ukuu
  pili kilichotokea kwenye RICHMOND.
  KAMA MLISHIRIKI NA kIKWETE.
  NNE CHAFUA KITI.'
  How Mwenyekiti kakutosa, kakaa kimya
  baada ya kuona unashutumiwa yeye kanyamazia au kashiriki kukumaliza kisiasa.
  Ulishirikiana nae kujenga nchi kakuacha,MTOSE"""'''''''''
   
 14. N

  Ngoiva Lewanga Senior Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unanikumbusha historia ya chief Sarwat wa mbulu enzi za mwalimu.
   
 15. n

  nyantella JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45

  Once Green always Green! ni kama Sabodo & RA, Banyani Mbaya pesa yake dawa! hivi wakija CDM itawapokea au
   
 16. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  DASA na Wana JF,

  Ingekuwa Vizuri tungempata Mhusika Mwenyewe, Dr. Slaa aje humu ajibu, tumesikia mengi, Sasa tumwombe Dr.Slaa aje ajibu hoja hii
  Hata Mwalimu Nyerere alishatabiri, Mpinzani wa Kweli atatokea CCM

  Nawakilisha
   
 17. facebook

  facebook Senior Member

  #17
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Chadema ni kiusiwa cha makapi? Waliotoswa na CCM wote wanapokelewa CDM
   
 18. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  mkuu soma hapo juu kwenye post yangu,ukiwa na swali lolote kuhusu karatu uniulizi.
   
 19. M

  Makupa JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Naamini kabisa huu.mjadala kaanzisha dk.Slaa mwenyewe
   
 20. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  wewe uliyebaki magamba ndiye mjanja hongera,
   
Loading...