Dr Slaa ajibu upotoshaji wa Mwandishi Mayage dhidi ya CHADEMA

Nampongeza Dr Slaa kwa kusikika baada ya kujificha kwa muda mrefu. Nimefuatialia majibu yake, but kinachonitatanisha ni kwamba, huyu dr hana sera mpya. Kwanini kila akiongea popote lazima atoe reference za EPA na Ufisadi?

Huu ni muda muafaka kwake kubadilika.
Wananchi tunahitaji kupata mapya kutoka kwake. Tunahitaji kusikia juhudi anazozifanya na chama chake kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.

Huu ndio ubongo wetu!! Maisha bora hayaletwi na ahadi mpya majukwaani bali utekelezaji wa yale ulioahidi jana. Umbumbumbu wako unakufanya ufananishe SIASA na BONGO FLEVA. Ufisadi ni tatizo la kudumu na ndio kinachotukwamisha. Tutumie akili zetu kujua matatizo yetu yanaanzia wapi. Mmezoea kusikia maneno matamu na kuyaita tumaini jipya hata kama huoni dalili ya kutekelezwa kwake.

Hapa ndio nashangaa hizi akili zenu za shule za kata. Unapouliza CHADEMA wanafanya juhudi gani kuleta maisha bora unadhihirisha ujinga mkubwa kwa sababu mbili.
1. Unawadai maisha bora kwa mtaji gani uliowapa? Ni CHADEMA ndio wenye dhamana ya rasilimali za nchi? Kama chama cha siasa, ulihitaji walime na kugawa maharage mtaani km CCM walivyogawa sukari Igunga wkt wa uchaguzi ndio uone uwajibikaji wao?

2. Sio kazi ya chama kuwapa maisha bora watanzania. Huu uongo ndio uliowafanya mkawachagua CCM bila kufikiri wanawaahidi nini. Chama kazi yake ni KUJENGA MISINGI BORA na KUTOA TIJA. Misingi bora inajengwa kwa kuondoa ya zamani (km ambavyo CHADEMA wanajaribu kufanya) na kuweka mipya itakayowawezesha wananchi kufanya shughuli zao kwa tija. Maisha bora yataletwa kwa usimamizi mzuri na mgawanyo wa haki wa rasilimali za nchi. (Tofauti na huu wa viongozi kujinufaisha kwa kujiongezea posho kila kukicha) Tumia akili yako ndogo kupambanua mambo kabla hujapost matapishi humu.

Na hii dhana yako ya kuwa Dr.Slaa anajificha nao ni utoto. Ulitaka aseme nini ikiwa hana la kusema kwa wakati huo? Au unafikiri Nape kupita jukwaani akihubiri mambo yasiyo na mashiko ndio anachapa kazi?! If you have nothing to say, say nothing!
 
Hizi ni past issues...we need something new, something different
Hata kama ni past issues,lakini kumbuka ndio issues zilizoturudisha nyuma WATANZANIA,na ndio zinazozidi kututesa mpaka leo.Au wewe na MAFISADI wenzio hamlioni hili?
 
Ok...tayari ameshatutoa usingizini! what is next? mbona kila siku anazidi kutuamsha?
waendelee tu kutuamsha. Sisi
wakristo huwa tunasema Yesu atarudi watu wote watakaposikia injili hivyo bac sera za cdm zitakaposambaa kwote mpk huku vijijini tunakoshobokeaga ubwabwa ndo wataendelea na plan B.
 
Swali la zamani hupata jibu la zamani, swali jipya hupata jibu jipya Sheikh.
Daudi...nadhani wewe ni mfuasi mzuri wa CDM, lakini sitaki kukutoa kwenye mada...mna mpango gani na Slaa kwa sasa? Naona kama mmemtenga sana kwenye masuala mbali mbali ya kichama.
 
waendelee tu kutuamsha. Sisi
wakristo huwa tunasema Yesu atarudi watu wote watakaposikia injili hivyo bac sera za cdm zitakaposambaa kwote mpk huku vijijini tunakoshobokeaga ubwabwa ndo wataendelea na plan B.
Plan B ilikuwa kwenda Ikulu kupiga picha na Rais..nayo imefanikiwa kwa 100%
Turudi kwenye main topic dada jane..
 
