Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

Dr. Slaa akimbia Mdahalo wa Kesho

Safi sana wazo langu lilikuwa hilohilo kamanda asitokee. Kwanza mdahalo wenyewe ati kupitia azam TV wangapi tungeona. Pili mdahalo unakiingilio shamee kabisa. Tatu wahusika hawaendani kiuzito mmoja (ztto) angetolewa k.o Mara baada ya kipenga kupulizwa
 
huyu muandaa mdahalo anakurupuka ameandaa mdahalo wa wagombea urais au mdahalo wa kuzungumzia watia nia wa urais...kama watia nia kuna vyama bado mchakato haujaanza na kama ni mdahalo wa kuzungumzia mchakato wa urais basi angekipa chama husika mualiko na sio mtu....iweje mdahalo uwashirikishe na wagombea ubunge pamoja na urais sijaona mantiki yake ....mufuruki amejishushia hadhi asiwe na haraka asubiri wagombea wachaguliwe na vyama vyao then aandae .....mdahalo wenyewe unalipa kingilio 100000 ...atakuwa anatafuta hela huyuuuu
 
Mzee ni mwoga sana kisa tu atakuepo Zitto.
 
Last edited by a moderator:
Mfuruki ni kama hajajipanga anaandaje mdahalo na kuutangaza bila mawasiliano na wahusika kujuzwa kabla.
 
Acha ujinga wewe kuwaita watu wezi, ukiambiwa uthibitishe beyound resornable dought utaweza? Au kazi kupokea maneno ya kishabiki ya wanasiasa uchwara halafu unahitimisha ndani ya halmashauri ya kichwa chako kibovu halafu unajipongeza. Mbona humsemi mwizi aliyewauzia mafuso mabovu na maspika mabovu kwenye kampeni zenu 2010?
Mafisadi ya ccm walitakiwa wawe mahabusu lakini wao ndo wanatangaza nia za kugombea uraisi ccm.Lipumba
 
Huyu Mufuruki alikuwa hazijui fitina za wabongo?
 
Umoja wa watendaji wakuu wa kampuni wa CEO RoundTable (CEOrt) umeandaa mdahalo wa kuzungumzia mbio za urais utakaowahusisha viongozi wa vyama vya upinzani, Profesa Ibrahim Lipumba, Dk Willibrod Slaa, Zitto Kabwe na Emmanuel Makaidi, lakini Chadema imesema itakuwa tayari kwa midahalo baada ya mchakato wa ndani kukamilika.


Kauli hiyo ya Chadema inaweza kuwa kikwazo kingine kwa CEOrt kuendesha midahalo hiyo baada ya wa kwanza uliokuwa uhusishe makada 10 wa CCM wanaoomba ridhaa ya chama hicho kuwania urais, kushindwa kufanyika kutokana na viongozi wa sekretarieti kutoa kauli tofauti siku moja kabla.


Kiongozi wa CEO, Ali Mufuruki alisema jana kuwa Dk Slaa, Profesa Lipumba, Makaidi na Zitto, ambaye ni kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo, wamethibitisha kushiriki kwenye mdahalo huo utakaofanyika kesho kuanzia saa 1:00 jioni jijini Dar es Salaam.


Lakini Dk Slaa aliiambia Mwananchi jana kuwa Chadema itakuwa tayari kushiriki kwenye midahalo baada ya kumaliza mchakato wa kupata mgombea wake na kukamilisha Ilani ya Uchaguzi, mambo ambayo alisema hupitishwa na vikao vya juu.


"Kamanda, sijui kama ni kongamano au mdahalo: 1. Chadema inaendeshwa kwa katiba, kanuni na taratibu zake. Hadi siku ya leo taratibu zetu hazijafikia kupata aspirants (watangazania)," alisema katibu huyo mkuu wa Chadema katika ujumbe wake mfupi wa simu.


"2. Kama kuna waliopata aspirants, Chadema bado mchakato wetu unaendelea. 3. Midahalo inafanywa kwa msingi wa ilani. Chadema ilani yetu haijafika bado mbele ya vikao vya maamuzi, yaani Baraza Kuu na Mkutano Mkuu. Hivyo tukienda mdahalo tutakuwa tunazungumzia ilani ipi?


"Hivyo tuko tayari kwa midahalo yote baada ya mchakato wetu wa ndani kukamilika."


Mufuruku alikuwa ametuma taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa facebook na alipopigiwa simu na Mwananchi, alithibitisha kuwapo kwa mdahalo huo ambao alisema utaonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni, redio na intaneti.


Kuhusu ushiriki wa Zitto, ambaye atagombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mufuruki alisema CEOrt imemualika kwa kuwa ni kiongozi wa chama ambacho kinaweza kusimamisha mgombea wa urais.


"Kushiriki si lazima uwe unachukua fomu za kugombea urais. Yeye ni kiongozi wa chama ana mawazo yanayoweza kutoa mchango kwenye mdahalo," alisema Mufuruki.


CEOrt imepanga kufanya midahalo kadhaa mwezi huu na Juni 25 itaendesha mdahalo utakaoshirikisha wagombea kutoka CCM baada ya kada mmoja tu, Balozi Amina Salum Ali, kujitokeza kwenye mdahalo wa kwanza na hivyo kusababisha uahirishwe.


Profesa Lipumba, ambaye amechukua fomu za kuomba ridhaa ya CUF kupitishwa kugombea urais kwa mara ya tano iwapo jina lake litapitishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliiambia Mwananchi jana kuwa atashiriki kwenye mdahalo huo, kama ilivyo kwa Makaidi ambaye amepitishwa na NLD kuwania nafasi hiyo.
 
Acha ujinga wewe kuwaita watu wezi, ukiambiwa uthibitishe beyound resornable dought utaweza? Au kazi kupokea maneno ya kishabiki ya wanasiasa uchwara halafu unahitimisha ndani ya halmashauri ya kichwa chako kibovu halafu unajipongeza. Mbona humsemi mwizi aliyewauzia mafuso mabovu na maspika mabovu kwenye kampeni zenu 2010?

Epa,Richmond ,Escrow n.k siyo wizi ndani ya ccm?
 
ila ccm walipokimbia mliponda yaan CDM hamna jema ukweli no kuwa slaa kamkimbia ZZK,hana uwezo wa kujenga hoja mbele ya Zitto

CCM waliconfirm kushiriki wakaingia mitini dakika za majeruhi tena bila taarifa.Hata hivyo Dr Slaa ataendaje kwenye mdahalo wa wagombea,kwani ameshatangaza nia kuwa ni mgombea? Hapo mwenye sifa ya kushiriki mdahalo ni Prof.Lipumba tu,ZZK hana sifa ya kushiriki kwa vile si mgombea.
 
mkigoma

sawa dr slaa jibu alilokuuliza comrad nape utueleze wahisani wamekuambia nini
 
Last edited by a moderator:
Katika hali isiyokuwa ya kawaida chadema imekimbia mdahalo uliokuwa umeandaliwa kwa ajili ya kuelezea malengo na namna jinsi vyama vya upinzani vilivyojiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu,hali hiyo imekuja mara baad ya chadema kupata taarifa kuwa katika mdahalo huo atakuwepo kiongozi wa act wazalendo ndugu zitto kabwe,awali walikuwa wamekubali kuhudhuria lakini baada ya kupata taarifa ya zitto kushiriki wakakacha na kusingizia hawajaandaa ilani,sababu ya kutokuandaa ilani ni ya kipuuzi kwani mda wa uchaguzi umekaribia na wanasema hawajajipanga,lipumba athibitisha kushiriki
 
Back
Top Bottom