shizukan
JF-Expert Member
- Jan 16, 2011
- 1,158
- 563
Nampongeza Dr Slaa kwa kusikika baada ya kujificha kwa muda mrefu. Nimefuatialia majibu yake, but kinachonitatanisha ni kwamba, huyu dr hana sera mpya. Kwanini kila akiongea popote lazima atoe reference za EPA na Ufisadi?
Huu ni muda muafaka kwake kubadilika.
Wananchi tunahitaji kupata mapya kutoka kwake. Tunahitaji kusikia juhudi anazozifanya na chama chake kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.
Huu ndio ubongo wetu!! Maisha bora hayaletwi na ahadi mpya majukwaani bali utekelezaji wa yale ulioahidi jana. Umbumbumbu wako unakufanya ufananishe SIASA na BONGO FLEVA. Ufisadi ni tatizo la kudumu na ndio kinachotukwamisha. Tutumie akili zetu kujua matatizo yetu yanaanzia wapi. Mmezoea kusikia maneno matamu na kuyaita tumaini jipya hata kama huoni dalili ya kutekelezwa kwake.
Hapa ndio nashangaa hizi akili zenu za shule za kata. Unapouliza CHADEMA wanafanya juhudi gani kuleta maisha bora unadhihirisha ujinga mkubwa kwa sababu mbili.
1. Unawadai maisha bora kwa mtaji gani uliowapa? Ni CHADEMA ndio wenye dhamana ya rasilimali za nchi? Kama chama cha siasa, ulihitaji walime na kugawa maharage mtaani km CCM walivyogawa sukari Igunga wkt wa uchaguzi ndio uone uwajibikaji wao?
2. Sio kazi ya chama kuwapa maisha bora watanzania. Huu uongo ndio uliowafanya mkawachagua CCM bila kufikiri wanawaahidi nini. Chama kazi yake ni KUJENGA MISINGI BORA na KUTOA TIJA. Misingi bora inajengwa kwa kuondoa ya zamani (km ambavyo CHADEMA wanajaribu kufanya) na kuweka mipya itakayowawezesha wananchi kufanya shughuli zao kwa tija. Maisha bora yataletwa kwa usimamizi mzuri na mgawanyo wa haki wa rasilimali za nchi. (Tofauti na huu wa viongozi kujinufaisha kwa kujiongezea posho kila kukicha) Tumia akili yako ndogo kupambanua mambo kabla hujapost matapishi humu.
Na hii dhana yako ya kuwa Dr.Slaa anajificha nao ni utoto. Ulitaka aseme nini ikiwa hana la kusema kwa wakati huo? Au unafikiri Nape kupita jukwaani akihubiri mambo yasiyo na mashiko ndio anachapa kazi?! If you have nothing to say, say nothing!