Hata kama ni past issues,lakini kumbuka ndio issues zilizoturudisha nyuma WATANZANIA,na ndio zinazozidi kututesa mpaka leo.Au wewe na MAFISADI wenzio hamlioni hili?
Kinachotutesa watanzania ni Uvivu wetu. Tukijituma kila kitu kinawezekana...unaweza ukiangalia wenzetu waliondelea wanavyojituma. hizo issue za Ufisadi ni za miaka hii ya karibuni, Umasikini tulikuwa nao toka enzi hizo
 
Daudi...nadhani wewe ni mfuasi mzuri wa CDM, lakini sitaki kukutoa kwenye mada...mna mpango gani na Slaa kwa sasa? Naona kama mmemtenga sana kwenye masuala mbali mbali ya kichama.
Mi sio DAUDI MCHAMBUZI,lakini swali hili linanihusu kama MWANA CHADEMA,nauliza KIVIPI?Funguka.
 
shizukan,shizukan,shizukan.......heshima kwako mkuu nimezipenda point zako inaonesha unakijua unacho kiongea,achilia mbali wajinga wachache wanao halibu zana ya great thinker
 
Mi sio DAUDI MCHAMBUZI,lakini swali hili linanihusu kama MWANA CHADEMA,nauliza KIVIPI?Funguka.
kama katibu mkuu, yeye ndiye mtendaji mkuu wa mambo yote yahusuyo chama...recently sijamsikia kabisa. Chama kimekuwa kikifanya madudu mbali mbali especially lile la kwenda ikulu kupiga picha, kupingana kuhusu posho baina ya wabunge wa CDM, kushiriki maadhimisho ya uhuru, katiba na mengine mengi. Kama katibu mkuu..nilikuwa nategemea kumsikia akiplay role yake, lakini hajaongea chochote, matokeo yake anakuja kumjibu mwandishi na tena shallow na kwa kutoa reference ambazo tumeshazichoka!
 
Kinachotutesa watanzania ni Uvivu wetu. Tukijituma kila kitu kinawezekana...unaweza ukiangalia wenzetu waliondelea wanavyojituma. hizo issue za Ufisadi ni za miaka hii ya karibuni, Umasikini tulikuwa nao toka enzi hizo

Bora uwe na uvivu wa mwili kuliko kuwa na uvivu wa kufikiri. Kusema Watanzania ni wavivu ni matusi. Hizi wanazoiba na kugawana zinatoka kwenye masaburi yako? Mtu mwenye akili kama zako mimi namfananisha na KUKU WA MAYAI. Kuku wa mayai ndiye hutaga yai, likaondolewa pale bandani lkn kesho akataga lingine bila kujiuliza la jana limekwenda wapi.

Ni kweli tunatakiwa tufanye kazi, lkn mustakabali wa jasho letu ni muhimu. Kama tunafanya kazi isiyo na tija hatutaitwa wachapakazi badala yake tuitwe majuha. Kuna faida gani kulima kwa jasho, kuvuna kwa taabu, kuhangaika na kusafirisha mazao toka shambani, halafu tuje kuyaweka ktk ghala lililojaa panya? Huo ndio uchapa kazi?

Strategic issues must first be examined fully before putting effort on execution of the parts. Otherwise ni ujinga. Tena kama una mawazo hayo ujue wewe ni mjinga nambari moja. Ni akili za kitumwa tu ndio zinaruhusu kufanya kazi bila kuangalia mafao yanatumikaje.
 
Kaka Rejao hivi wewe unafikiriaga kuwa kazi za cdm ni zile zinazoelezwaga humu jf tu. Njoo huku vijijini ndo utajua kazi anazozifanya dr wa ukweli na cdm kwa ujumla. Mi ni mwl tena wa shule za msingi niko kijijini sana na kusini mwa tz, sio mchaga lkn nimeelewa nini anachokiongea dr na cdm kwa ujumla. Spirits walioniambukiza hao watu natahakikisha naisambaza kwa kadri ya uwezo wangu. Ukumbuke mi ni mwl ninashinda na watoto mia sita kila siku ambao wana wazazi wao. Mateachers tumejipanga kuleta PANTANZANIZIM instead of PANAFRICANISM. Nyie kaeeni kuongojea Mbowe na Slaa kwenye maandamano. Waacheni wapumzike kazi kubwa walishamaliza.
 
