DR. Slaa alifanya uamuzi wa busara, Rose Kamili anajuta

Binafsi naona mkanganyiko mkubwa sana kwa kiongozi mkubwa katika chama ngazi ya Katibu Mkuu kitaifa awe na mke ambaye anaitikadi na mapenzi kwa chama tofauti. Kwa vyovyote katika uongozi mambo mengi ya kikazi huwepo nyumbani, kwani kuna yasiyofichika ofisini, bora kuyahifadhi nyumbani, ndio maana tunaona viongozi katika nafasi nyeti nyumba zao hulindwa hata kama hawako ndani ya nyumba zile.

Dr. Slaa kwa vyo vyote katika hili kulikuwa na jambo ambalo lilimwia vigumu kisiasa kuendelea na huyu Rosi Kamili kwa vile kulikuwa na uwezekano mkubwa wa siri za chama kuvujia chama kingine, kwa usalama wake na wa chama bora jambo hili kulimaliza kisiasa ili kutuliza nerves.
 
Dr. Slaa kwanza pole kwa udhalilishaji anaokufanyia huyo kuwadi wa magamba, pamoja na kumsaidia alipotoswa na magamba kwenye ubunge hana shukrani. Baada ya kuona mafanikio yako na kujua unaelekea kuwa Rais wa TZ awaota u-fist lady wakati si saiz yako. Mwanamke gani huyo hana nidhamu, ebu wana JF niambieni ni mwanasiasa gani yuko chama tofauti na mke wake. Sasa huyu Rose Kamili ana akili kweli, mimi kuanzia alipotumiwa kumfumania mumewe ndipo nilipomuona *****. Ebu angalia Mama Klinton wa Marekani yule kidosho alipotaka kumdhalilisha mumewe alipoweka msimamo. Mimi naiomba mahakama itoe hukumu Dr. amuoe kipenzi chake na mke mwenye nidhamu na mtiifu. Dr. naomba nialike nije kushuhudia na kusheherekea nawe. Dr. endelea kuwa kimya waache mawakili wako waendeshe kesi, wewe endelea kuimarisha. Naishia hapa, udumu Dr. Slaa idumu Chadema chama kitakacho ikomboa Tanzania.
 
Uwepo wa Jf unategemea sana wapuuzi kama nyie kupost uharo.
So far so good!

Rose ni pumba kivyako?
Josephine ni pumba kivyako?
Zinaa ni pumba kivyako?

Kipi ambacho sio pumba kwako? Slaa kuzini na kuzaa na hao wanawake wawili nje ya ndoaa? au kuwa Katibu Mkuu wa chadema basi ndio hata ukosefu wake wa uadilifu kwako ni sawa tu? huyo wadhifa wake unalipiwa mshahara kwa kodi zetu. Ni lazima tuoneshe udhaifu wake wa maadili na uongo wake wa kuita hao kuwa wake zake wakati hajawaoa. Usiwe punguani. Ukweli ubaki kuwa ukweli hata kama ni mchungu.
 
Pumba nyingi hazina mwanzo wala mwisho. Uzinzi ni uzinzi tu. Iwe kwa Rose au kwa Josephine, haibadilishi hilo.
Wangapi ni wazinifu??? Jana tu; wangapi walizini; yamkini hata wewe??? Yuko wapi wa kumpiga yule mwanamke mawe......?
 
Pumba hizi haziwezi kulingana na zile unazo mwaga darasani huku unamezea mate kupewa hata ukuu wa wilaya uache kupambana na chaki .Maana hata leo najiuliza ulipate PhD ya Uchumi na wanafunzi wako kweli wanakuelewa ukiwafundisha ?

