tusaidie, Zitto akihutubia huko Kasulu amesikika akisema Mgombea wa Urais wa ACT atapatikana mwezi wa nane? Mdahalo huu unaeleza kwamba washindani wa hoja ni wagombea/ Watia nia wa Urais kupitia Vyama vyao.
Swali ni je Dr Slaa anaenda kama nani? Maana hatujasikia akisena kwamba atagombea, wala chama chake hakijampitisha kugombea nafasi hiyo Sasa aende pale kama nani? Tuje kwa Zitto,anaalikwa kwenye Mdahalo kama nani? Hatujasikia akisema kwamba atagombea, Hata Katiba yenyewe haimruhusu kugombea, Chama chake ndo hicho kimesema mgombea kitampata mwezi agost. Yeye anaenda kama nani kwenye mdahalo?
Tukisema huyu mwandaaji wa Midahalo anakurupuka kama mkojo wa Asubuhi tunadanganya? Siku zote Kande ni mchanganyiko wa Mahindi Maharage au Njegere, Ukichanganya Ugali nyama Maharage na Mboga mboga kwa pamoja huo mchanganyiko tunauitaje?
Hapa haogopwi Zitto wala yeyote, Zitto katangaza kuogombea Ubunge huko Kigoma Mjini. Huko kwenye Midahalo ya Watia nia wa Urais anakwenda kufanya nini? Je huu si mpango madhubuti wa kushusha haiba za Wagombea Urais? Huyu mwandaaji wa Midahalo hiyo anawasiliana kwanza na watu anaotaka kufanyanao Midahalo? Kama angekuwa anawasiliana nao nadhani ile hasara ya kutofika kwa watia nia Urais kupitia ccm asingeipata. Na kwakuonyesha umbumbumbu wake kaendelea na utaratibu uleule.. Naam hajajifunza lolote..!!
BACK TANGANYIKA