Kaka Rejao hivi wewe unafikiriaga kuwa kazi za cdm ni zile zinazoelezwaga humu jf tu. Njoo huku vijijini ndo utajua kazi anazozifanya dr wa ukweli na cdm kwa ujumla. Mi ni mwl tena wa shule za msingi niko kijijini sana na kusini mwa tz, sio mchaga lkn nimeelewa nini anachokiongea dr na cdm kwa ujumla. Spirits walioniambukiza hao watu natahakikisha naisambaza kwa kadri ya uwezo wangu. Ukumbuke mi ni mwl ninashinda na watoto mia sita kila siku ambao wana wazazi wao. Mateaches tumejipanga kuleta PANATANZAIZIM instead of PANAFRICANISM. Nyie kaeeni kuogojea Mbowe na Slaa kwenye maandamano. Waacheni wapumzike kazi kubwa walishamaliza.
Asante sana dada Jane..kwa hizi red umeelezea dhana nzima ya Chadeama.
Kwa kitendo chako cha kuwa mwalimu wa shule ya msingi na kuweza kuwa internet 24hrz ni juhudi kubwa sana. Umenifanya niamini kila kitu kinawezekana na wote tukiamua tuinaweza. Washauri walimu wenzako wafanye kazi kwa juhudi kama wewe na waache kulalamika kilasiku.
 
Bora uwe na uvivu wa mwili kuliko kuwa na uvivu wa kufikiri. Kusema Watanzania ni wavivu ni matusi. Hizi wanazoiba na kugawana zinatoka kwenye masaburi yako? Mtu mwenye akili kama zako mimi namfananisha na KUKU WA MAYAI. Kuku wa mayai ndiye hutaga yai, likaondolewa pale bandani lkn kesho akataga lingine bila kujiuliza la jana limekwenda wapi.

Ni kweli tunatakiwa tufanye kazi, lkn mustakabali wa jasho letu ni muhimu. Kama tunafanya kazi isiyo na tija hatutaitwa wachapakazi badala yake tuitwe majuha. Kuna faida gani kulima kwa jasho, kuvuna kwa taabu, kuhangaika na kusafirisha mazao toka shambani, halafu tuje kuyaweka ktk ghala lililojaa panya? Huo ndio uchapa kazi?

Strategic issues must first be examined fully before putting effort on execution of the parts. Otherwise ni ujinga. Tena kama una mawazo hayo ujue wewe ni mjinga nambari moja. Ni akili za kitumwa tu ndio zinaruhusu kufanya kazi bila kuangalia mafao yanatumikaje.
hebu kama CDM tuambieni mna strategies gani kama hii ya kuongeza juhudi katika kufanya kazi hamuikubali?
 
Nilisoma hayo maoni ya Mayage lakini kuanzisha chama kipya ameenda mbali sana labda kuboresha ingefaa zaidi. Ningependa kwa hili kutofautiana na watu wengi humu ndani. Maoni ya Mayage yafaa kufikiliwa mara mbili au kuyaboresha. Mimi kwa maoni yangu ningependa kuona CHADEMA ikajua kuwa Ufisadi kwa nchi za Kiafrica ni mfumo wa kimaisha ambao hasa umejengwa na vyama vilivyorithi utawala wa mkoloni.

Ni vigumu sana kutengamisha ufisadi na ukoloni kwani vyote viwili vina matokeo sawa, ikiwa ni pamoja ya kufifisha uchumi wa nchi masikini na pia watu wanaofisadi huwa mara nyingi wanatunza mali zao kwa nchi zilizo endelea kama Uswisi ambako huko watu wanazitumia kama mikopo kwa nchi hizo. Tungependa kuona CHADEMA ijue kuwa huo ni mfumo wa kijamii na ije na ideology mbadala au mfumo mbadala wa maisha.