Ana PHD huyu? basi yangu naikataa. Hata kufikiri straight kwake ni kazi
 
images
images
images

Mahusiano Dr. Slaa na Rose Kamili
Pingamizi la Rose Kamili dhidi ya Ndoa tarajiwa ya Dr. Slaa ni majeruhi anayetafuta mganga wa kienyeji amponye. Kuna dondoo kadhaa za kujiuliza katika tukio hili:
  1. Dr. Slaa hajawahi kuonekana hadharani na Rose Kamili kwamba ni wachumba, wanandoa au mahusiano ya kindoa katika muda wote ninaomfahamu Dr. Slaa.
  2. Dr. Slaa hawajawahi hata mara moja kutamka juu ya mahusiano yake na Rose Kamili.
  3. Rose Kamili hajaonyesha uthibitisho wa hati ya ndoa ila anatoa maelekezo kwamba ndugu na jamaa wanafahamu ndoa ya kienyeji ilifanyika kitu ambacho hakitambuliwi kisheria.

Kinyume chake:
  • Dr. Slaa ametangaza mara ya kwanza kuwa na mchumba katika kampeni za uchaguzi Mkuu uliopita na kumtambulisha mchumba wake hadharani na mchumba wake huyo kumhudumia Dr. Slaa muda wote hadi sasa.
  • Tangu Dr. Slaa atangaze hivyo Rose kamili hajawahi kuchukua hatua zo zote au kutoa kauli ye yote hadi pale alipoambiwa Dr. Slaa anajiandaa kufunga ndoa na kuamua kuweka pingamizi.
  • Rose kamili hajawahi kuonekana hadharani au kuonyesha dalili ya wazi kwa umma kwamba Dr. slaa ni mchumba au mume wake.
  • Dr. Slaa hajawahi kusema chochote kibaya juu ya Rose Kamili hali kadhalika Rose kamili hajafanya hivyo juu ya Dr. Slaa.

Mgongano wa kisiasa.
Muda wote Dr. Slaa alipokuwa Mbunge wa Karatu kupitia Chadema, Rose Kamili alikuwa diwani huko Babati kupitia CCM.

Dr. Slaa akiwa Candidate wa kiti cha urais kupitia Chadema, Rose Kamili alikuwa anagombea ubunge kupitia CCM na akatolewa nje ya uringo kwa kura za maoni.
Rose Kamili baada ya kutupwa nje ya uringo ndipo alipoamua kugeukia upande wa Chadema kupata ridhaa ya kuendelea na azima yake ya kugombe kiti cha Ubunge.
Rose Kamili baada ya kushindwa kwa kura dhidi ya mpinzani wa CCM, kwa huruma Chadema wakamzawadia ubunge wa viti maalum na akapokea kwa unyonge mkubwa.

Dr. Slaa alijihadhari dhidi ya Rose kamili
Dr. Slaa angeshinda kiti cha Urais kwa tiketi ya Chadema na anayesema kwamba alikuwa mke wake na angeshinda kuwa mbunge kwa tiketi ya CCM, maana yake Rais kutoka Chadema angekuwa na mke ambaye ni wa kutoka CCM wakiishi pamoja wenye itikadi tofauti.
Hapa kuna picha kamili ya yaliyojilia, kwani muda mrefu tu Rose kamili hakuwa upande wa Chadema aliko Slaa kiitikadi, wakati huo Dr. Slaa amekuwa na wadhifa mkubwa chamani akiwa Katibu Mkuu na pia Mbunge. Kama katibu mkuu wa chama kuna mambo mengi ndani ya nyumba ambayo ni siri za chama mke anaweza kuzijua na kuzivujisha kwa CCM kwa vile ndiko aliko na mapenzi nako.

Jambo hili kwa mtazamo wangu isingewezekana Dr. Slaa aamua kufunga ndoa na mwanamke ambaye anaonekana kisiasa yuko kinyume kabisa na msimamo wake wakati ana wadhifa mkubwa kitaifa. Kwa vyo vyote uamuzi wa busara ulihitajika na ndivyo alivyofanya Dr. Slaa. Rose Kamili alikosa ustahimilivu na unyenyekevu na kuwa na jicho la kuona mbali, mwenzake Mshambuzi aliwahi kuona.

