Dr Slaa ajibu upotoshaji wa Mwandishi Mayage dhidi ya CHADEMA

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Wakuu,

Nimefurahishwa sana na kitendo cha Dr Slaa kujibu upotoshaji wa Mwandishi Mayage S Mayage.

Hoja kuu mbili za Mayage zilijibiwa;
1. Chadema wanafanya uanaharakati na siyo siasa
2. Anashawishi Chama kipya cha kisiasa kianzishwe ambacho ni makini zaidi ya vyama vyote vilivyopo.

Majibu ya Dr Slaa gazetini ktk gazeti la Raia Mwema la Leo.:

1. Chadema wanafanya uanaharakati na siyo siyo siasa

Dr Slaa alihoji Mayage kushindwa kutoa maana ya siasa na kushindwa kutofautisha vizuri siasa na Uanaharakati. Pia akampa darasa kidogo kuwa uanaharakati ni mojawapo ya mbinu inayotumika wakati mwingine kulingana mazingira husika.

Dr Slaa akamkubusha kuwa uanaharakati huo wa Chadema ndio ulioibua hoja ya EPA, Richmond na Buzwagi. Akatoa ushauri kuwa hansard ya Bunge ya 2007/8/9/10 inatosha kumpa majibu sahihi. Kwenye hansard hiyo atakutana na mambo makubwa mawili. Mosi, Dr Slaa alivyokuwa anapigwa point of Order na kutakiwa kufuta kauli zake kuhusu hoja zake za EPA, Twin tower ya Benki kuu, CIS na nyingine nyingi. Pia tishio la Spika wa Bunge Samwel Sitta kupitia TBC kuwa Nyaraka alizo nazo Dr Slaa (kuhusu ufisadi) ni feki na anaziwasilisha polisi ili ashtakiwe.

Pili hoja ya Buzwagi iliyosababisha Zitto kabwe kusimamishwa Ubunge na matokeo yake yanajulikana. Haya ndiyo matunda ya siasa za Chadema ambazo mwandishi mayage anayaita ni uanaharakati na siyo siasa makini.

Tuanzishe chama makini vilivyopo ikiwepo Chadema vimeshindwa.

Mayage anadai tuanzishe chama makini siyo kwa sababu Chama hicho kipya kina sera mpya bali kwa sababu Chadema wanafanya uanaharakati.

Dr Slaa anafafanua kuwa Chadema ni Chama makini kwa kuwa waliendelea kushikia Bango hoja ya ufisadi hadi leo taifa nzima linapinga ufisadi.

Hili linawezekana tu kutokana na kuwa baada ya Chadema kukwamishwa na Spika Bungeni, walikodi Helikopta wakazunguka mikoa 12 ya Tanzania na kupeleka hoja hizo kwa wananchi kama mahakama kuu kuliko zote kwa wanasisa. Mzunguko huo ulihitimishwa Mwembe Yanga kwa kutaja mafisadi 11. Dr akaendelea kueleza; Hoja za Mayage ingekuwa na Mashiko kama angeenda ktk mikoa hiyo 12 na kuona impact ya hoja hizo za Dr Slaa na Zitto Kabwe.

MAFISADI WENGINE WAKO KORTINI
Dr anafafanua kuwa hakuna anayebisha hata Mayage atakubali kuwa wengiene kati ya watuhumiwa hao wa ufisadi wako kortini kwa kesi zinazohusiana na ufisadi huo.

Makala hiyo ikamalizia:

Bila utafikiti hakuna haki ya kuzungumza (No research, no right to speak)

Makala yataendelea wiki ijayo.
Ndugu Mhariri ni imani yangu kuwa utanipa nafasi nijibu baadhi ya hoja za Mayage zenye sura ya upotoshaji kwa manufaa ya wasomaji wako na Watanzania wenye nia ya kujua ukweli kwa ujumla. Ni imani yangu utachapisha majibu hayo kikamilifu ili upande wa pili wa shilling ufahamike kwa wasomaji wako na wananchi kwa ujumla..
Mimi ni msomaji wa Gazeti letu la Raia Mwema na magazeti na mitandao mbalimbali hivyo kufuatilia mijadala mbalimbali. Kila nilipoona dalili ya upotoshaji nimekuwa nikijaribu kuweka kumbukumbu sawa. Siku za karibuni nimekuwa nikifuatilia makala zilizokuwa zikitolewa na Mayage S. Mayage kwenye Raia Mwema.