Kitendo cha kutaja jina la fisadi mmoja au majina wawili au kumi kilipaswa kitambulike kuwa hao Mafisadi ni zao la mfumo tajwa then kuja na mfumo mbadala ambao ungejenga ideology ya chama. Kwa sasa inakuwa vigumu kutofautisha kazi ya Chama kama CHADEMA katika kupambana na ufisadi na Kazi inayofanywa na kile kikundi ndani ya CCM ambacho pia kinajimbambanua kwa jina la wapambanaji wa Ufisadi. CHADEMA inaonekana kusimama katika kuikosoa CCM katika kimatukio zaidi na si katika ki mfumo ambao CCM imeukwaa kwa muda mrefu na inashindwa kujitoa kwani iko ndani mfumo huo.

Sasa hivi naandika haya maoni inawezekana kuna watu wanapanga njama kufanya ufisadi katika ofisi mojawapo ya serikali au sector binafsi. Kuja kutaja jina na mwizi wa leo mwakani inamsaidia nini mtu wa kawaida inayechota maji umbali mrefu au ambaye muda huu amekosa kitanda Mwananyamara hospital kaamua kulala chini wakati mwizi tayari kajenga nyumba, au kahonga Malaya hela yote aliyoiba?

Wakati mwingine inakuwa vigumu kujua msimamo wa CHADEMA kama chama katika mambo ya kitaifa. Kwa mfano ni nini msimamo wa CHADEMA katika shirikisho la kisiasa la Africa mashariki?, Nini msimamo wa chadema katika mambo ya ushoga ambayo sasa yanaoneka wazi yatakuwa gumzo kwenye nyanja ya siasa kwani sasa yananzaa kuingizwa kwa mfumo wa shinikozo.

Ni kipi CHADEMA wanakiami kwenye swala la muungano?. Haya mambo mara nyingi ukiuliza huwa tunapata majibu tofauti tena mengi si majibu bali maoni. Ni bora kuweka mfumo na ideology ambayo chama kinaamini then wananchi wakaelimishwa na wapigia kura wanachokiami.

Kilichopo sasa ndani ya CHADEMA ni wazi kabisa chadema inaonekana kupambana na matendo mabovu ya CCM kwa kutaja jina la mtu mmoja mmoja na hajulikani wazi kama je iwapo CCM itawapeleka mahakamani hao watu na wakifungwa na mahakama kwa uharifu wao baada ya hapo CHADEMA itakuja na issue gani nyingine?

Je itasibiri tena nusanusa wake wavujishe siri zingine ili watu wengine washitakiwe?. Mimi naamini katika hizo strategy ndio zinazopelekea watu kama akina Mayage kufananisha CHADEMA na WANAHARAKATI

CHADEMA ijenge mfumo wa kuingiza maoni mapya na kutoa vitu ambavyo havikijengi chama kwa hivyo itakuwa respiratory system ya chama ambayo itakiweka hai muda wote, bila hivyo chama kinajenga suffocation system kama ya CCM ambayo sasa imejisokota na inashindwa itoke vipi mpaka sasa.

Mfumo uliopo wa ufisadi katika nchi zinazoendea tuna u-underrate sana, ndio maana serikali imeunda chombo kama TAKUKURU ambacho inajua wazi wala hakiwezi tokomeza rushwa. Mfumo wa Rushwa wa nchi zinazoendelea uko very complex, kuna watu wako ndani ya system ya rushwa bila hata kujua.

Hebu fikilia mwanafunzi wa chuo kikuu anayegoma au kuandamana kupinga rushwa wakati ada yake inalipwa na baba, mama au mjomba yake ambaye anapata hiyo ada kwa ufisadi. Hao jamaa wakifukuzwa kazi nini hatma ya huyo kijana?. Je kwa mfumo huo huyo kijana atakaa upande gani katika kupambana na ufisadi?.