Mshambuzi ameonyesha ukomavu wa hali ya juu, uvumilivu wa hali ya juu na kujituma kwa hali ya juu dhidi ya mchumba wake Dr. Slaa. Hadi damu imemtoka dhidi ya mchumba wake ni dalili tosha aliamua kwa moyo wake liwalo na liwe Josephine Mshumbuzi once for all Dr Slaa projected her all in all for life. Rose Kamili ana nini binafsi alichoonyesha katika maisha yake kwa Dr. Slaa kama ana upendo wa kweli tukilinganisha na Josephine Mshumbuzi?

Nguvu ya Pingamizi la Ndoa
Katika kesi nyingi unahitajika ushahidi wa hati za ndoa ambazo ni kithibitisho kwamba kuna ndoa ambayo imefungwa kisheria iwe ni serikalini au kanisa katoliki ambalo huongozwa na Canon Law.
Ndoa za kimila hazina hati na hivyo hazitambuliwi kama ndoa. Sina hakika kama utoaji mahari ni uthibitisho wa kufunga ndoa kimila, lakini kisheria halikubaliki.

mpendwa,

umechemka!!

sheria za tanzania zinatambua ndoa za aina tatu:

1. ndoa za kiserikali
2. ndoa za kidini
3. ndoa za kimila

kutokana na kutambulika kwa ndoa hizi, ndio maaana hata mahakama zetu huchukulia kitendo cha mahari kurudishwa kama uthibitisho wa kuvunjika kwa ndoa husika. kazisome vizuri sheria kabla ya kuja hapa na mahaba na dk. slaa bila weledi wa sheria

ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God!
 
Binafsi naona mkanganyiko mkubwa sana kwa kiongozi mkubwa katika chama ngazi ya Katibu Mkuu kitaifa awe na mke ambaye anaitikadi na mapenzi kwa chama tofauti. Kwa vyovyote katika uongozi mambo mengi ya kikazi huwepo nyumbani, kwani kuna yasiyofichika ofisini, bora kuyahifadhi nyumbani, ndio maana tunaona viongozi katika nafasi nyeti nyumba zao hulindwa hata kama hawako ndani ya nyumba zile.

Dr. Slaa kwa vyo vyote katika hili kulikuwa na jambo ambalo lilimwia vigumu kisiasa kuendelea na huyu Rosi Kamili kwa vile kulikuwa na uwezekano mkubwa wa siri za chama kuvujia chama kingine, kwa usalama wake na wa chama bora jambo hili kulimaliza kisiasa ili kutuliza nerves.

mpendwa,

usichanganye siasa na ndoa!

slaa alimpenda rose kama mwanammke na akazaa nae watoto wawili. sidhani kama alimpenda rose kama "mwana-ccm"

pia ukumbuke kuwa kabla slaa hajahamia cdm alikuwa ccm an aalihamia cdm baada ya kutoswa kura za maoni za ubunge mwaka 1995!

na usistaajabu kukuta kuwa hadi leo, slaa ni ccm damu damu!!

yote yanawezekana katika siasa za tanzania. watu wanazingatia maslahi binafsi kwanza klabla ya maslahi ya taifa!!

ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God!
 
Jumlisha yote hayo kwa sentensi moja kwamba Dr. Slaa ni mtu ambaye ni "decisive". Nadhani huwezi kuwa na President Dr. Slaa halafu akaachia mambo yanakwenda shagalabagala kama yanavyokwenda Tanzania hivi sasa.Huwezi kuwa na nchi mambo yanakwenda hovyo halafu wewe unakwenda kula vitumbua ulaya. Oh Loard save us
 
mpendwa,

umechemka!!

sheria za tanzania zinatambua ndoa za aina tatu:

1. ndoa za kiserikali
2. ndoa za kidini
3. ndoa za kimila

kutokana na kutambulika kwa ndoa hizi, ndio maaana hata mahakama zetu huchukulia kitendo cha mahari kurudishwa kama uthibitisho wa kuvunjika kwa ndoa husika. kazisome vizuri sheria kabla ya kuja hapa na mahaba na dk. slaa bila weledi wa sheria

ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God!