Makala ya mwisho ilitoka katika Raia Mwema la Desemba 7 hadi 13, 2011, ukurasa wa 22. Baada ya kusoma makala yake ya kwanza nilimwandikia ujumbe mfupi wa sms. Kimsingi nikimshauri asipende kufanya mahitimisho kwenye mambo mazito na hasa yanayohusu jamii na taifa kwa ujumla bila kufanya utafiti.

Kabla hata toleo la gazeti lililofuata halijatoka nikaanza kupokea simu na sms kutoka kwa watu waliojiita wapenzi wa CHADEMA, wakilalamikia ujumbe wangu wa sms kwa Mayage.

Nilistuka sana na kujiuliza maswali yafuatayo; mosi, kama ni kweli waliokuwa wakiniandikia sms na kunipigia simu ni wapenzi wa CHADEMA walijuaje majibu yangu ya sms kwa Mayage, kabla gazeti linalofuata halijatoka? Je, walipewa na Mayage na kama ni hivyo, kwa lengo gani?

Pili, lugha iliyotumika kwa wote japo walijitambulisha kuwa sehemu mbalimbali za Tanzania ilifanana na hakuna hata mmoja aliyejielekeza kwenye hoja ya msingi kuwa, Mayage ametoa hitimisho bila kufanya utafiti.

Iweje wote wana lugha inayofanana walikaa wapi kujadiliana na kupanga ujumbe wa kunitumia? Iweje wote hakuna anayezungumzia hoja yangu ya msingi, bali msisitizo ni katika walichokiita "kumtukana Mayage? Hili nalo liliashiria upungufu mkubwa kwa kuwa hitimisho lisilotokana na utafiti wa kina daima lina upungufu mkubwa, hasa katika jambo zito kama mikakati ya chama.

Je, watu hao walitarajia mikakati ya chama ingeliwekwa hadharani? Ni jeshi la ajabu linaloweka mikakati yake hadharani? Ni kwa msingi huo, nilitarajia Mayage kama ni mtu makini na mwenye nia njema kama anavyoonekana kutaka kutushauri, angelifanya utafiti aghalab angegundua mikakati au hatua kadhaa zinazochukuliwa na CHADEMA kujiimarisha na kujikita katika ngazi mbalimbali kwa lengo la kuchukua dola 2015.

Je, Mayage anajua kuwa hakuna kanuni moja na inayofanana katika siasa kwa kuwa siasa "is a game of dynamics" yaani ni mchezo wa mbinu na mikakati.

Hata hivyo, hata hao waliosema kuwa nimemtukana au kumdhalilisha Mayage, hawakueleza ni tusi gani ametukanwa. Kutokana na mazingira hayo, nimeona nitoe ufafanuzi ufuatao.

Si mara ya kwanza
Si mara ya kwanza tunajibishana na Mayage, baada ya makala au nyaraka zake. Kwa wale wanaokumbuka alikuwa akiandikia gazeti la Rai. Mayage aliwahi kuandika "Waraka wa wazi kwa Dakta Slaa" katika makala tatu mfululizo na zote zilikuwa za upotoshaji. Makala hizo zilikoma pale nilipomjibu kupitia gazeti hilo hilo.

Katika barua zake hizo niliamini tatizo lilikuwa kutokufanya utafiti, lakini baadaye niligundua kuwa licha ya kutofanya utafiti Mayage alikuwa "kuwadi" wa waliomtuma kwa malengo waliyokuwa wakijua wenyewe.

Jambo hilo alilikiri kwangu kwa sms Mayage mwenyewe, baada ya kuondoka Gazeti la Rai. Nami nikampongeza kwa unyofu na uwazi wake. Kama ni mkweli na mnyofu atatoka hadharani na kukiri mawasiliano kati yetu.

