Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa ameweka bayana kwamba chama hicho kikuu cha upinzani nchini hakitashiriki mdahalo wa wagombea Urais wa upinzani hapo kesho.
Kiongozi huyo aliyekuwa anasubiriwa na mamilioni ya Watanzania kwenye mdahalo huo ametoa sababu kubwa mbili kwa chama chake kutoshiriki...
Sababu ya kwanza ni kwamba CHADEMA bado haijampata mgombea Urais na mchakato wa ndani unaendelea.
Na sababu ya pili ni kwamba Ilani ya chama bado haijapitishwa na vikao vya juu vya chama hicho na itakuwa ni kichekesho kwenda kwenye midahalo bila kuwa na Ilani ya chama.
Dr Slaa amesema chama hicho kitakuwa tayari kushiriki midahalo ya aina hiyo mara taratibu za kumpata mgombea Urais zitakapokamilika ndani ya chama!