DR. Slaa alifanya uamuzi wa busara, Rose Kamili anajuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DR. Slaa alifanya uamuzi wa busara, Rose Kamili anajuta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 14, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  Mahusiano Dr. Slaa na Rose Kamili
  Pingamizi la Rose Kamili dhidi ya Ndoa tarajiwa ya Dr. Slaa ni majeruhi anayetafuta mganga wa kienyeji amponye. Kuna dondoo kadhaa za kujiuliza katika tukio hili:
  1. Dr. Slaa hajawahi kuonekana hadharani na Rose Kamili kwamba ni wachumba, wanandoa au mahusiano ya kindoa katika muda wote ninaomfahamu Dr. Slaa.
  2. Dr. Slaa hawajawahi hata mara moja kutamka juu ya mahusiano yake na Rose Kamili.
  3. Rose Kamili hajaonyesha uthibitisho wa hati ya ndoa ila anatoa maelekezo kwamba ndugu na jamaa wanafahamu ndoa ya kienyeji ilifanyika kitu ambacho hakitambuliwi kisheria.

  Kinyume chake:
  • Dr. Slaa ametangaza mara ya kwanza kuwa na mchumba katika kampeni za uchaguzi Mkuu uliopita na kumtambulisha mchumba wake hadharani na mchumba wake huyo kumhudumia Dr. Slaa muda wote hadi sasa.
  • Tangu Dr. Slaa atangaze hivyo Rose kamili hajawahi kuchukua hatua zo zote au kutoa kauli ye yote hadi pale alipoambiwa Dr. Slaa anajiandaa kufunga ndoa na kuamua kuweka pingamizi.
  • Rose kamili hajawahi kuonekana hadharani au kuonyesha dalili ya wazi kwa umma kwamba Dr. slaa ni mchumba au mume wake.
  • Dr. Slaa hajawahi kusema chochote kibaya juu ya Rose Kamili hali kadhalika Rose kamili hajafanya hivyo juu ya Dr. Slaa.

  Mgongano wa kisiasa.
  Muda wote Dr. Slaa alipokuwa Mbunge wa Karatu kupitia Chadema, Rose Kamili alikuwa diwani huko Babati kupitia CCM.

  Dr. Slaa akiwa Candidate wa kiti cha urais kupitia Chadema, Rose Kamili alikuwa anagombea ubunge kupitia CCM na akatolewa nje ya uringo kwa kura za maoni.
  Rose Kamili baada ya kutupwa nje ya uringo ndipo alipoamua kugeukia upande wa Chadema kupata ridhaa ya kuendelea na azima yake ya kugombe kiti cha Ubunge.
  Rose Kamili baada ya kushindwa kwa kura dhidi ya mpinzani wa CCM, kwa huruma Chadema wakamzawadia ubunge wa viti maalum na akapokea kwa unyonge mkubwa.

  Dr. Slaa alijihadhari dhidi ya Rose kamili
  Dr. Slaa angeshinda kiti cha Urais kwa tiketi ya Chadema na anayesema kwamba alikuwa mke wake na angeshinda kuwa mbunge kwa tiketi ya CCM, maana yake Rais kutoka Chadema angekuwa na mke ambaye ni wa kutoka CCM wakiishi pamoja wenye itikadi tofauti.
  Hapa kuna picha kamili ya yaliyojilia, kwani muda mrefu tu Rose kamili hakuwa upande wa Chadema aliko Slaa kiitikadi, wakati huo Dr. Slaa amekuwa na wadhifa mkubwa chamani akiwa Katibu Mkuu na pia Mbunge. Kama katibu mkuu wa chama kuna mambo mengi ndani ya nyumba ambayo ni siri za chama mke anaweza kuzijua na kuzivujisha kwa CCM kwa vile ndiko aliko na mapenzi nako.

  Jambo hili kwa mtazamo wangu isingewezekana Dr. Slaa aamua kufunga ndoa na mwanamke ambaye anaonekana kisiasa yuko kinyume kabisa na msimamo wake wakati ana wadhifa mkubwa kitaifa. Kwa vyo vyote uamuzi wa busara ulihitajika na ndivyo alivyofanya Dr. Slaa. Rose Kamili alikosa ustahimilivu na unyenyekevu na kuwa na jicho la kuona mbali, mwenzake Mshambuzi aliwahi kuona.