Kwa nini niliandika sms
Niliposoma makala ya Mayage katika Gazeti la Raia Mwema, kwa kutumia saikolojia tu ya kawaida nilijua alikokuwa akielekea ndiyo maana nikamtumia sms bila kutaka kumjibu kwenye gazeti ili ajirekebishe kabla hajafika mbali.

Kwa bahati mbaya, nia yangu njema kwa Mayage ikaanguka kwenye jiwe gumu, badala ya kuanguka kwenye udongo wenye rutuba. Hii haikuwa kwa bahati mbaya, kwani wakati anaanzisha safari ndefu ya makala zake alikuwa anajua alitaka kuhitimisha vipi.

Hii imeonekana dhahiri katika makala yake ya sasa "Ombwe….mbadala wa CCM ni chama kipya". Mengine yote ni kisingizio tu.

Hoja anazotoa kwetu
Hoja zake ni kwanza, CHADEMA ijikite zaidi katika "kufanya siasa badala ya uanaharakati wa maandamano". Pili, wabunge wa CHADEMA wanatakiwa kuja na programu za maendeleo kwa wananchi wa majimbo yao "ili yasije yakakikuta yaliyokikuta chama cha NCCR-Mageuzi.."

Tatu, katika makala yake ya wiki iliyopita yenye kichwa cha habari "Sababu tunayo, tuwang'oe 2015", alitoa sababu mbalimbali na hatimaye alitoa "ushauri kwa wazalendo wenye uchungu wa kweli ….kuanzisha chama cha siasa makini sasa, si kusubiri kesho na Watanzania wakiunge mkono kwa nguvu zote…"

Majibu kwa hoja zake
Mimi sina tatizo na ushauri wa kuanzishwa kwa chama kipya kwa kuwa ni haki ya kikatiba ya Watanzania. Msingi wa kumtaka Mayage kufanya utafiti ni katika upotoshwaji dhahiri wa Mayage, ambaye kwa ufundi mkubwa amejenga hoja kinzani (fallacy) inayoonyesha kuwa CHADEMA si chama makini, hakifanyi siasa makini bali kinafanya tu uanaharakati. Huu ndio msingi na kiini cha kumtaka bwana Mayage afanye utafiti kuhusiana na hoja zake.

Kama hoja za Mayage kutaka kianzishwe chama kipya inatokana na hoja za Richmond, ufisadi na sasa Jairo, na kama angelikuwa makini kidogo na kufanya utafiti kidogo tu angeligundua ni kiasi gani CHADEMA ni ‘chama makini' hadi kujitosa MwembeYanga, Septemba 15, mwaka 2007 na kuibua hadharani (baada ya jitihada za kutumia Bunge kushindikana), hoja za ufisadi wa Benki Kuu, EPA kwa ujumla wake, Twin Tower ya Benki Kuu, Kagoda, Ufisadi kupitia Commodity Import Support (CIS) na nyingine nyingi.

Inatosha kufungua kumbukumbu rasmi za Bunge (hansard) za mwaka 2007/2008/2009/2010. Msomaji na mfuatiliaji makini anaona wazi kupitia hansard jinsi Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, alivyokuwa akipigwa "point of order" kutakiwa kufuta sehemu ya hotuba yake na Spika, bila shaka kwa lengo la kuuficha ukweli usijadiliwe bungeni.

Mayage atakumbuka jinsi Spika wa Bunge, Samuel Sitta alivyokimbilia TBC1 na kutangaza kuwa "Nyaraka alizokuwa nazo Dokta Slaa (kuhusu ufisadi) ni feki na kuwa anaziwakilisha polisi ashitakiwe".

CHADEMA hatukutetereka
CHADEMA ilishikia bango bila kutetereka, pamoja na vitisho na matusi yote hoja hizi sasa zinajulikana, taifa zima leo linajua ufisadi mkubwa unaokumba nchi yetu katika nyanja mbalimbali.