Ninammini nchi zetu zinazondelea zinawasomi ambao wanaweza kuja na mfumo mbadala, watu tukae na tuweze kuponder kutafanyeje na tuwe na vyama vya aina gani katika karne hii badala ya kucopy na kupaste siasa ya mataifa ambayo hayazitakii mema nchi zetu kwa kupitia mfumo wa vyama rafiki ambao mimi wala sioni mantiki yake.

Hayo ndio maoni y
 
Mayenga ni miongoni mwa watanzania ambao bado wanahitaji kuelimishwa kuhusu wapi tumetoka, wapi tulipo na ni wapi tuendako. Mayenga Kumbuka kabla ya CDM hakuna mtu hata mmoja alithubutu kuongelea ufisadi na kuikosoa serikali, si magazeti wala vyombo vya habari!

Awali watanzania wengi hakujua nini chanzo hasa cha dhiki na matatizo yao. Pamoja na hayo serikali na chama tawala vilitumia uelewa mdogo wa demokrasia kwa raia kuzidi kutukandamiza na kuvifanya vyama vya upinzani kama ni kwa ajili ya fujo.

Kupitia CDM watu tumeweza kuwa na upeo wa kuyaona maovu na madhaifu ya serikali yetu na kuyahoji. Hatuwezi kukurupuka kama unavyofikiria, Chama kama chama kinajengwa kwa misingi ya watu na kwa mfumo ambao serikali ya ccm ilishauweka nguvu ya ziada ilihitajika ili kutranform watu kutoka kwenye mindset ya chama kimoja kukubali vyama vya upinzani.

Kazi bila kuwa na element za unaharakati huwezi kufaulu. CDM haina dola hilo ilijue, tacts inazozitumia lazima ziwe za ki-uharakati na kisiasa ili kwanza kugain popularity kazi ambayo mpaka sasa imefanywa kwa ufanisi mkubwa. Na kwa kuwa hili limefanikiwa ndo maana unaiona CDM imekuwa chama threat kwa ccm na vyama vyote na kiko tayari kuichukua nchi!

Mayenga just cool down maana wewe naona unakata tamaa na mfumo uliopo ambao kimsingi ni matokea ya jamii legelege ambayo lazima kwanza iwe transformed kama CDM inavyofanya baada ya hapo tutafika wewe unakokutaka. In a mathematical language you can't count 2 before 1
 
Ni vizuri kafanya hivyo!

Sijalisoma bado la yaelekea anajibu kwa kuonyesha postive achievements za CHADEMA na hilo ni kosa!

Mayage kasema chama kina nafasi wafanye zaidi ya walivyofanya sasa! Sasa inaonekana watu hawapendi kukosolewa, hili nalo ni mapungufu ya kiuongozi! Ndo maana Dr Slaa naye hafai kuwa kiongozi wa nchii hii!

Haya ni maoni yangu kama mwana CHADEMA, unafiki kwangu hauna nafasi!!!
kuna jambo linalo kusumbua kuhusu CDM na bado hujaliweka wazi

OK Umeanza kwa kusema amefanya vizuri na unamalizia kwa kusema hafai kuwa kiongozi......which is which..?

Yaekea una ugomvi na Mbowe aua uongozi wa juu wa CDM na sababu za ugomvi huo huzisemi Mwanchama anaye kipenda chama chake muda wote anakuwa tayari kukitetea na kukilinda kwa kuwashauri viongozi wa chama pale unapo ona mambo hayaendi sawa. Kuna njia nyingi zinazo kubalika kichama na mwanachama lazima awe anazijua ili kuwasiliana na viongozi wake

Kwa upande wako naona huna mapenzi mema na chama chako hata kama ni mwanachama ...Kwani Kwenye thread yako ya kwanza ulisema Mbowe hafai na anapaswa kuondolewa ktk nafasi yake na ukasema Dr Slaa anafaa. Leo unasema Dr Slaa hafai nasababu huzisemi

Kimsingi hata kama ni mwanachama ulipaswa kuachia ngazi kwanza ili wengi waendelee mbele watu kama ninyi ndiyo mnao loga chama kisiendelee kwani Uongozi unabaki kuwafikiria unamawazo gani labda mjenga kumbe mnabomoa
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom