Jamani huyu Meneja anaitwa Jacob Sumary ni ndugu yake na Sioi Sumary aliyegombea ubunge na Joshua Nassary huku Arumeru Mashariki, Nasary alivyompiga chini Sioi kwa ushirikiano mkubwa kabisa na viongozi wote wa CDM akiwemo Dr. Slaa sasa huyo Meneja ndo kalipa kisasi kwa njia hiyo. Nadhani kajidanganya coz Dr atalala popote mpaka kitakapoeleweka
Uo ni ubabe wa kishangingi, inafurahisha kuona kila mtendaji anafikiri anafanya kitu ili kuidhalilisha cdm kumbe ndo wanakiaribia chama tawala.
...Unajua katika ajira za SU kama VETA ambapo huenda huyo meneja alichomekwa tu hapo basi anakwenda kwa amri za wabwana wakubwa tu. Anakosa hata ujasiri wa kuhoji kwa nini mteja aliyelipiwa chumba ghafla aondolewe kwa kisingizio kuwa mteja mwingine amelipia.....Ni udhaifu unaowatafuna magamba....:eek2:jamaa hana skills za biashara...
Kuwabadilisha enyi wajinga na Wachumia-tumbo wote
Pia katika hatua nyingine umeme ulizimwa mji mzima wa Mikumi jana kuanzia asubuhi hadi usiku katika kile kilichoonekana ni hujuma ya Tanesco ili Dr Slaa ashindwe kuhutubia,hata hivyo mbali na kukosekana umeme mikutano ya Dr Slaa ilifurika umati mkubwa wa watu huku kiongozi huyo akiwaambia maelfu ya watu atawahutubia hata bila vipaza sauti.
Spot on........Haya ndio matatizo la kuchanganya siasa na uchumi. Kwa kumtendea visivyo Dr. Slaa, je huyo meneja ameonyesha ukomavu wa kutaaluma? Je, amevutia wateja au amewafukuza?
Kwa kuzima umeme siku nzima ili kumkomoa Dr. Slaa, umesimamisha shughuli zenye thamani kiasi gani ambazo utekelezaji wake huhitaji nishati ya umeme? Kwa utendaji huu, tusitegemee maendeleo yoyote.