Nashukuru kwa hilo, lakini mimi niliongelea zaidi ndoa zenye kutoa hati za ndoa ambazo ni za kiserikali na kidini. Kwa vyo vyote mwenye kufunga ndoa kanisani kizuizi lazima kiwe ni hati halali ya ndoa inayotambuliwa na kanisa au serikali. Hizi ndoa za mkeka ni danadana isiyo na hakika na pengine husumbua vichwa.
 
mpendwa,

usichanganye siasa na ndoa!

slaa alimpenda rose kama mwanammke na akazaa nae watoto wawili. sidhani kama alimpenda rose kama "mwana-ccm"

pia ukumbuke kuwa kabla slaa hajahamia cdm alikuwa ccm an aalihamia cdm baada ya kutoswa kura za maoni za ubunge mwaka 1995!

na usistaajabu kukuta kuwa hadi leo, slaa ni ccm damu damu!!

yote yanawezekana katika siasa za tanzania. watu wanazingatia maslahi binafsi kwanza klabla ya maslahi ya taifa!!

ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God!

Kuna kitu ambacho hujanielewa. Mapenzi, ndoa na security in administration. Kiongozi wa nchi au kiongozi ambayo yupo katika nafasi kubwa ya kutunza siri za kitaifa kichama au nafasi nyeti nyingine ni muhimu kuangalia suala hilo kwa vile mambo mengi ya kiuongozi wigo wake umepanuka hadi nyumbani na chumbani. Siri nyingi za kikazi ziko nyumbani. Hivyo mapenzi ya dhati kwa mumewe angetakiwa kugeukia aliko mume wake ili kuwa kitu kimoja katika majukumu aliyo nayo mume wake hasa Dr. Slaa alipochaguliwa kuwa Katibu mkuu wa Chadema. Lakini hili la kubaki ameng'ang'ania tu upande ambao ni kinyume cha aliko mume wake ni kasoro na ni hatari kwa usalama wa mume kwa nafasi aliyo nayo na pia hatari ya siri nyingi za kazi za mume wake kuvuja.

Slaa alipochaguliwa na Chama chake kuwa Mgombea wa Uraisi Tanzania, Rose Kamili aliendelea kuegemea CCM kugombea ubunge kupitia chama hicho. Je, Slaa angechaguliwa kuwa Rais wa Tanzania angekuwa na Mke ambaye ni kutoka chama cha upinzani cha CCM, mambo hayo hata kwa usalama tu wa kiongozi hayakubaliki na vyombo vinavyolinda usama wa Kiongozi wa nchi jambo hili ingawa si sheria lakini ni common sense tu.

Kumbuka Kikwete au Mukama wake zao wawe wanachama na wafuasi tikitiki wa Chadema, whats gona be?
 
Jumlisha yote hayo kwa sentensi moja kwamba Dr. Slaa ni mtu ambaye ni "decisive". Nadhani huwezi kuwa na President Dr. Slaa halafu akaachia mambo yanakwenda shagalabagala kama yanavyokwenda Tanzania hivi sasa.Huwezi kuwa na nchi mambo yanakwenda hovyo halafu wewe unakwenda kula vitumbua ulaya. Oh Loard save us

Umesema kweli, kwani tukio la uamuzi huo ambao unaonekana kuwa na manufaa kwa kazi na chama chake ni uamuzi mgumu ambao una ugumu wake lakini wataka moyo, na aliweza vinginevyo siku hizi siri nyingi za Chadema zingekuwa nje nje tu, maana katibu Mkuu ndiye siri ya Chama.
 
Back
Top Bottom