Leo taifa nzima linaimba na kupinga ufisadi. Hii iliwezekana tu, kwa kuwa baada ya jitihada za bungeni kushindikana CHADEMA, kwa kukodi helkopta ilipita kwenye makao ya mikoa 12 ya Tanzania Bara na kupeleka hoja hizo kwa wananchi, kama Mahakama Kuu kuliko zote kwa wanasiasa. Mzunguko huo ulihitimishwa MwembeYanga kwa kutaja hadharani majina ya mafisadi 11.

Mafisadi wengine wako kortini
Hakuna anayebisha, na hata Mayage atakubali kuwa wengine kati ya watuhumiwa hao wa ufisadi leo wako mahakamani kwa kesi zinazohusiana na ufisadi huo.

Mayage anasema CHADEMA kinafanya kazi "ki uanaharakati" angelifanya utafiti kidogo tu angelijua matokeo ya uanaharakati huo kwa siasa za CHADEMA na kwa siasa za Tanzania baada ya MwembeYanga.

Kwenye sms niliyomtumia nilitumia neno kwa mtu yeyote anayefikia hitimisho (conclusion) bila utafiti ni ‘uvivu wa kufikiri' na bado nitasimamia hapo kwa kuwa kuacha hoja ya Mayage bila kupata majibu ya kina tutaruhusu upotoshaji unaozidi viwango vyote.

Aidha, Mayage ameshindwa kutoa tafsiri ya neno ‘siasa' badala yake anaona kinachofanywa na CHADEMA ni ‘uanaharakati' tu, na hivyo anawashawishi "Watanzania kuanzisha chama cha siasa makini".

Waanzishe chama makini siyo kwa kuwa chama hicho kipya kina ajenda mpya bali kwa vile tu CHADEMA si makini na kinafanya kazi "ki-uanaharakati".

Mayage anashindwa kuchambua kwa kina uhusiano wa karibu sana kati ya uanaharakati na siasa. Anashindwa kuona kuwa uanaharakati inaweza kuwa mbinu mojawapo (wakati mwingine ya lazima) ya kufikia malengo ya kisiasa.

Hoja ya Mayage ingekuwa na mashiko angelikuwa amepitia mikoa yote 12 ambako CHADEMA ilifanya mikutano ya hadhara (uanaharakati) na kulishitaki Bunge kuhusiana na ufisadi wa Buzwagi, hoja ya Kabwe Zitto iliyolifanya Bunge kumfukuza Zitto, bungeni kwa miezi takriban mine, na kuwaeleza kinagaubaga Watanzania ni nini matokeo ya mikutano hiyo kwa Watanzania na matokeo yake (impact) kwa siasa za Tanzania leo. Bwana Mayage alipaswa kukumbuka msemo kuwa bila "utafiti hakuna haki ya kuzungumza"(No Research no right to speak).


Itaendelea
PS: Awali mwandishi huyu alishapingwa na mwana JF mmoja hapa - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...mayage-s-mayage-umepotoka-hatudanganyiki.html
 
Nimesoma hiyo makala ya Dr.Slaa kwenye gazeti la Raia Mwema,amemjibu vizuri sana tena kwa busara na hekima,na huyu mwandishi kabla ya kuwa raia mwema alikuwa anaandikia gazeti la Rai,alisahawahi kuandika upupu mwingine kama ambao ameuandika kwenye gazeti la Raia mwema,Slaa alimjibu na mwandishi arikubali kupotoka.
 
Ni vizuri kafanya hivyo!

Sijalisoma bado la yaelekea anajibu kwa kuonyesha postive achievements za CHADEMA na hilo ni kosa!

Mayage kasema chama kina nafasi wafanye zaidi ya walivyofanya sasa! Sasa inaonekana watu hawapendi kukosolewa, hili nalo ni mapungufu ya kiuongozi! Ndo maana Dr Slaa naye hafai kuwa kiongozi wa nchii hii!

Haya ni maoni yangu kama mwana CHADEMA, unafiki kwangu hauna nafasi!!!
 