  Mshambuzi ameonyesha ukomavu wa hali ya juu, uvumilivu wa hali ya juu na kujituma kwa hali ya juu dhidi ya mchumba wake Dr. Slaa. Hadi damu imemtoka dhidi ya mchumba wake ni dalili tosha aliamua kwa moyo wake liwalo na liwe Josephine Mshumbuzi once for all Dr Slaa projected her all in all for life. Rose Kamili ana nini binafsi alichoonyesha katika maisha yake kwa Dr. Slaa kama ana upendo wa kweli tukilinganisha na Josephine Mshumbuzi?

  Nguvu ya Pingamizi la Ndoa
  Katika kesi nyingi unahitajika ushahidi wa hati za ndoa ambazo ni kithibitisho kwamba kuna ndoa ambayo imefungwa kisheria iwe ni serikalini au kanisa katoliki ambalo huongozwa na Canon Law. Ndoa za kimila hazina hati na hivyo hazitambuliwi kama ndoa. Sina hakika kama utoaji mahari ni uthibitisho wa kufunga ndoa kimila, lakini kisheria halikubaliki.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  all is fair in love and war

  busara hai apply kwenye 'matters of heart'
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Pumba nyingi hazina mwanzo wala mwisho. Uzinzi ni uzinzi tu. Iwe kwa Rose au kwa Josephine, haibadilishi hilo.
   
 4. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,257
  Likes Received: 1,194
  Trophy Points: 280
  huyo rose mzushi tu,anataka ufirst lady 2, mapenzi hayalazimishwi
   
 5. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,257
  Likes Received: 1,194
  Trophy Points: 280
  teh teh uzinz wa no.1 !!??nyani haoni.....
   
 6. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Katika ndoa za kikristu- endapo mwanandoa alikuwa na ndoa ya mitaala, huambiwa achague ni nani anapenda kufunga naye ndoa! Uchaguzi huo haupingiki!

  Slaa ataambiwa achague kati ya Rose na Josephine, akisema Rose - basi mambo yameisha. Kwa serikali nadhani maelezo ya mtoa hoja yana nguvu sana, yaani mwanandoa atapaswa aonyeshe na kuthibitisha kwa dhati kabisa mapenzi yake kwa mwenziwe lakini zaidi jamii iliwaona vipi!

  Je wameisha kinyumba kwa kipindi fulani hata kuwafanya wanajamii waamini hao ni mke na mume!
   
 7. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tatizo unadhani Slaa amezaliwa na kukua 2009! Rose na Slaa have been together for more than 20 good years! Long before massage parlour lady came to know hin!
   
 8. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Dr Slaa anawakosesha magamba usingizi!!! Hila kibao lakini mwisho wa siku, watanzania wanamtaka Dr Slaa awe kiongozi wao!!
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Pumba hizi haziwezi kulingana na zile unazo mwaga darasani huku unamezea mate kupewa hata ukuu wa wilaya uache kupambana na chaki .Maana hata leo najiuliza ulipate PhD ya Uchumi na wanafunzi wako kweli wanakuelewa ukiwafundisha ?
   
 10. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,672
  Trophy Points: 280
  Ungepata na BEHIND THE SCENE hii movie ndo ingenoga.
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hawanielewi ndio maana nikaja humu JF labda mtanielewa, lakini ikiwa mwanafunzi mwenyewe ni kama wewe, sijui? maana unaonesha uwezo wako wa kuelewa ni mdogo sana.
   
 12. k

  kubenafrank Member

  #12
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata Clinton alipatwa na mambo kama haya lkn hayana hoja yeyote na utendaji wake wa kuijenga chadema.Hizo ni mbinu za magamba kutaka kupunguza kasi ya kupigania uhuru wa tanganyika.Dr. tunakuombea Mungu Magamba hawatafanikiwa milele katika mbinu zao chafu
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hiyo ila ni Rose? au ni Josephine?

  Kuzini azini Slaa, dhambi uwasukumie wengine?
   
 14. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hii kesi ni nzuri sana kwa Dr. Slaa kwani naimani kwa vyovyote vile watanzania watafuatilia kwa karibu muda wote, na utawafanya hata wale minority wasiofuatilia habari za Dr. Slaa wafuatilie na ukweli mwisho wa siku utakuja kumpa kile kinachostahili.
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Zomba kama unakaa unawaza posho ya Nape na debe lako la CCM JF hakika hata ufundishaji wako ni buree sana .Mie nakuonea huruma na kujiuliza ikuwaje ukapata PhD hakika maana uko kitumbo zaidi hata shule yako haionekani kokote .Unasikitisha .Unataka ushibe wewe na uko wako huko kwenu wafe njaa kisa una manufaa na CCM ?
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  When the "worse" seems to overshadow the "better," you need to cling to this truth: feelings come and go; commitment does not.
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Jul 14, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Uwepo wa Jf unategemea sana wapuuzi kama nyie kupost uharo.
  So far so good!
   
 18. b

  bibi.com JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,155
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  tusifanye tena kosa la kuchagua kiongozi mzinzi tutalia kama tunavyolia sasa! huwa hawafikirii kwengine zaidi ya ndani ya suruali!
   
 19. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mijitu mingine sijui ipo practical ya journalism? Picha za padri na rose kibao tumeziona mahojiano pia afu watafuta sifa uonekane unamjua?
   
 20. l

  london JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2012
  Joined: Sep 12, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sahihisho ni kwamba ndoa za kimila zinatambulika kisheria ilimradi kuwepo na watu walioshuhudia hiyo ndoa ya kimila. Lakini pia si hilo tu bali pia sheria ya ndoa (Marriage Act, 1971) inaitambua kama ndoa hata km umekaa na mwenziyo under one roof for a period of two years hiyo yote nayo inaitwa marriage.

  Nimeona niweke angalizo hilo. Ila pia sikubaliani na Rose juu ya timing ya maombi yake mahakamani, mambo kadhaa nayaona kwa Rose, kwanza naturally mwanamke yeyote ambaye yuko single lazima aumie au awe na wivu anaposikia mwenziye anataka kufunga ndoa. Nahisi Rose asingeweka pingamizi kama alikuwa amenyaka mtu tayari.

  Pia naturally Rose lazima hisia za kuvinjari na Dr Slaa zimjie make flashback lazima akumbuke ze utamu aliyokuwa anapata na kuona sasa mwenzie anampokonya hata km alishaachia ngazi siku nyingi. Labda awe anamtaka Dr slaa bado, asifunge ndoa ili iwe rahisi kumvuta au kuendelea kubanjua amri ya sita.

  Pili Rose amekuwa na Dr Slaa pamoja na Mshumbuzi kwenye kampeni za uchaguzi 2010 lakini hakukataa kusimama jukwaa moja na mshumbuzi muda wote huo, muda wote wa 2011 na sehemu kubwa ya 2012. Hii inaonyesha Rose ni such an opportunist woman (mama mwenye tamaa ya mali), anafanyakitu kwa kutaka maslahi binafsi, ina maana mshahara wa ubunge na posho hazimtoshi kuhudumia watoto graduate ambao wataanza kazi hivi karibuni.

  Tena watoto ambao wamekopeshwa na bodi ya mkopo kusoma? sasa single women and widows wao watasema nini km mwenye kipato kikubwa hiki bado anatamaa hivi? Kwanza ikumbukwe Rose anapata mshahara wa ubunge usio na jimbo, kwa hiyo hela yake anaitumia yeye atakavyo tofauti na wabunge wenye majimbo, pia tofauti na Dr Slaa ambaye siyo mbunge anategemea posho tu za chama.

  Tatu, nadhani Rose bado ni mfuasi wa CCM na huenda ameahidiwa kiti cha viti maalum hata akitoswa chadema. Hii timing yake kufungua kesi inanipa wasiwasi sana kuwa huenda anatumiwa na CCM kumdhalilisha Dr Slaa.

  Huenda mama huyu kashauriwa vibaya na wana ccm wake kwani kwa taratibu za kanisa katoliki ndoa za kimila hazitambuliki. Kwa hiyo ndoa inaweza kuendelea kufungwa km askofu/padre hataogopa mkwara wa serikalikupitia mahakama yake.
   
Loading...