Huyu Mayage Mayage ni mfia tumbo. Sidhani kama ana capacity ya kuishauri CHADEMA ktk siasa. Mambo yanayofanywa na CHADEMA yapo juu ya uwezo wa Mayage wa kufikiri. Lkn kwa kuwa riziki ya Mayage inapatikana kwa kuandika Makala, Mayage anaamua kuandika kuhusu CHADEMA kwa kuwa anajua ndio itakayouza.

Mayage ni mfano wa Watanzania wengi wasiojua tunataka nini. Kama Tafsiri ya SIASA kwa Mayage ni kuongea uongo majukwaani na kuacha wananchi waumeze, basi Mayage ajue kuwa ndani ya CHADEMA siasa ni mchakato mzima wa KUIBUA, KUSIMAMIA NA KURIPOTI yale yote yanayoihusu nchi kwa manufaa ya wananchi.

Kwa kuwa ndugu yetu Mayage tumbo ndio linalomwongoza, hatupaswi kumchukia badala yake tumshauri. Na mimi binafsi ushauri wangu kwa Mayage ni kuanza kuandika Makala za CUF ambao wameonesha potentials zao za siasa za kisomali pale Manzese. Siasa za CHADEMA sio level yako, otherwise uwe na cheti kama cha Nape cha kuongea utumbo.

Wako ktk kurudisha hadhi na heshima ya tasnia ya habari,


Shizukan
 
Safi sana Dk Slaa. Nimefurahia ulipoonyesha unafki wa Sitta waziwazi katika bunge la tisa.
 
Wakina Dr. tunawahitaji sana,kipindi hiki ambapo tunaona mambo
hayaendi.
 
Ni vizuri kafanya hivyo!

Sijalisoma bado la yaelekea anajibu kwa kuonyesha postive achievements za CHADEMA na hilo ni kosa!

Mayage kasema chama kina nafasi wafanye zaidi ya walivyofanya sasa! Sasa inaonekana watu hawapendi kukosolewa, hili nalo ni mapungufu ya kiuongozi! Ndo maana Dr Slaa naye hafai kuwa kiongozi wa nchii hii!

Haya ni maoni yangu kama mwana CHADEMA, unafiki kwangu hauna nafasi!!!
Nafasi ya chama kufanya zaidi hutolewa na wananchi na chama hakina uwezo wa kuinyakua. Kama umekiri kuwa kwa kiasi fulani wamefanikiwa na unaamini wanahitajika kufanya zaidi, suala sahihi la wewe kufanya ni kuunga mkono yale yaliyofikiwa ili ridhaa ya wananchi ipatikane, wapewe dola na waweze kufanya hiyo zaidi unayoitaka.

Kuna tofauti kubwa kati ya kukosoa na kuponda. Usipoijua hiyo tofauti utagombana na mama mkwe wako. Mayage ameconclude kwenye makala yake kuwa solution ni kuanzishwa chama kingine, huu ni ukosoaji? Yawezekana huna nia mbaya ktk comments zako, lkn yaelekea huna akili pia. Ni nini unachohitaji wewe kama mwananchi, siasa za kubwabwaja majukwaani na kusubiri uchaguzi au chama kilicho active wakati wote kikiwatumikia wananchi?

Uanaharakati ndio hasa msingi wa mabadiliko chanya ktk mataifa ya kidemokrasia. Ndio njia ya kupata haki toka kwa watawala dhalimu. Shida yetu watanzania ni uoga wa mabadiliko. Badilika kimtazamo, acha uoga na unga mkono harakati hizi za CHADEMA. Tanzania haitakuwa huru kwa uwakilishi wa wabunge wanaoorodhesha msululu wa matatizo ya majimbo yao halafu wamalizie kwa 'naunga hoja mkono kwa 100%'.

Na kama shida yako ni yale yanayohubiriwa majukwaani na CHADEMA, labda nikuulize: Ulitaka wajadili nini zaidi ya yale yanayotukwamisha tusiendelee?

Kuna kingine kinachotukwamisha zaidi ya ufisadi, mikataba mibovu, wizi wa rasilimali, uwajibikaji mdogo, kujuana na kufumbiana macho tunapokosea?

Ni vyema wananchi tukaaacha upuuzi, hizi nguvu za kuisakama CHADEMA tungeielekeza kwenye kuisakama serikali iwachukulie hatua wanaotufilisi. Kama tutagoma kushiriki harakati na kukaa tusubiri kuanzishwa kwa chama kitakacholeta maajabu kwa kukaa ofisini na kukomesha mabaya haya, basi hatutakuwa na tofauti na Mayage anayewaza kwa kutumia tumbo.
Wako ktk kupinga mambo ya kijinga na ukosoaji usio na mashiko,

Shizukan
 
Ni vizuri kafanya hivyo!

Sijalisoma bado la yaelekea anajibu kwa kuonyesha postive achievements za CHADEMA na hilo ni kosa!

Mayage kasema chama kina nafasi wafanye zaidi ya walivyofanya sasa! Sasa inaonekana watu hawapendi kukosolewa, hili nalo ni mapungufu ya kiuongozi! Ndo maana Dr Slaa naye hafai kuwa kiongozi wa nchii hii!

Haya ni maoni yangu kama mwana CHADEMA, unafiki kwangu hauna nafasi!!!

Wewe ni fisadi tu, huna jpya kwa maana bado unaunga mkono ufisadi na kama unampinga Dr Slaa kwa hoja alizotoa utamkubali nani awe mkuu nchii, wewe uwezo wako wa kufikiria na kuchambua mambo na kuyaelewa ni mdogo sana kuliko kawaida....

Unasema Dr Slaa hafai kwa maana ipi? au ulitaka akubaliane na hoja za kipuuzi za huyo mayage ambazo zinapingwa na watanzania wengi?.....

acha upupu na wewe ni wale wale ambao waTZ wanawapiga vita.
 
Ni vizuri kafanya hivyo!

Sijalisoma bado la yaelekea anajibu kwa kuonyesha postive achievements za CHADEMA na hilo ni kosa!

Mayage kasema chama kina nafasi wafanye zaidi ya walivyofanya sasa! Sasa inaonekana watu hawapendi kukosolewa, hili nalo ni mapungufu ya kiuongozi! Ndo maana Dr Slaa naye hafai kuwa kiongozi wa nchii hii!

Haya ni maoni yangu kama mwana CHADEMA, unafiki kwangu hauna nafasi!!!

Mayage ni njaa tu inasumbua mkuu anajipendekeza ili apate mkate wa siku toka kwa anaowakuwadia.Pole ndugu kama ndiyo uwezo wako wa kuijua siasa umeishia hapo.Ila ni haki yako kutoa mawazo keep it up.
 
Siku zote CHADEMA tunasema ni chama makini chenye viongozi mahiri katika kujenga hoja, DR ndiye mwasisi wa mapambono dhidi ya ufisadi na chama chetu kitaendelea kusimamia ukweli huu Huyu mwandishi anatakiwa atambue kuwa watanzania wanatambua kuwa chadema ndiyo mkombozi wa uchumi wa tanzania na Tanzania tunayoitaka (Tanzania we want)
 
Nyie CHADEMA ni watu gani msiotaka kukosolewa???? Mayage katika makala yake aliwakosoa na kuwataka mfanye vizuri zaidi lakini mmeigeuza makala yake kuwa ugomvi kana kwamba amewatukana matusi ya nguoni. Ni nyie mnaolalamika hali ya nchi kwa sasa na kuhoji kama kweli Rais ana washauri. Nyie mnaukataa ushauri wa Mayage, je huyo Padri wenu aliyeasi akiingia Ikulu atamsikiliza nani?
 
Safi sana Dr Slaa, Mayage alitukela watz wengi wenye uelewa.
 
umefanya vema sana kumweleza ukweli mayage! inabidi watanzania tuamke na kukazania maendeleo yetu zaidi na si kupinga tuu bila kufikiri!
 
Huyu Mayage Mayage ndio nani? Sijawahi kumsikia au kumsoma popote. Kama kuna mtu ana profile yake atumwagie hapa ili tuone kama ana sifa za kutosha kubishana na Dr wa ukweli.
 
Back
Top Bottom